Tetesi: TBC hakukaliki, muda wowote Zuhura Yunus anakuja na mkeka!

Kheeeeeee meli mwanza hadi Zambia 🤔🤔 au hiyo meli itakua inapaa angani kama ya kwenye the avengers wa marvel studios 😁😁
 
Samahanini nipo nje ya mada ila hili ni jambo zuri pia

KAMA UNATUMIA TIGO BORA UTOE 40K ILA UOKOE HELA UNAZONUNUA DATA&DK KWA MIAKA 2 (GB48 KILA MWEZ+DK 2000)*

Watumiaji wa tigo njoo nikuunge huduma hii uwe unapewa gb 48 na dk 2000 kila mwezi kwa miaka miwili, huduma hii sahivi unaungwa pekeyako na sio kikundi.

Uhakika na usalama wapesa yako ni 100% mana hela unailipa direct Tigo kama unavyojiunga na vifurushi vingine, mm nakupa maelekezo tu ya kujiunga, ( ukijiunga nalipwa na tigo ).

kama ukitaka kujiridhisha nikishakupa maelekezo unaweza kupiga 100 uulizie ujiridhishe kabla ya kulipia.

PIA KUNA GB35+1000DK KILA MWEZ KWA 30K, MUWE WATU WAWILI.

HUNITUMII HELA YOYOTE HATA MIA!

Karibu hata uniulizie tu nikupe maelekezo bure!

KAMA UKITAKA TUKUTANE TUFANYE KAZI LIVE PIA INAWEZAKANA

NITEXT WHATSAPP

0717700921
 
kwani huyo kikwekwe sijui kikeke ndio ataleta impact gani na yeye wale wale tu, haina maana kukaa ulaya BBC ndio unajua kila kitu, kimsingi ni mweupe tu mtu anayeweza kutangaza sio lazima awe kiongozi, tiibiisiisiimeu wana matatizo mengi ya kimfumo hata umweke paka pale anaweza kuongoza kwani wanakua sio wao wanaendeshwa na remote kutoka magogoni.
 
We Sheikh Yahaya, Mzee Wa kuwachafua, uliishia wapi na huu uchafu wako

View attachment 2948917
Tetesi zinaelekeza Salim Kikeke anaendelea kutajwa kumng'oa Ayub Rioba alijizindika pale TBC. Hii ni baada ya chombo hiki cha Wananchi kushindwa mambo mengi na kufuja fedha za umma huku Watumishi wake wengi wakijianzishia makampuni shindani na TBC. Ukichukua TIN za Watumishi utashangaa wao ndio wana maduka yanauza bidhaa kwa TBC.

1. TBC ni chombo cha umma ambacho kinapaswa kuwa na weledi wa hali ya juu. TBC inapaswa kujitofautisha na vyombo vya mchongo vilivyozagaa nchini.

2. Kuna matukio mengi ambayo TBC imeyafanya bila kuzingatia weledi. Itoshe kuyataja machache:

2.1 Mwaka 2014 wakati wa Mjadala wa Katiba, TBC ilikuwa ikitoa upendeleo na kukera wengi akiwemo Mwandishi nguli Maggid Mjengwa wa Iringa ambaye alilazimika kulalamika.

Aidha, TBC ghafla ilikatisha matangazo Aprili 14, 2014 wakati Mhe Tundu Lissu akitoa maoni kwa niaba ya Kamati yake! Dr. Slaa, aliyekuwa KM CHADEMA, akazomoka:

"TBC ni adui wa mageuzi. Serikali imesahau kuwa ilisaini Maadili ya Vyombo vya Umma vitumike kwa manufaa ya umma bila upendeleo".

2.2 Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2020, TBC ilikinaisha kwa kuonesha kampeni za CCM tu 24/7 hadi kupachikwa jina la utani TBCCM ilihali TBC ni chombo cha umma na kuna uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa vyombo vyote vya habari vya umma vinapaswa kutoa haki sawa kwa vyama vyote.

2.3 Machi 10, 2017, TBC, kwa uchawa wake, ilitulisha "Bongolanderz" matango pori kwa kudai eti Rais Donald Trump wa Marekani amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi nzuri ! Enzi zile, ungedhani kuna mashindano ya Mawizara na Taasisi za umma kumsifia Rais Magufuli! Uchawa huu ukapelekea waandishi 9 wa TBC wasimamishwe! Waliosimamishwa ni Gabriel Zakharia, E. Mramba, P. Constantino, D. Mmari, R. Mpenda, L. Mushi, A. Wawa, C. Ruza na J. Losai.

2.4 Desemba 23, 2015, TBC iliwakera "Bongolanderz" nchi nzima pale ilipokatiza ghafla Taarifa ya Habari Saa 2 usiku na kuonesha harusi ya Kibopa mmoja kwa Saa 3! Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari (Maelezo), Assa Mwambene akatiririka:

"TBC ilichofanya si sahihi. TBC ni chombo cha umma hakikupaswa kuonesha mambo ya mtu binafsi kwa zaidi ya saa tatu. Saa tatu umma unaangalia mtu anavyomsifia mke wake? Kisa amelipa milioni 17? Hii si sawa".

2.5 Baadhi ya Watangazaji wa TBC uelewa wao ni mdogo sana kiasi kwamba kwenye mahojiano mubashara kuhusu mambo muhimu ya Kitaifa wanauliza maswali ya kijinga/kitoto sana na kukera mno (wapo baadhi wanauliza maswali ya maana mf Gabriel & Elizabeth). Aidha, wengine wanashindwa kutofautisha baadhi ya herufi mf "R" na "L".

2.6 Septemba 4, 2019. Kamati ya Maudhui ya TCRA ilitoa onyo kali kwa TBC kwa kukiuka Sheria, Kanuni na Misingi ya Uandishi wa Habari kwa kuonesha picha zisizofaa.

2.7 TBC ilifuta matangazo mubashara ya Bunge kwa sababu za kimchongo 2016. Ilielezwa kuwa TBC haitakuwa ikionesha bunge mubashara kwavile eti "Bongolanderz" wengi huwa makazini hivyo wanaacha kazi na kuangalia bunge! Tuliosomea Cuba tulibaini ni fiksi. Mhe Spika Ndugai baada ya "kustaafu" akamwaga mambo hadharani:

"Leo niseme ukweli; sababu ya kuachana na kuonesha bunge "live" ni kwavile tulibaini Wabunge wa upinzani walikuwa wanapata coverage kubwa inayowapa kichwa. Tulibaini wengi hawaendi majimboni kwao, wanatumia bunge tu na wengine wanaishambulia sana Serikali ili wajulikane kwavile wanajua kuna Bunge "live"!.

2.8 Tukio la majuzi la MV Mwanza ndio fungakazi. Mwandishi, bila kupepesa macho wala kutikisa mustachi, ameeleza eti meli hiyo itafika hadi Malawi & Zambia! Kwani inatumia matairi ? Hivi mnatuchukuliaje lakini? Mbaya zaidi, nimeiona taarifa rasmi iliyotolewa na Mamlaka ambayo haikutaja nchi hizo hivyo mwandishi kaongea urongo mwingine! Cha ajabu, hadi leo TBC haijatuomba radhi!

NB:
Ikumbukwe kuwa Mhe Harrison Mwakyembe alipokuwa Waziri wa Habari, Sanaa & Utamaduni, alieleza bungeni alipowasilisha bajeti ya Wizara yake ya 2017/18 kuwa moja ya changamoto kubwa za TBC ni kutozingatiwa kwa maadili ya uandishi wa habari.

Miaka 7 baadaye, tatizo bado linataradadi!
?
 
4
Samahanini nipo nje ya mada ila hili ni jambo zuri pia

KAMA UNATUMIA TIGO BORA UTOE 40K ILA UOKOE HELA UNAZONUNUA DATA&DK KWA MIAKA 2 (GB48 KILA MWEZ+DK 2000)*

Watumiaji wa tigo njoo nikuunge huduma hii uwe unapewa gb 48 na dk 2000 kila mwezi kwa miaka miwili, huduma hii sahivi unaungwa pekeyako na sio kikundi.

Uhakika na usalama wapesa yako ni 100% mana hela unailipa direct Tigo kama unavyojiunga na vifurushi vingine, mm nakupa maelekezo tu ya kujiunga, ( ukijiunga nalipwa na tigo ).

kama ukitaka kujiridhisha nikishakupa maelekezo unaweza kupiga 100 uulizie ujiridhishe kabla ya kulipia.

PIA KUNA GB35+1000DK KILA MWEZ KWA 30K, MUWE WATU WAWILI.

HUNITUMII HELA YOYOTE HATA MIA!

Karibu hata uniulizie tu nikupe maelekezo bure!

KAMA UKITAKA TUKUTANE TUFANYE KAZI LIVE PIA INAWEZAKANA

NITEXT WHATSAPP

0717700921
40k unalipa kila mwezi?
 
Back
Top Bottom