SIRE
Member
- Feb 20, 2022
- 83
- 119
Wakuu naanza kwa salamu zangu za dhati kwenu pia poleni na mihangaiko ya siku nzima ya leo.
Kabla sijaenda kwenye maada. Naanza kwa kusema kuwa najiona kuwa na bahati sana kuwa katika jamii ya siri kama hii ambapo kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake bila kuhofia kutambulika katika jamii husika kitu ambacho kimafanya watu wawe huru sana kutoa mawazo na maoni yao ya siri juu ya maada mbalimbali.
Paso na kupoteza wakati wenu naomba nianze na kuelezea hili swala ambalo naliona kama kero kwangu.
Nimekuwa nikisumbuliwa na Typhoid na UTI ambazo zinarudi tena muda mfupi ( makadirio ya mwezi mmoja au miwili) baada ya kutumia dawa za hospitalini. Hii shida sikuwahi kuwa nayo nilipokuwa mtoto lakini ni haki ambayo imejitokeza nikiwa mkubwa. Nakumbuka nilipokuwa mtoto nilikuwa nakunywa hata maji ya bombani bila shida yeyote, lakini hali ilibadilika nilipojiunga na advance. Hali hii imekuwa endelevu mpaka imekuwa kero kwangu.
Nimetumia dawa karibia zote zinazohusiana na Typhoid na UTI. Baada ya kutumia kidogo napona lakini baadae naanza kupata dalili tena.
Nafikia kipindi naogopa pengine matumizi yaliyozidi ya dawa za hospitalini yataleta athari kwenye ini au figo.
Naomba kwa aneyejua dawa za asili Ili nipate kuwa natumia pengine zikanitatulia hili tatizo langu.
Natanguliza Shukrani zangu kwenu kwa usaidizi mtakaonipatia.