TB JOSHUA: Kuna Rais East Africa atatekwa na Club kulipuliwa

Yaani huyu Pastor yeye anatabiri matendo ya kishetani tu. Kwa nini hajatabiri mambo ya neema kwa "wana" wa Mungu

Alileta story ya Boko Haram kufutika ikagonga mwamba. Huwa anacheza na probability za matukio katika jamii kulingana na mazingira halafu anakuja na majibu.

Halafu matukio yakitokea ndiyo huwa anajitokeza na kudai alitabiri na limetokea.
.......................
......................

He's getting richer wakati waumini na wafuasi wake wengi getting poorer.

Really? :A S 39:
 
Nadhani kasema ilishatokea huko nyuma, kwamba watu walikuwa wanacheza na kunywa na bomu likalipuka. Kampala at 2 places come to mind during the 2010 World Cup RSA.

Sasa, kuhusu kumteka Kaguta.........sijui!!!!
 
Boko haram kila siku piga hapo Nigeria mbona hajatabiri? wajinga ndiyo waliwao.
 
Imeandikwa kuwa mtawatambua kwa matendo yao,kutabiri na mambo yakatokea haimaanishi kuwa ni mtumishi wa Mungu. Anaweza kutabiri mambo kwa nguvu za mwovu na yakatokea na hapo ndipo wanadamu huchanganyikiwa. Siku za mwisho watatokea manabii wa uongo watafanya ishara nyingi na yumkini hata walio wateule watadanganyika. Tuweni macho wachungaji wengi wa siku hizi wanafanya Kazi ya Yule mwovu na kujitajirisha wenyewe. Wanaongelea zaidi mahitaji ya kimwili na kusahau kabisa maisha ya kiroho.
 
kama mimi namwamini sana huyu mtumishi wa Mungu,kwani Mungu wetu anamtumia sana,ndugu zangu watanzania mwaminini huyu Tb joshua kwani ni mtumishi wa kweli na Mungu anamtumia sana.
...siku ukija kustuka it will be too late....wewe fanya mambo yako kwa bidii, muombe mungu wako wa kawaida...basi haya mambo mengine yatakuangaisha kwenye maisha
 
Hajatabiri mafisadi wote Tanzania watubu na kurejesha rasilimali walizokwapua???!!!! Atabiri na mambo mazuri si haya ya kumaga damu tu au kuwa na matukio mabaya katika maisha. Kwa nini asitabiri neema??? Bahati mbaya siku hizi makanisa na wanaojiita manabii wanatumia nguvu za giza na uchawi mwingi unatoka Nigeria!!!! Wachungaji, manabii sijui na mitume kila siku Nigeria wanaenda kupata ndumba za kuongeza waumini. Halafu kanisa moja eti kiongozi anakuwa na kikundi cha maombi eti kazi yao ni kuombea watu wapate mapepo na magonjwa ili eti waende kanisani kuombewa na pale watakuwa waumini na kulipa sadaka!!! Ni ya kweli haya msikatae!! Aibu sana.
 
Vyombo vya ulinzi na usalama tusije kumbuka shuka kunakucha na mzalau mwiba....... take care on our beloved leaders may the living GOD guide you Amen
 
napitaaaaaaaaa

waya kwiiiiiii????
ALITABIRI KIFO CHA MICHAEL JACKSON pia na ikatokea. "A super star (in America) will go on his way of no return before end of this month......) ndivyo alivyosema, na mwezi huo huo Ikatokea.

ndiyo, NI MASUALA YA KIIMANI lakini huyu bwana ni tofauti kidogo, si vizuri KUPUUZA.
 
Kinachonisumbua na watabiri kama TB Joshua jinsi wanavyotabiri habari za mambo mabaya. Huyo Mungu huwa hawaonyeshi na mazuri pia? Hebu mtu mmoja aniambie kitu: Ni utabiri gani aliyowahi kutoa ukatimia kama si yale tu yanayofanywa katika masinagogi yake.

Mimi nafikiri yakitokea aisadie polisi kuwapata wahalifu; au amwombe Mungu amwonyeshe wahalifu ili uovu uzuiwe.
 
Yaani huyu Pastor yeye anatabiri matendo ya kishetani tu. Kwa nini hajatabiri mambo ya neema kwa "wana" wa Mungu

Alileta story ya Boko Haram kufutika ikagonga mwamba. Huwa anacheza na probability za matukio katika jamii kulingana na mazingira halafu anakuja na majibu.

Halafu matukio yakitokea ndiyo huwa anajitokeza na kudai alitabiri na limetokea.

Kila mtu na shamba lake la mavuno ya kimaisha na wajinga ndiyo waliwao.

He's getting richer wakati waumini na wafuasi wake wengi getting poorer.

Mbona hilola Bokoharamu ndio umekomalia U mmoja wa wana kundi hilo nini! Mengi ametabiri na yametukia.
 
Mbona hilola Bokoharamu ndio umekomalia U mmoja wa wana kundi hilo nini! Mengi ametabiri na yametukia.
Mtabiri anayeongea na "Mungu" kama anavyodai hawezi kuambiwa jambo na mungu wake na lisitokee labda huyo mungu ni kutengeneza na siyo yule "Mungu" aliyeumba mbingu na dunia anayefahamu kila kitu kwa sababu ni yeye aliyeviweka.

"Mungu" aliyeumba mbingu na dunia hana room for manoeuvre kwa sababu neno lake ni kweli.

Endeleeni kumtajirisha huyo mtabiri wenu kwa sababu imani haina maswali na fikra kinzani kama tunavyohoji na kufikiria kutokana na matendo yake yanayotoa wingu la mashaka katika utendaji wake.
 
Mtabiri anayeongea na "Mungu" kama anavyodai hawezi kuambiwa jambo na mungu wake na lisitokee labda huyo mungu ni kutengeneza na siyo yule "Mungu" aliyeumba mbingu na dunia anayefahamu kila kitu kwa sababu ni yeye aliyeviweka.

"Mungu" aliyeumba mbingu na dunia hana room for manoeuvre kwa sababu neno lake ni kweli.

Endeleeni kumtajirisha huyo mtabiri wenu kwa sababu imani haina maswali na fikra kinzani kama tunavyohoji na kufikiria kutokana na matendo yake yanayotoa wingu la mashaka katika utendaji wake.

Katika GT ninaowakubali hapa jukwaani wewe mmoja wao ng'wanamapalala
 
Last edited by a moderator:
Really? :A S 39:
Mkuu, kwa nini unashangaa.

Hakuna utabiri ulifanyika kwenye vitabu vya dini na haukutokea kwa sababu hao watabiri walikuwa wanaongea na Mungu wa kweli ambaye neno lake ni kweli kabisa.

Huyu ni mtabiri gani anayeongea na "Mungu" ambaye anachokisema hakitokea?.

Mungu wake siyo yule wa kwenye Biblia anayoitumia kwa sababu yule wa kwenye biblia huwa hakosei kwa sababu NENO lake ni KWELI.

Hata waganga wengine wa kienyeji wanaweza wakafanya zaidi ya anachokifanya. Angesema tu yeye ni mganga wa kienyeji anayetumia Biblia kufikisha ujumbe labda ningemwelewa kidogo kuliko kujibandika unabii.
 
Huu uzi sijui ulianzia wapi. Nimekutana nao ghafula. Namshukuru Mungu nimepata nafasi ya kuupitia wote. Jambo moja nimegudua; hakiri za binadamu hazitakaa ziujue ukubwa na mipango ya Mungu; labda kwa neema.

Wachache niliokutana nao ktk jukwaa la siasa, leo ndo nimejua jinsi walivyo. Sikujua kama mtu anaweza kuwa na ushahidi wa kikatiba ktk maelezo yake na asiweze kuwa na ushahidi wakutosha wa kumtuhumu mtumishi wa Mungu. Kwa bahati mbaya watu kama hawa wakiingia ktk siasa mlinzi wao mkuu ni waganga wakienyezi.

Kibaya zaidi ni pale nilipoona kituko cha mwaka, maoni ya mmoja ktk huu uzi yanatisha....ni kama majigambo...majigambo ya kipepo, na ni ya woga. Nachelea kusema ktk anga zake anamwona TB Joshua. Tatizo mmoja yuko upande mmoja na mwingine yuko upande mwingine. Wakikutana kuna kitu kitatokea.

Nivizuri ukatembelea chanel ya 'emmanuel tv' ili ujue nini mtumishi huyo anafanya kabla ya kutuhumu usiyoyajua.

Kinachonisikitisha hapa ni kama tunataka Mungu afanye aliyoyatabili TB ndo tujue kwamba yeye ni Nabii. Kinyume chake tuamini yeye ni 'Mwongo'.
Hii ni imani yako kama ilivyo imani kwa watu wengine. Watu hawakatazwi kuhoji pale mtu anapotoka kwenye imani na kuweka hoja ya kutaka watu wamwamini kama ni mjumbe wa Mungu wa kwenye Biblia kwa matendo na matukio anayoyafanya.

Hebu nieleze ni wapi katika Watabiri wa kwenye Biblia anayoitumia huyu Tb Joshua walitabiri jambo ambalo baadaye halikutokea?. Mungu wa kwenye Biblia anafahamu kitu kitachotokea kabla hata ya kutokea and NO room for manoeuvre kwenye neno la Mungu wa kwenye Biblia.

Kama Mungu aliongea na Tb Joshua na kumwambia kama kuna jambo bays litatokea na Tb Joshua akawaeleza wana wa Mungu jambo hilo lakini baadaye Mungu akazuia lisitokee, kwa nini huyu "Mungu" hakurudi kumwambia tena awaambie wana wake kama hilo jambo halitatokea tena badala yake akakaa kimya tu kitu ambacho kinatafsirika ni uwongo.
 
Back
Top Bottom