TBC yapaswa muwajibike kwa kuruhusu Hotuba ya Slaa inayotetea Ufashisti

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,837
Nimeisikiliza hotuba ya Dk Slaa kuhusu Legacy ya Magufuli, sikatai kuwa Magufuli ana mambo mazuri na ana legacy yake inayopaswa kuenziwa, lakini alikuwa na mapungufu mengi ambayo hata wana CCM wenyewe wanakubali, na Rais Samia mabye ndiye mwenyekiti wa CCM na Rais kwa sasa anarekebisha mabaya ya Magufuli

Sasa Dk Slaa alipaswa kujikita kwenye m,azuri ya Magufuli na kuyaacha yale mabaya na sio kulazimisha kutetea mabaya

Kwanza kabisa Slaa anaanza kwa kuilamumu Serikali ni kwa nini ilikaa kimya kuhusu Magufuli kuugua, anailamu serikali ya sasa huku akijua Magufuli na serikali yake ndiyo ambayo ilikuwa ikiendesha mambo kwa usiri na propaganda, Serikali yake tunakumbuka ilivyoingiza propaganda nyingi kwenye ugonjwa wa Covid na waliokuwa wakifariki kwa ugonjwa huo walisemwa wamefariki kwa changamoto za kupumua

Slaa anaenda tena kumtetea Magufuli kuhusu mauaji ya watu, na kusema pia mbona Ulaya watu pia wanauawa, sasa Ulaya watu wakiuawa ndio inakuwa excuse ya kuua?

Slaa pia anatetea uamuzi wa Magufuli kuhusu kubambikiza watu kesi na kusema pia kipindi cha Kikwete kuna watendaji wa vijiji walikuwa wakibambikiza watu kesi, jamani baya linahalalisha baya? ameshindwa kujikita tu kuelezea mazuri badala ya kulazimisha kumsafisha?

Slaa ameonekana pia kuunga mkono uamuzi wa Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopatga mimba kurudi shule na kusema hata Ulaya walikuwa wanafanya forced sterlization, sasa inahusiana vipi?

Slaa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Upinzani anasema Magufuli anasemwa alikuwa sio mwanademokrasia lakini alipendwa na wanyonge na hilo ndio la muhimu, kweli? sasa alijiunga na upinzani ya kazi gani kama demokrasia haina umuhimu?

TBC kuweni makini, msomeni Samia kwa sasa anataka nchi yenye amani, siasa safi na maendeleo, ufashiti tulishaachana nao
 
Slaa anaenda tena kumtetea Magufuli kuhusu mauaji ya watu, na kusema pia mbona Ulaya watu pia wanauawa, sasa Ulaya watu wakiuawa ndio inakuwa excuse ya kuua?

Slaa pia anatetea uamuzi wa Magufuli kuhusu kubambikiza watu kesi na kusema pia kipindi cha Kikwete kuna watendaji wa vijiji walikuwa wakibambikiza watu kesi, jamani baya linahalalisha baya? ameshindwa kujikita tu kuelezea mazuri badala ya kulazimisha kumsafisha?

Haya maelezo ni ya kweli? Basi mleta mada au Moderator muwajibike kuweka video tujiridhishe kama kweli Dr.Slaa aliongea huu ujinga
 
Humjui Slaa wewe, unakumbuka alisema nini kuhusu Lissu kupigwa risasi?
 
Shida ya watu wengi humu ni kudhani kuwa Jf ndio nchi(Tanzania), kwamba kupitia wimbi la nyuzi mbalimbali zilizoanzishwa humu za kupondea kila kitu kilichofanya na JPM basi wamemaliza.

Acheni watu watoe maoni yao kama jinsi nyinyi mnavyoanzisha nyuzi humu, kila mmoja ana msimamo wake juu ya JPM.

HUYU atamchukia,YULE atampenda na ndo kanuni ya maisha popote pale.
 
Ametumika vya kutosha,aliyemtumia hayupo.
Kuna uwezekano kaishapata fununu mother anamtema,
Analialia nini sasa?,
Dhambi ya usaliti inamtafuna,na mimi naomba iendelee kumtafuna tu period...
Ule wa kumpa Lowassa Go ahead baada ya kumuimba kwa muda mrefu kuwa ni fisadi, haukuwa usaliti??

Ulitaka Slaa akubaliane na mtu ambae amekemea kwa miaka kadhaa? Yeye alionyesha msimamo wake, na hata hivyo baadae huyo Lowassa hakubaki CDM sasa hapo mwenye akili ni nani?

Dhambi ya usaliti itamtafuna Mbowe.
 
Back
Top Bottom