Tatizo la wanawake kutoshika ujauzito

Pole Mpendwa dada, wakati mwingine hutegemea na mzunguko wengine wanamzunguko mfupi, na wengine mrefu hivyo inaweza ikakuta wewe unamzunguko mfupi ambao siku zako za hedhi ndizo siku za kupata mimba jaribu kuwasiliana na madaktari kwa hilo, ingawa inakuwa hujisikii sana kukutana na mwenzi wako kipindi hicho.

Ongea na daktari mueleze kuhusu mzunguko wako wa hedhi, akusaidie kwani kuna shemeji yangu naye alikuwa na hilo tatizo, yaani mke wa mdogo wangu, Mungu aliwajaalia walipata mtoto kwa njia hiyo, yani ya kukutana kipindi cha hedhi. Angalia siku ya kwanza ya hedhi esabu siku moja na siku ya mwisho kabla ya siku unayopata hedhi ndipo mzunguko wako ulivyo kama sikosei ingawa si mtaalamu sana.

Kingine unaweza kuesabu siku kumi toka umeanza hedhi kama siku ya kwanza hizo pia huwezi pata mimba mpaka siku ya kuminamoja mpaka ishirini hapo mkikutana namwenzi wako pasipo kupumzika lazima mimba ikamate kama unamzunguko mrefu au hujafuatilia.

Toka hedhi kama siku ya kwanza mpaka ya kumi (free huwezi pata ujauzito ni bahati sana) ila siku ya kumi na moja toka hedhi mpaka ishirini bila kupumzika hapo lazima. Pia jitahidini kula vizuri, msitumie vilevi vikali, hakikisha mmeo anapata mlo mzuri na muda wa kupumzika.

ASANTE
 
Pole sana Mpwa.

Mimi nakushauri sana, tulia na ondoa fikra zako kuwa umerogwa wala sijui nini tena huko, tulia na jishughulishe na mambo mengine, mie ndugu yangu wa kuzaliwa nae kabisa, mkewe alikaa miaka mitatu na hatimae wiki tatu zilizopita amepata mtoto wa kiume, mwingine ni mtu ambaye nilisoma nae Mlimani, hajawahi kupata mtoto na akajiunga chuo akitokea kazini tuaksoma kozi yetu ilikua miaka minne hadi mwaka wa nne tuanakaribia kuondoka ndio kitumbo kikatuna; kuna mtu alishawahi kuniambia eti hata ukiwa na fikra tu kuwa mimi sishiki/sibebi mimba basi yawezakuwa, akani-refer kwenye kitabu na maandiko yanayohusu the power of positive thinking.

Hebu na wewe wakati wa ile shughuli amini kuwa inawezekana then itawezakana,cheza mechi kwa ufundi kabisa huku mkiwa wote mme-clera your mind from doubt. umeskia Mpwa na MUNGU wangu ninayemwamini na Kumtumikia akakubariki na kukufariji ukanyonyeshe mtoto kwa maziwa yako mwenyewe, kumbuka Sarah alipata mtoto akiwa ameshapita kwene menopouse (sp). Why not you miaka miwili tu?

Kuna ushindi na amani unapomtegemea MUNGU kuliko kusema eti umerogwa. Amen
 
Pole mamy, mtangulize mungu kabla ya kuwaza madaktari bingwa na waganga wa jadi, tatizo lako ni dogo unapresha sana ya kubeba mimba ndio maana toa akili kwenye mimba jaribu kuachilia ili akili ikae sawa waza mambo mengine punguza kupania mimba, halafu siku ambayo uko kwenye heat ndio ufanye hilo tendo, sio kila siku mimba inashika mama. Tuliza kichwa relax mtoto atakuja mwenyewe bila wewe kujua.
 
Amen bwana Elli. Mungu akujaalie. Nilichanganykiwa ila kwa sasa nipo safi. Nashukuru kwa ushauri wenu wadau, hata huyo aliyeniambia nijiandae kuachika mungu ambariki ampe uzao kama wa mfalme suleiman.
 
Last edited by a moderator:
Idd,

Aghrr, hivi wewe unafikiri uko perfect sana? Unahisi huyu dada amejitakia? I doubt ya age .hivi JF hatuna age limit eee? Huna hata mtoto wewe, unajiona kidume kisa kinanihii chako kinasimama!! Hata kama unao watoto wangapi, hujaona au kusikia mtu anazaa watoto na Mola anawapenda zaidi na kubaki mkiwa? Unajiamini vipi wewe kuwa hayawezi kukukuta haya? Hii mitoto ya JK bwana!!!!!!

Pole sana dada, simama imara na iko siku utaitwa mama!
 
Hello Check with Rhesus Factor + or Rhesus Factor -

Au check Antigen and antibodies balancies.

May be your husbands sperm become antigen hence they become killed by your antibodies.

There are certain injections you can get and pregnancy is absolute.

Consult Specialist Doctor for Women
 
Asante sana kwa maelekezo ya dawa.Vipi hizi dawa zinapatikana wapi?yaani ni wapi naweza kwenda nunua?
Kaulize hizo Dawa kwenye Maduka ya wauza dawa za kiarabu wauza Dawa wa Kipemba hapo Dares-Salaam mimi zamani nakumbuka ilikuwa ni Kariakoo Mtaa wa pemba sijuwi siku hizi hayo maduka ya wauza Dawa za Kiarabu wauza viungo vya pilau wako wapi? Maana mimi sipo

Bongo nipo nje tena ni siku nyingi sana ulizia kwa Wapemba au waarabu watakufahamisha kama una jirani muarabu au mpemba wewe muulize atakufahamisha wapi zinapatiakjana hizo dawa ukishindwa nijuulishe nitakup adada yangu atakusaidia dawa ya kuweza kupata ujauzito.
 
Mr's goole

Pole sana kuna dada mmoja pia alikuwa na tatizo kama lako kunadaktari mmoja anamfanyia special treatment with different methods hivi tunavyoongea wiki 2 zilizopita imenasa so ni PM nitakuunganisha.
 
Last edited by a moderator:
With Jesus, everything is possible.Believe in Jesus and wait upon HIM.Ni mewaona wengi wenye tatizo kama lako sasa wananyonyesha.As long as dr amethibitisha kuwa hakuna mwenye tatizo kati yenu, basi inahitajika nguvu isiyo onekana!.By the way kuna semina ya mtumishi wa Mungu mwl Mwakasege inaanza jumapili hii pale kinondoni biafra kuanzia saa 9 usikose.

Great advice! the problem is this; most of them want to solve spiritual problems intellectually!
 
GREAT ADVICE:

Mithali 3:5-6. "mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,wala usizitegemee akili zako mwenyewe;katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako.

usiziamini na kuzitegemea sana akili za binaabamu! usijaribu kutatua matatizo ya kiroho kwa akili za kibinaadamu na wala usifanye ushirikina utajiongezea matatizo.

Yesu Krsto alikuja kuwafungua waliofungwa.Muamini na mpokee awe BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.
GOD BLESS YOU
 
Straight corner

Vijitu vingine vinajifanya rijali kumbe hata wa kusingiziwa hana! Hiyo ndiyo raha ya JF watu wana uhuru wa kumwaga hata pumba!
 
Last edited by a moderator:
Pole mpendwa, mie nina rafiki yangu ameolewa kakaa kwenye ndoa miaka saba bila mtoto lakini mwezi wa saba mwaka huu kanipigia na kunambia ana ujauzito haamini kila baada ya week anapima. Mungu ni mwema endelea kumuomba atakupa mtoto.

Mwingine alikaa kwenye ndoa miaka sita bila mtoto family ya mume ilianza kumjia juu na hatimaye mmewe akabadilika na kumpa talaka baada ya kukaa kwao mwaka akapata mwanamme mwingine na kuolewa mungu alivyo mkubwa sasa kishajipatia mtoto wa kiume. Kwa hiyo usikate tamaa hata kidogo.
 
Pole sana mpendwa Mungu ni mwema atakupigania2 na ipo ck utapata mtoto! Coz hata mimi nina shem wng leo ni mwaka wa tano huu tangu waoane na bro hadi sasa hawana mtt na wapo fresh2 wanaendelea na life kama kawaida na kuzidi kumwomba Mungu2! So ondoa hofu endelea kufuatilia hizo dawa wanazokuambia wana member na kumwomba Mungu awasaidie!
 
Back
Top Bottom