Tathmini yangu fupi kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri

Kama tunavyojua kuanzia leo ndio ukomo la Mawaziri. Kutokana na kuapishwa rasmi kwa Raia John Magufuli... Kinachofata sasa ni Rais kuitisha bunge na kupeleka jina la Waziri Mkuu ambaye pasipo shaka naona Majaliwa Kassim atarudi.... Pamoja na kurudi Majaliwa, hawa watu watamsaidia sana Rais katika utendaji wake...

1. Ummy Mwalimu - abaki pale pale Afya
2. Sagini (Butiama) - aende TAMISEMI
3. Prof. Ndalichako - abaki pale pale...
Napendekeza Dr. Lyabwene Mtahabwa apewe wizara ya elimu.
 
Lakini mawaziri na manaibu wote wanasubiri Magufuli afikiri na kuwaagiza wafanye nini. Hata akiteuliwa Kibajaji kuwa waziri wa Elimu ni sawa kabisa, wako pale tu symboliccaly. Maamuzi yote yanafanywa na Mtukufu Magufuli.
 
Matamanio yangu mimi nikama ifuatavyo:

Philip Mpango - Waziri wa Fedha & Mipango

Charles Kimei - Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Kimei asaidiane na Philip Mpango)

Note: Combination ya Philip Mpango na Charles Kimei itanoga kwa sababu Philip Mpango nikama anauzoefu wakutosha wa upande wa Planning na Charles Kimei anauzoefu wakutosha wa upande wa Finance 'Banking Industry'

Au

Charles Kimei - awe Waziri wa Wizara mpya itwayo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Masoko

Ili mchumi huyu akatusaidie kutuletea wawekezaji nchini na kututafutia masoko ya bidhaa zetu
 
Wizara nyingine nyeti (kwa kupaisha uchumi, utengenezaji wa ajira, kuongeza mapato ya serikali, na kuleta fedha za kigeni nchini) ambazo pia zinatakiwa kupata watu makini ni:
  • Kilimo, Ushirika & Umwagiliaji (wizara hii inazalisha ajira, inapunguza umasikini wa kipato, inatoa malighafi za tanzania ya viwanda, na exports)
  • Mifugo & Uvuvi (wizara hii inazalisha ajira, inapunguza umasikini wa kipato, na kutoa bidhaa za kusafirisha nje ya nchi na mwishowe taifa kupata fedha za kigeni)
  • Uchukuzi & Usafirishaji (wizara hii inazalisha ajira, ina ongeza mapato ya serikali na kuiletea nchi fedha za kigeni)
  • Madini (wizara hii inazalisha ajira, inaongeza mapato ya serikali, na kuleta fedha za kigeni)
  • Utalii (wizara hii inazalisha ajira, inaongeza mapato ya serikali na kuleta fedha za kigeni)
  • Michezo, Sanaa & Ubunifu (vijana wengi wako hapa; wamejiajiri kupitia sports & games, muziki, filamu, tamthilia, ubunifu wa mavazi, urembo, na issue chungu nzima)
 
Mnashabikia upupu,mnaua demokrasia afu mnapanga vyeo ilimuendelee kututiaumasikini.Kwa yeyotealiyechangia kuua vyama vingi,kupora haki za wapinzani,MUNGU AMUUNGUZE KWA MOTO MKALI,ABAKI MAJIVUMATUPU.Nyambafu
 
Mwanzo kabla ya kuteua hao mawaziri huwa inaandaliwa instrument ambayo inaelezea themes na taasisi zitakazohusika. Kwa hilo ninamuomba Mh. Rais aunganishe baadhi ya taasisi maana bado zina duplications ya majukumu mno. Kwa mfano taasisi zifuatazo:

1. SIDO na TIRDO kuwe na taasisi moja kubwa yenye kubeba majukumu yote combined na kuwe na idara kubwa zikiwemo Research na Industrial Development

2. Tanzania National Business Council unga na Tanzania Investment Centre na National Economic Empowerment Council. Hizi zinafanya very duplicate roles na nyingine zinamezana mfano investment vs empowerment n.k

3. Ongezeeni nyingine
 
Ni hivi!
Mfalme alimtafutia sababu gambo akamvua ukuu wa mkoa ili agombee ubunge!

Nilishasemaga Hilo watu wakanipinga kabla hata ya uchaguzi!
Ni hivi huyu mfalme kapanga Kila kitu,hakuna haja ya kushindana nae keshaapishwa tusubirie siku zijazo chache akisema kitu Tena kwa uchungu
 
Kiboko ya Zitto Kabwe Kigoma Mjini

Huyu Jamaa ni Afisa Kipenyo wa miaka mingi sana,

Akiwa Katibu wa Ccm Mkoa wa Dsm aliwahi kupambana na Mzer Mengi miaka hiyo

Pia aliwahi kutumwa kumkosesha Uenyekiti wa Mkoa Mzee Mangula
mkuu samahani hivi afisa kipenyo ndo usalama wa taifa kwa jina lingine wanaitwa afisa kipenyo
 
Hapo namwona mbobezi katika sheria na masuala ya usafirishaji Dr. OSCAR KIKOYO akiingia kwenye wizara.
 
Back
Top Bottom