TB JOSHUA: Kuna Rais East Africa atatekwa na Club kulipuliwa

hivi kuprophesize maana yake nini? Jana mwenyewe (t.b.joshua) alizungumzia kuhusu seers akiwalenga waganga na fortune tellers sasa sijui seers maana yake nini?
Ofcourse nabii sindio prophet anaoneshwa future events na anazisema, sasa kutabiri, kubashiri sijui maana yake sana, na si tuna watabiri wa hali ya hewa?
Mmesaha yule samaki aliyekuwa akitabiria mechi za kombe la dunia? Ila kwa bahati kiumbe huyo hakipo hai tena.
 
Haiwezekani taarifa hizi apewe na Allah maana wanaondaa hayo mashambulizi ni watu wake

Kwenye elimu ya ramli katika dunia ya roho kila kiumbe huongea na rafiki yake kibaya huongea na mbaya na kizuri huongea na mzuri.Kwa sheria hiyo TBJOSHUA angekuwa mtu mzuri mwenyezi Mungu angemweleza anavyolinda watu wake dhidi ya hao washambulizi lakini kwa kuwa ni mbaya anapata taarifa na nia za ule upande wa washambuliao yaani mashetani.Mashetani yanamwambia kile yanataka kufanya mara nyingi.Yeye ni MEDIUM CHANNEL za mashetani.Anaposema watu wajiandae hawaambii waumini kanisani kupitia TV anawaambia wachawi na wale wapendao kunywa damu na kula maiti wajiandae kupata mlo eneo hilo analotamka.Taarifa zake za muhimu kwa wanga na wachawi hasa wa nigeria.

Ndio maana nikasema Mwambieni TB JOSHUA akome asicheze na tanzania na mmwambie wenyewe hawataki.Mwambieni akome asisogee Tanzania tunajua kuliko anavyojua abaki na mashetani zake akitaka nyama akaue boko haram asithubutu Tanzania.
 
Kwani ameacha kuhubiri neno la Bwana amekuwa Mtabiri. Hivi mbona watu wanaanza kukengeuka kiimani, badala ya kuamini neno la Mungu ambalo linahubiri amani, furaha na upendo wnageukia kuhubiriwa hofu? Wagalatia 5:22 anasema "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu" Na imeandikwa tena jatika
Jeremiha 17:5-9 Bwana asema hivi, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake maana moyoni mwake amemwacha Bwana.6. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. 7. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. 9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Acheni kumtegemea sijui Nabii mtegemeeni Mungu wenu. Ishini kwa imani na si kwa utabiri
 
elimu ya unajimu makao makuu yake ni kule SCOAN inapopatikana.
mi sioni tofauti ya huyu na yule marehemu mnajibu wa magomeni. yesu akishuka leo! huyu jamaa sijui atajificha wapi
 
Si mimi ni utabiri wa TB Joshua leo, ameonyeshwa rais mmoja Africa atatekwa na ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza then wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya, Angalizo, amesema siyo kenya tena,je itakuwa nchi gani?

Misa ya leo jumapili ndo kasema, na amesema ataendelea kuomba ili jumatano na alhamisi ijayo aonyeshwe ni rais gani na nchi gani.

VIDEO:



Jamani tuombe sana isiwe tanzania


Kwa hiyo tujiandae na msiba wa kitaifa?
 
Last edited by a moderator:
Tusipuuze ya Nabii Joshua. Kunaweza kuwa na ukweli na hivyo kila mtu ataje jina la Mungu kwa imani yake.

Ref. Marehemu shehe Yahaya alikuwa mtabiri wa kweli
 
Poor interpretation of the bible, no wonder you read it as mwananchi.
Tunahitaji comment Kama yako kufaham watu Kama ww mpo.
Angalizo unaposoma neno la Mungu specifically bible Muombe Roho Mtakatifu upate kuelewa zaid usiishie kusoma single line na kufanya hitimisho, soma neno kisha jipe muda wa kutafakari.

Hongera wewe unayeielewa bible.
 
Wanga mna matatizo sana, mwenye Tanzania ni Mungu mwenyewe na wala si mchawi yeyote au kikundi cha waganga. I know you know how dangerous TBJ is to your evil missions.
Kama kweli wewe una huruma na watanzania, washauri wakatolewe mapepo na sio kuwaada eti anatumia mapepo.

Kama hujui chochote kaa kimya fanya tafiti Ogopa kuwa sema watumishi wa Mungu laana nje nje
 
Huyo ukimuita Mshirikina na Mzinzi na yule aliyekuwa anapiga mtoto wa miaka 9 na kupewa utume na Mganga wa kienyeji kwenye pango (Al qaba) utamuitaje?

povu la nini wewe, tatizo unafikra finyu sana si vizuri kukashifu dini za wenzako mi ni mkristo kama wew tena catholic but huyu jamaa ni mzinz na mshirikina utabiri gani wa mambo mabaya tu je bible inatufundisha ivyo? fikiri kabla ya kunena ndugu.
 
Yaani huyu Pastor yeye anatabiri matendo ya kishetani tu. Kwa nini hajatabiri mambo ya neema kwa "wana" wa Mungu

Alileta story ya Boko Haram kufutika ikagonga mwamba. Huwa anacheza na probability za matukio katika jamii kulingana na mazingira halafu anakuja na majibu.

Halafu matukio yakitokea ndiyo huwa anajitokeza na kudai alitabiri na limetokea.

Kila mtu na shamba lake la mavuno ya kimaisha na wajinga ndiyo waliwao.

He's getting richer wakati waumini na wafuasi wake wengi getting poorer.

Umenena mkuu, people shud stop dis stupidity of believing in superstitions....even da wholy books dat dey use explains clearly dat no mor prophet after Muhamad(s.a.w)...By da way wajnga ndo waliwao;)
 
Kama hujui chochote kaa kimya fanya tafiti Ogopa kuwa sema watumishi wa Mungu laana nje nje

Soma bandiko langu vizuri ulielewe ndipo uanze kutoa shutuma. Hii tabia ya kuingia jf na kuanza kutoa comments bila kusoma na kuelewa mada au comment ya mtu haifurahishi hata kidogo
 
Huyo pastor ndiyo mzushi.

Huyu Pastor anatumia matatizo ya wananchi ambayo ni mali na roho kujitajirisha huku waumini wake wakiendelea kuwa masikini kila siku.

Mavuno ni mengi palipo na umasikini wa mali na roho lakini wavunaji na huyu pastor ni wachache sana.

Zaburi 1

1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
 
Back
Top Bottom