Tatizo ni siasa au upinzani?!

arnolds

Senior Member
Oct 10, 2009
105
57
Wadau hii ishu ya profesa Baregu kunyimwa mkataba mi sijailewa hasa ina misingi ipi! Baregu hakupewa mkataba mpya wa ajira kama ilivyokuwa kwa wahadhiri wengine waliostaafu kama yeye.

Kwa maelezo ya waziri ghasia, “Baregu hakupewa mkataba mpya wa ajira baada ya ule wa awali kumalizika kwa misingi ya Kanuni za Utumishi wa Umma na maelekezo kuhusu ushiriki wa watumishi wa umma katika siasa,".
Profesa Baregu alistaafu kazi kwa mujibu wa sheria Februari 24 mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 55. baada ya kustaafu, aliajiriwa kwa mkataba na UDSM mara tatu na mkataba wa mwisho ulimalizika Januari mwaka 2008,

tujiulize je wakati anapewa mikataba baada ya kustaafu swala la yeye kujihusisha na siasa lilikua halionekani?? Au tukizungumzia siasa tunamaanisha kujihusisha na upinzani?
Tunajua kuwa, serikali imekuwa ikitoa ajira kwa mikataba kwa wastaafu ili wasaidie kutoa huduma wakati ikifanya jitihada za kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Swali la kujiuliza ni je, huduma za profesa Baregu kama mhadhiri hazihitajiki tena?.
Hivi serikali haioni kuwa tunahitaji mchango wa wataaluma kama hawa ili kuikomaza siasa nchini?
 
Back
Top Bottom