TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

M
Mambo ya bunge live ni kuleta uchochezi tu,ndo maana hata mataifa makubwa yenye democracy kubwa kuliko sisi hakuna mambo ya bunge live,
jk alitudekeza sana,,sasa hivi NI KAZI TU
ataifa gani hayaonyeshi live achene ushamba if you are not informed just shutup don't tell lies
 
Sisi wananchi ndio tunalipa kodi kuiendesha TBC. Tunataka tuone live kazi za wawakilishi wetu bungeni. Serikali isiwe na uoga kupitiliza hadi kutunyima haki hii muhimu na wala Tanzania ya Magufuli si masikini kiasi hicho.
 
Mlishaambiwa na Kikwete kuwa Magufuli ni mkali. Sasa mnaia lia ini?
Hakuna anaelia ila watu tunasikitika kwsbb wanashindwa kufikiria. Km unaweza kuiachia TBC2 inagonga mziki 24/7 mwaka mzima halaf bunge linaloitaji wiki mbili unashindwa kurusha live. Kama ni kupunguza gharama wazime TBC2
 
Nchi za Ulaya na America! Bunge zao zina Television ziitwazo televisheni za bunge!. Sisi atujafika huko, tulitakiwa tujikongoje live na hii tulionayo!. Ila ndo hivyo tena!.
 
Poleni sana wakuu naona nape kawatouch sana,lakini nahakika sio uamzi wake pekee.

Zama za kuuza sura kwenye luninga zimepita,NI KAZI TU
 
Kwa nilivyoona leo wanavyozomea bora tu wasitishe labda itasaidia wabunge kuwa makini maana wengine alitumia nafasi hiyo kuwa maarufu kwa kutukana kuzomea na kufanya vituko wakijua kesho wataandikwa magazeti na kuongelewa kila kona
Safi sana Magufuli
hapa kazi tu
 
Teh teh teh JF kuna wanafiki wengi mbona walio kuwa wanaiponda TBC na kusema huwa hawaangalii hio Channel Leo ndo wanatokwa na povu hapa na kulalamika hadi mishipa inatoka

Si mlisema nyinyi hua mnaangalia ITV, TBC Inapendelea Leo mbona mmeipenda ghafla

Kweli nimeani Ng'ombe haoni umuhimu wa mkia wake hadi pale utakapo katika ndo anaona umuhimu wa mkia
 
Tuangalie pande zote za shillingi , kama kweli tunataka kubana matumizi , gharama za uendeshwaji wa bunge pia unatakakiwa udhibitiwe. Hii itahusisha posho zao na masurufu mbali mbali lakini hata matangazo
Billion 4 kwa kutangaza nini ? Hakuna cha maana zaidi ya maigizo bumgeni. Kwani kama kuna jambo la maana kufanyika lazima lioneshwe live.
Ni mambo mangapi yaliyorushwa live yalileta ufanisi? Msimamo juu ya muswada Fulani hauhitaji kurushwa live au la ndiyo usimamiwe vilivyo na wabunge. Wajibu wao ni kuwatetea wanancha wakionekana au bila kuonekana.
 
Kiukweli JK II ana mazuri aliyoyafanya tusiyaone mabaya tu vyombo vya habari vilipewa uhuru kweli kweli yaani vilikuwa vinavuka hadi mipaka na yeye alikuwa anatabasamu tu kama kawaida yake tena hadi kuna vyombo vya habari vimefungiwa juzi kwamba vimefunguliwa kiholera holera bila vigezo lakini enzi za JK vilikuwa vinafanya tu kazi lakini bado kuna watu walimponda JK kwamba ananyima uhuru wa vyombo vya habari kuna siku JK alisikitika kweli kwamba na akafafanua ananyimaje uhuru wa vyombo vya habari wakati serikali ina redio 1 tv 1 redio za binafsi kibao , tv za binafsi kibao , magazeti chungu nzima...kiukweli tutamkumbuka JK II
 
Siku ile MV spice ikizama, TV binafsi zilikuwa zinaonyesha hayo matukio Live, lakini TBC ilikuwa ikionyesha muziki wa Taarab.
 
Back
Top Bottom