TBC inapoteza wafuatiliaji kwa mambo ya kujitakia wenyewe

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Mwanzo nilikuwa sina uhakika sana kama TBC TANZANIA inafatiliwa na inawasilizaji wengi sana . ila baada ya kutazama interview ya Salama na Oscar Oscar.

ndo nikajua na nikathibitisha kuwa Tbc Tanzania ina wasikilizaji wengi sana.

nadhani na nilitajia kuwa TBC TANZANIA ingekuwa mfano bora kwa Boardingcasting Corporation kwa hapa Tanzania.

na hata likitokea tukio lolote lile la kitaifa kama msiba na majanga ya kitaifa wananchi ukimbilia kuwasha Tv ukimbilia kutazama TBC TANZANIA na Usikiliza TBC FM ndio chombo cha habari cha Taifa. lakini cha ajabu TBC wenyewe sijui wamekufa au labda bado wapo mwaka 1920 wakati sisi tupo 2022.

Baada ya kuingia mtandaoni jana na kukutana na tukio la ajali ya ndege ya kampuni ya Precious Air. kitu cha kushangaza zaidi Millard ayo alikuwa kashapost , Sky news walipost CNN na pia aljazeera wamerepoti tukio la ajali ya ndege .

Tanzania kabla ya hata TBC TANZANIA kufanya hivo.

Mwaka 2011 Meli ilizama Zanzibar CNN ikawa breaking news asubuhi, Jumapili.

TBC TANZANIA walikuwa wanapiga taarabu...huko ndiko kuna PhD holder wa nadharia ya uandishi wa habari.

nikajua labda kutokana na mapungufu na makosa ya mwaka 2011 watakuwa wamedeveloped.

Lakini hali imekuwa mbaya zaidi wakati tukio la ndege ya precision air inapata ajali tukio lilitokea jana asubuhi. vyombo vya habari hadi vya nje vilikuwa vinaripoti breaking news,wakati TBC TANZANIA walikuwa na kipindi cha kwaya na baadaye wakaweka kipindi cha mapishi.

Tukio limetokea asubuhi mida ya saa 2 asubuhi wakati TBC TANZANIA wanareport tukio saa 7 mchana huko.

nashindwa kujua na nakosa majibu pia hivi TBC TANZANIA haina mareporter TANZANIA nzima ?

na sio TBC TANZANIA peke yake infact ni mainstream media zote za Tanzania wameonesha irresponsibility kubwa sana.yaani tukio limetokea asubuhi wanasubiri watuletee zile taarifa zao za habari zilizohaririwa za saa mbili usiku.

kiufupi bado nitaurahumu jeshi la uokoaji.

hauwezi kumwambia ndugu wa marehemu kauli ni mipango ya mungu akakuelewa. ( Wasovieti wanaelewa hapa namaanisha nini). jeshi la polisi lilifika lakini walikaa pembeni tu na zipo baadhi ya picha zikiwaonesha wakiwa wamesimama kuwatazama wananchi waliokuwa wanavuta ndege kwa kamba.

Pia natupa lawama TBC TANZANIA zaidi kuliko hata media nyingine kwa sababu TBC TANZANIAni chombo cha umma wanawajibu zaidi.

Uwenda labda habari zinatolewa kwa maagizo maalumu, hadi ruhusa itoke juu inaonesha wazi hakuna uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hii.

VIKOSI VYA UOKOAJI NA TBC TANZANIA munatakiwa kubadilika sasa.
 

Attachments

  • status_me_status_25ceede2-47fe-429f-a363-bdbee9b28b22.mp4
    1.9 MB
  • %23BREAKING_Vyombo_vya_Ulinzi%2C_Usalama_na_Uokoaji_kwa_kushirikiana_na_Wananchi_wamefanikiwa_...mp4
    625.8 KB
Kuna laana kwenye mwenge. Ukiiuhusisha na mambo ya mwenge unakuwa sehemu ya laana na maisha yako yote huzuni itakuwa ni sehemu yako.

Isaya 50:11
[11]Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Behold, all ye that kindle a fire, that compass yourselves about with sparks: walk in the light of your fire, and in the sparks that ye have kindled. This shall ye have of mine hand; ye shall lie down in sorrow.
 
Hebu ngoja kwanza unasema
20221104_095105.jpg
 
Kwan kuna shida gan?
As long as salary slip inasoma mwisho wa mwezi hawaoni cha ajabu
 
Bila kusahau Ndiyo Local Channel pekee itakayoonesha Kombe la Dunia...

Hapa wata,amaji watakuwa wengi
lakini hapo ni kwenye entertainment kuna watu kadhaa sio wote wanaofatilia football lakini kuna habari za seriouz zinazofatliwa na watu weng zaidi mbona hazipew kipaumbele
 
Kuna laana kwenye mwenge. Ukiiuhusisha na mambo ya mwenge unakuwa sehemu ya laana na maisha yako yote huzuni itakuwa ni sehemu yako.

Isaya 50:11
[11]Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Behold, all ye that kindle a fire, that compass yourselves about with sparks: walk in the light of your fire, and in the sparks that ye have kindled. This shall ye have of mine hand; ye shall lie down in sorrow.
🤔🤔🤔🤔😭
 
Back
Top Bottom