Elections 2010 TBC1 waonyesha picha za wakimbizi kunani?

matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,052
242
Wanajamvi leo TBC wamekuwa wakionyesha sana documentary ya wakimbizi wa Congo waliopo hapa kwenye kambi zetu za hapa nchini. Nimeona documentary saa sita mchana na saa tisa alasiri.

Je ni zile mbinu za 1995 za Mkapa kuwatisha watanzainia waogope kuchagua upinzani??

:confused2:
 
:doh: sijui hii nchi yetu inaelekea wapi.... wanadhani kuonyesha vipindi vya wakimbizi ndio solutions sio solution ni kuwaacha wananchi wachague kwa haki yao kiongozi wanayemtaka hata wakionyesha mauwaji ya kibari bado haitosaidia kitu kwani watanzania wa leo sio wa juzi wameamka wanauelewa wa yote wanayo yafanya hivyo hao TBC na Vibaraka wao imekula kwao, jumapili 31/10/2010 tunatoa ajira mpya kwa
Orginal Dr. W.P.Slaa
 
Nothing is permanent, except change. This is the right time for change in TZ. With or without the documentaries changes are inevitable.
 
Duh, hawa ndo wakuanza nao kuwalipua na mibomu, kwanza wakose hizo ofisi then wanaofanya kazi hapo nao waende mbele za haki mapema. Hawana uchungu wala hawaoni kipi cha kufanya, tunakatwa kodi kwa ajili ya kuendesha hicho kituo cha umma. Its too sad, TBC1 ni kama wahuni fulani wasioenda shule.
 
Hivi leo hii ni mtanzania gani utamtisha kwa documentary?Mi nakumbuka enzi za vyama vingi vinaanza ndo watu walikuwa na hofu kuwa upinzani ni vita.Leo hii watu wanajua ukweli na wameelimika.Wanajisumbua tu....
 
Leo imeonyesha TBC huko congo hakuna mizengwe!, Generali Ulimwengu alionyesha yaliyojiri kule Zenji kwenye channel ten, wakamwita sio raia. waache wacongo na congo yao, sisi tunataka changes, miaka nenda rudi upuuzi ni uleule kama nchi ya kifalme. sasa wameanza kuwaanda watoto wao kwa nguvu zoote!!.
Titakuja toana roho mchana mchana hapa jamaniii!!
 
Wanajamvi leo TBC wamekuwa wakionyesha sana documentary ya wakimbizi wa Congo waliopo hapa kwenye kambi zetu za hapa nchini. Nimeona documentary saa sita mchana na saa tisa alasiri. Je ni zile mbinu za 1995 za Mkapa kuwatisha watanzainia waogope kuchagua upinzani??:confused2:

Mwaka 1995 ilikuwa imepita miaka mi3 tangu tutiwe changa la macho kuwa "vyama vingi vitaleta vita". Ilikuwa ni rahisi sana kurubunika.

Kwa sasa watafulia tu na hizo picha zao. Bora waoneshe "Kijiweni Sesami" wadanganye watoto.
 
hata wakiweka filamu ya ESCAPE FROM SOBIBOR...moto ni ule ule... Halafu nimesikia pande za Iringa huko daladala zote zilizowekewa bendera ya sisiemu zimepewa "ofa" ya kutokamatwa na Traffic mpaka uchaguzi uishe!! sijui imekaaje hii...atakaepata taarifa zaidi embu atumwagie hapa!!
 
Mkimbizi ana tofauti gani na mtanzania anayetembea toka asubuhi mpaka jioni akitafuta chupa za plastiki auze ili wanae wale, anatofauti gani na mtanzania anayepiga kelele asubuhi na jioni vituoni kuita watu wapande dalalala, ili wanae waende shule, anatofauti gani na wakinadada wanaokesha macho kutafuta hela angalau mkono uende kinywani.

Mkimbizi ana tofauti gani na mama anayelala chini hospitali akienda kujifungua hospitali ya serikali, anatofauti gani na baba anayeenda hospitali akiwa na malaria na kuambiwa hatibiwi mpaka alipe hela na kununua dawa, mkimbizi ana tofauti gani na mtanzania ambaye mtoto wake anashindwa kwenda shule ya msingi na kwa bahati akifaulu anashindwa hata kumlipia ada na akienda chuo kikuu hapewi mkopo na badala yake anayepewa mkopo wa kiwango cha asilimia 100 ni mtoto aliyesoma St. Something.

Mkimbizi ana tofauti gani na mfugaji wa kitanzania anayehamishwa kwa sababu eti ardhi aliyopewa na babu zake wanapewa mfalme wa uarabuni.

TBC amkeni watanzania wengi wamekuwa wakiishi maisha ya ukimbizi ndani ya nchi yao kwa muda mrefu sana nadhani wakati umefika wa kuondokana na ukimbizi huo.

Tambueni kama kweli mnaonyesha mnachoonyesha ndio maisha halisi ya watanzania, ila tatizo mlikuwa mko isolated sana na maisha ya kawaida ya Mtanzania.
 
Mabadiliko hayaogopi! Najaribu kuwapigia na kuwashauri waonyesha za "Romania"! Simu hazipokelewi!:doh:
 
Watachelewesha mabadiliko, lakini hawawezi kamwe kuyazuia! Mama wa kwanza mwenyewe anashangaa kila anapopita anaoneshwa alama za vidole za "V," sasa kuna kazi tena hapo?
 
Wanajamvi leo TBC wamekuwa wakionyesha sana documentary ya wakimbizi wa Congo waliopo hapa kwenye kambi zetu za hapa nchini. Nimeona documentary saa sita mchana na saa tisa alasiri. Je ni zile mbinu za 1995 za Mkapa kuwatisha watanzainia waogope kuchagua upinzani??:confused2:
Unfortunately tuna chini ya silimia kumi ya watu wenye kuona TV kutokana na umaskini uliokithiri
 
Back
Top Bottom