Taswira ya TWAWEZA na UWEZO Kenya, Uganda na Tanzania inaenda kuingia doa na dosari kubwa

Baba Wawili 2012

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
413
335
Aidani Eyakuze ni Mkurugenzi mkuu wa Tweweza east africa, namfahamu sana kijana huyu aliechukua nafasi ya Rakesh pale Twaweza. Eyakuze ni rafiki mno tena wa karibu sana na January Makamba, na katika ile proposal concept ya Makamba pale Mlimana city ya kutanganza nia pale mlimani Eyakuze ndie aliekuwa consultant mkuu wa ile proposal ambayo leo kwa kiasi kikubwa imekuwa adapted na Mgombea wa CCM Magufuli na makamba kuwa karibu kuhakikisha inatekelezeka mfano kuipa kila kijiji sh milioni 50.

BADO naconect urafiki wa Eyakuze na Makamba katika takwimu alizozitoa Juzi ktk media january na leo za twaweza....ni km watu wanalala na kuamka pamoja.

Kwa thread hii, Aidani Eyakuze ameidhalilisha taasisi kubwa kama Twaweza kwa kununuliwa na ccm kupitia January na kupika tafiti zenye kuifurahisha ccm...hii ni hatari sana kwa taaluma ya Aidan Eyakuze ambaye Taasis yake inaeshimika kwa tafiiti zenye kulenga kuboresha mambo mbali mbali kwa serikali kwa watu wake. mfano mmoja ni Elimu kwa kupitia mradi wake wa UWEZO Tanzania inafanya tafiti na kuipa mrejesho serikali kwa chanamoto mbali mbali za ukweli toka kote nchini na serikali kupitia wizara ya elimu na TAMISEMI mara nyingi imeonyesha mabadiliko na kufanya utekelezaji kwa baadhi ya maeneo hayo Muhmu. sasa My take ....kama ccm inakununua Aidan..hivi chama hiki kikiwa madarakani kiendelee kuamnini na kufanyia kazi tafiti zako zijazo?? na hasa sasa nasikia mtaongeza evaluation katika afya na mazingira?

Aidani..sio masikin wa hela kwa elimu na nafasi yake pale twaweza...uswahiba wake tena wa siku nyingi na January anaamua kupindisha taaluma yake na taasis yake kutoa matokeo ya kufurahisha ccm hii aitosh kuzuia maamumuzi ya wananchi wanaotaka mabadiliko ambayo UWeZO Tanzania imevumbua madudu mengi tu uko chini katika tafit zake za elimu kwa miaka 5 mfululizo.Aidan wanishangaza sana.
IMAGE ya Twaweza na UWEZO Kenya, Uganda na Tanzania inaenda kuingia doa na dosari kubwa sana kwa upenzi huu binafsi wa Aidan Eyakuze na January Makamba.

Hivi dhambi hii kwa CCM, January na Aidan mtaungamia wapi ili hali nafsi zenu zinajua mnafanya hujuma ya makusudi.....shame on YOU Aidan na Shame on Makamba.

Mungu akupe uhai mrefu Mr Rakesh, ata kama Mkapa alikuwa rafiki yako sana ulimkosoa sana na kumpa fact wakat wa "HAKI ELIMU" hadi ulipooingia TWAWEZA hukusita kufanya hivyo kwa Kikwete na mengi tumeyaoona yanabadilika.....lakini kwa aliechukua Kijiti chako AIdan eyakuze huku sio tena ameendeleza ameamua kufanya Twaweza na UWEZO kuwa taasisi Ndogo za CCM.Shame na kwa washauri wake Uganda, Tanzania, na Kenya..

Nilikuwa napitia report nzima ya Twaweza, kama mtaalam wa utafiti naweza kusema kuna madhaifu makubwa kadhaa.

1. Methodology (technique) iliyotumika

2. Variable ya age hasa kwenye swali la 4 (nani utamchagua) haisapoti results obtained/conclusion. Kwenye inferetial statistics haijawahi kutokea kitu kama hicho, hii ya Twaweza ndio ya kwanza dunia nzima

3. Respondents kupewa simu na power bank ni unethical kwa maana nyingine respondents alikuwa na probability ya 95 c.f ya kuwa influenced

4. Kufikia sample ya watu 1800 kwa "enumeration" ina maana wamehoji kaya 200 tu Tanzania nzima. Na kaya hizo hawajatuambia kama wametumia stratified sampling techniques kwanza kabla ya kufanya random sampling huku wakijua Tanzania ina mikoa/wilaya etc

5. Results za Twaweza kwenye age varible hairespond na taarifa za tume ya uchaguzi... Na kiitafiti hii ndio njia rahisi kujua kama data ni cooked.

Mytake: Tusiyumbe wala kutetereka. Kuna tafiti ambazo nafkiri zitakuja na kutupa reliable & valid data kuliko hii ya Twaweza ambayo imepikwa na January, Aidan na Maria Sarungi
Pro. Kitila Mkumbo.

Utafiti ulifanyika kabla ya vyama vyote kutangaza wagombea!! Kabla ya Ilani kuzinduliwa! Kabla ya kampeni kuanza kufanyika!! Sasa unapomuuliza mtu atamchagua nani wakati hata wagombea wengine hawajui unategemea nini?

Au ulikuwa ni utafiti kati ya Magufuli na Lowassa?

Ni sababu zipi ziliwasukuma TWAWEZA kuharakisha utafiti wao? Kwamba hawakuweza kusubiri vyama vyote viteue wagombea ndio wahoji wananchi? Endapo watasema huo ni utafiti wa awali kwa hiyo huo mwingine utaangalia nini? Matokeo yake watayatoa tarehe moja na ya NEC baada ya tarehe 25.10?

Matokeo haya yanaakisi/reflect uhalisia gani? Najua wengi hatuna akili kama hao watafiti lakini angalau tunaweza kuhoji mambo mepesi kama haya.
Ila utafiti wa TWAWEZA ni wa kipuuzi sana. Haustahili kupewa uzito wowote. Wameharakisha ili kupata mileage kwamba na wao wapo.

Kama walitaka kujua kati ya Lowassa na Magufuli nani zaidi basi wangeandaa kipindi cha Radio wakasubiria simu kama Nani Zaidi ya Radio One sio kuita utafiti!!

Next time mtuheshimu na sisi tutawaheshimu. Hongereni kwa kuingiza siku. Hatujawalipa sisi.

==========================================

Magazeti ya leo yalivoandika
Dar es Salaam. Matokeo ya utafiti wa Twaweza kuhusu Uchaguzi Mkuu yamepingwa na wasomi, wanaharakati na wanasiasa, akiwamo mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ambaye ameuponda na kueleza kuwa matokeo halisi yatapatikana Oktoba 25.

Utafiti huo unaonyesha kuwa kama kura zingepigwa kati ya Agosti na Septemba, mgombea wa CCM, Dk John Magufuli angeibuka na ushindi wa asilimia 65, wakati Lowassa angepata asilimia 25.

Lakini wadau waliohojiwa na Mwananchi jana wamesema utafiti huo haujaakisi hali halisi inavyoonekana kwenye mikutano ya kampeni, ambayo inaonyesha wawili hao wanachuana vikali kutokana na kukusanya mashabiki wengi.

"Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki. Tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata," alisema Lowassa kwenye akaunti yake ya twitter.

Kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Ndanda jana, ikiwa ni muda mfupi baada ya Twaweza kutangaza matokeo ya utafiti huo, Lowassa alisema anashangazwa kwa kuwa wananchi wanaomuunga mkono ni wengi.

"Kuna utafiti wa kura ya maoni umetolewa ukisema eti Magufuli amepata asilimia 65 na mimi 25. Nawashangaa kwa kuwa wanaoniunga mkono wako wengi," alisema Lowassa na kuwaoji wananchi wangapi watampigia kura katika uwanja huo.

Huku wakishangilia wananchi hao walimjibu Lowassa "Tutakupigia" huku wakinyoosha mikono juu.

Baadaye Lowassa alisema: "Tutawajibu kwenye kura tarehe 25 na hamuwezi kukosea kwa kuwa mnaziona mvi hizi. Nangojea mafuriko ya kura kutoka kwenu."

Lowassa alijiondoa CCM baada ya jina lake kuenguliwa na Kamati Kuu na kujiunga na Chadema Julai mwishoni. Chama hicho kilimpa fursa ya kugombea urais, akiungwa mkono na vyama vingine vya NLD, NCCR-Mageuzi na CUF vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Maoni ya wadau

Mbali na Lowassa kutokubaliana na matokeo ya utafiti huo, wadau walioongea na Mwananchi pia walionyesha kuupinga.

Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama alisema matokeo ya utafiti wa Twaweza hayalingani na hali halisi ya kisiasa inavyoendelea nchini.

"Kile kinachoonekana huko nje ni picha mbili tofauti," alisema Profesa Mlama.

Alisema licha ya kwamba Twaweza wamefanya utafiti huo kwa kutumia vigezo vyao, matokeo yasingeonyesha tofauti kubwa kati ya wagombea hao.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Profesa Kitila Mkumbo ambaye alisema: "Matokeo halisi tutapata baada ya wananchi kupiga kura Oktoba 25."

Wakati wadau hao wakizungumzia tofauti ya uhalisia wa hali ilivyo na matokeo ya utafiti, mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Loisulie aliwataka wapinzani kutopuuzia maoni hayo ya wananchi, hasa kutoelewa nafasi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

"Wanaweza wakapuuzia utafiti huo kwa kuwa unampa ushindi Dk Magufuli, lakini sio hili la Ukawa si chama cha siasa kilichosajiriwa kwa sababu itakapofika Oktoba 25 watu wanaweza kwenda kwenye karatasi ya kupigia kura kutafuta Ukawa," alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema licha ya kukosa uhalisia kwa hali ya kisiasa iliyopo, matokeo hayo yanaweza kuwa changamoto kwa Ukawa, kujipanga upya na kuangalia mbinu za kuongeza ushawishi kwa siku zilizobakia.

Hata hivyo, Mbunda alisema matokeo hayo hayawezi kutabiri ushindi wa urais kati ya Dk Magufuli na Lowassa.

"Haileti mantiki kwa mashabiki wa Lowassa halafu utafiti uonyeshe amepata asilimia 25 ya kura. Ningependa ufanyike utafiti mwingine ili kuondoa maswali yaliyopo kwa sasa," alisema.

Wakili wa kujitegemea na makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari alisema matokeo hayo ya Twaweza ni sehemu ya CCM kutapatapa na utafiti a;iouita "feki na wa kutengeneza".

Profesa Safari alisema haiingii akilini, muungano wa Ukawa na Lowassa ukatoa asilimia 25.

"Nusu ya vijana tumeshiriki kampeni za kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura na hata utafiti wetu unaonyesha CCM watashindwa. Kwa hivyo wanatafuta kurubuni taasisi ziwatengenezee uhalali wa kukubalika," alisema Profesa Safari.

Maoni kama hayo yalitolewa na Profesa Gaudence Mpangalla kutoka Chuo Kikuu cha Ruaha ambaye alisema ni matokeo ya propaganda za CCM.

Alisema Lowassa akiwa CCM, matokeo ya utafiti wa taasisi hiyo yaliyonyesha alikuwa anaongoza kwa ushawishi katika nafasi ya urais.

"Nina shaka na hiyo methodolojia waliyoitumia kwa kweli," alisema Profesa Mpangalla.

Dk James Jesse, mhadhiri wa UDSM, Kitivo cha Sheria pia alikuwa na shaka na utafiti huo.

"Matokeo haya yanaonesha walihoji watu fulani walioandaliwa na hawakuhoji watu mchanganyiko," alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku), Stephen Mwakajumulo alisema kama Twaweza iliweka vigezo sahihi vya utafiti, basi upo uwezekano wa majibu kuwa sahihi.

"Kumbuka mwaka 2005 ilifanya utafiti wa aina hiyo na kueleza kwamba mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete angeshinda kwa asilimia 80 na matokeo yake yakawa kweli,'' alisema na kuongeza mara nyingi utafiti unafanyika ili kutafuta mwelekeo wa ukweli kwa kutumia vigezo muhimu.

Wanasiasa

Mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli (CCM), January Makamba alilalamika kuwa utafiti huo umewapunguzia asilimia za ushindi kwani wanaamini itakuwa zaidi ya asilimia 65.

"CCM haishangazwi na matokeo hayo kwa sababu, Magufuli amefika maeneo ya vijijini zaidi kuliko mgombea yeyote, ameeleza sera zinazoeleweka na ana sifa za uadilifu lakini wanaojadili mabadiliko hawaendani na historia yao, mwonekano wao ndiyo sababu wananchi wamekatishwa tamaa na hoja zao," alisema ambaye wiki iliyopita alitangaza matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ambayo hakuitaja unaoonyesha kuwa Magufuli anaongoza kwa asilimia 69.

"Mafuriko ya (mgombea wa NCCR-Mageuzi mwaka 1995) Agustine Mrema na (mgombea wa Chadema 2010) Dk Willibrod Slaa hayajawahi kutokea hadi sasa. Haya yanayojitokeza kwa Lowassa badala ya kuwasaidia yanawadhalilisha kwa kuwa mgombea wao hana uwezo hata wa kujieleza jukwaani kwa hivyo matokeo hayo yanaakisi ukweli wa hali halisi iliyopo...sasa wanaopinga na wao waje na utafiti wao tuone."

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kabla ya kuzungumzia utafiti huo wataujadili kwa kina kuangalia mazingira yaliyotumika kuufanya.

"Kwanza tuone ulivyofanyika ndiyo tutatolea ufafanuzi," alisema.

Katibu Mkuu wa chama cha Sauti ya Wananchi (Sau), Ali Kaniki alisema matokeo hayo hayawezi kuaminika kwa asilimia kubwa.

"Kuna taasisi Uingereza walifanya utafiti kama huo na chama cha Labour Party kilioneokana kuongoza sana, lakini hadi matokeo yanatangazwa kilianguka vibaya," alisema.

"Lakini inatakiwa kuheshimu utafiti huo na tusidanganyike na hoja za mafuriko. Wanaojitokeza kwenye mafuriko siyo wote wanaopiga kura."

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi alisema matokeo hayo ni chanzo cha kuashiria hatari ya machafuko, hivyo kusingekuwa na sababu ya kutoa utafiti huo kwa muda mfupi uliosalia.

"Ukiangalia ndani yake kuna propaganda za kisiasa zinazochezwa na CCM na inaweza kutuletea shida. Watu wako kwenye presha sana nadhani ingekuwa sahihi kusubiria uchaguzi ufanyike tu."

Mwenyekiti wa UDP mkoani Dar es Salaam, Joachimu Mwakitinga alisema hakuna uhusiano wa hali halisi na matokeo ya asilimia 65 kwa Magufuli. Mwakitinga ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Mamlaka na Taratibu za Uendeshaji Uchaguzi, alisema matokeo hayo ni uchochezi wa kampeni unaoweza kusababisha madhara makubwa kwenye Uchaguzi Mkuu.

Wanaharakati

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk.Hellen Kijo-Bisimba alisema sampuli iliyotumika kwa matokeo ya utafiti huo inaweza kuwa imeathiriwa na mazingira ya maeneo husika. "Wakati mwingine sampuli inaweza kudanganya na kuwa tofauti kabisa na uhalisia wa hali ilivyo na wakati mwingine kuelezea uhalisia wenyewe."

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sikika, Irinei Kiria alisema sampuli ya Watanzania 1,848 ni idadi ndogo na isiyoakisi Watanzania milioni 23 wanaotarajiwa kupiga kura mwaka huu.

"Lakini pia, wiki mbili tangu kufanyika uchaguzi huo ni muda unaoweza kubadili upepo mkubwa wa kisiasa kwa hivyo haiwezi kuwa matokeo halisi kwa hali ya sasa."

Kiria alisema matokeo ya utafiti huo kwa Lowassa na Magufuli ni sawa na usiku na mchana kutokana hali halisi ya kisiasa ilivyobadilika katika uchaguzi wa mwaka huu.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi za Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema matokeo na hali ya kisiasa nchini yanaonyesha tofauti kubwa.

Mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Arusha (Angonet), Petro Ahham alisema utafiti ni mzuri, lakini pengo la ushindi wa CCM ni kubwa sana.

"Kwa hali ilivyo sasa huwezi kusema kuna mshindi wa asilimia 65, labda tuelezwe walioulizwa maswali ni waliojiandikisha tu sio hawa tunaowaona kwenye mikutano," alisema.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Alline Ngirwa alisema utafiti huo umeonyesha ni maeneo gani hasa ambayo wananchi wanakerwa, kwa hivyo utawasaidia katika kipindi hiki wanapojiandaa kuamua.

"Wananchi wanakerwa na huduma za afya, ukosefu wa maji na elimu duni. Kwa hiyo matokeo ya utafiti huu yanatoa mwangaza kwa wapiga kura na wagombea juu ya vitu wanavyohitaji kwenye serikali ijayo," alisema Ngirwa.

Mkurugenzi wa taasisi ya Compas Communication, Maria Salungi alisema utafiti huo si matokeo ya uchaguzi na kwamba katika kipindi kilichobaki kuelekea Uchaguzi Mkuu, yanaweza kubadilika.

"Haya sio matokeo ya uchaguzi ni maoni ambayo yanaweza kubadilika kulingana na wagombea watakavyoendelea kufahamika zaidi kwa wananchi, hivyo jamii isipokee kama ndio matokeo halisi," alisema

Alisema katika utafiti huo, wengi waliohojiwa walitoa majibu kulingana na wagombea kufahamika zaidi, kutokana na majina yao kutajwa mara kwa mara ikiwemo kwenye vyombo vya habari na mabango.

Alishauri vyama vinavyounda Ukawa kuwaelimisha wananchi ambao wanaamini kwamba siku ya kupiga kura, watachagua Ukawa chama ambacho hakipo.

Wananchi

Wananchi waliozungumza na Mwananchi walisema wanashangazwa na matokeo ya utafiti huo, unaoonyesha hakuna mchuano mkali baina ya wagombea wa nafasi ya urasi tofauti na hali ilivyo.

Julian Mgigo, mkazi wa Buguruni alisema utafiti huo umefanywa baada ya waliohojiwa kupatiwa simu na chaja, hivyo huenda matokeo hayo yasionyeshe uhalisia wa mwenendo wa wagombea.

"Kwa maoni yangu naona hilo linaweza kuathiri matokeo halisi ya kukubalika kwa mgombea," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Anasahau, wameshatupanga tutakaotangulia ahela, wao wabaki, hawajui tumechoka? point ya wasiosoma na wazee kwa nini iwe advantage kwa ccm?

Tanzania haijawah kutendewa haki na wasomi na wanataaluma.

Nchi itaangua ktk machafuko yalaZma.

ili aslimia za CCM zitoshe ilibidi kuchukua kundi linaloamim Magufuli atapata asilimia nyingi, ni watu wachache Sana utawaaminisha kwamba Magufuli anamshinda Lowasa. Hii ni dalili mbaya kwa wapiga kura.


aidha hii ni ili kauli za kuingia ikulu zibebe mashiko
 
Waacheni watapetape kwa tafiti za kimagumashi, Oct 25 tutamaliza kesi.
 
huyu main presenter wa huu utafiti ameshindwa kuwa professional kwa kupresent takwimu kulingana na utafiti waliofanya ( kama kweli ni legitimate results) anatumia muda mwingi kudefend matokeo hata kama umati haujauliza swali, kuonyesha uhalali wa matokeo yao, ameonyesha mapenzi ya dhati kwa ccm hasa aliposisitiza magufuli hana ufisadi, sijui ndo anataka akumbukwe kwenye nafasi za kuteuliwa na magufuli, anaonekana very arrogant,plz be professional, it is a shame to academicians and intellectuals
acha fisadi aitwe fisadi
 
Twaweza imekua jumba la porojo na wanajishushia heshima yao! Yan wameshazaraulika kupita kiasi hawana hadhi tena hapa Tz! ofisi yao sasa waifanye tawi la ccm
 
Wameudhi sana bora wasingeonyesha tafiti hizo mana ndo wameongeza kasi ya kumtaka lowassa.
 
Twaweza ni jimbo ngome la uchaguzi la ccm.
Acha wafanye upuuzi wao,
tutawaonyesha hapo otkb 25.2015,
ila nawashukuru kwa sababu ukawa tutapiga kasi zaidi kukampeni kwa siku zilizosalia.ok.
 
Aidani Eyakuze ni Mkurugenzi mkuu wa Tweweza east africa, namfahamu sana kijana huyu aliechukua nafasi ya Rakesh pale Twaweza. Eyakuze ni rafiki mno tena wa karibu sana na January Makamba, na katika ile proposal concept ya Makamba pale Mlimana city ya kutanganza nia pale mlimani Eyakuze ndie aliekuwa consultant mkuu wa ile proposal ambayo leo kwa kiasi kikubwa imekuwa adapted na Mgombea wa CCM Magufuli na makamba kuwa karibu kuhakikisha inatekelezeka mfano kuipa kila kijiji sh milioni 50.

BADO naconect urafiki wa Eyakuze na Makamba katika takwimu alizozitoa Juzi ktk media january na leo za twaweza....ni km watu wanalala na kuamka pamoja.

Kwa thread hii, Aidani Eyakuze ameidhalilisha taasisi kubwa kama Twaweza kwa kununuliwa na ccm kupitia January na kupika tafiti zenye kuifurahisha ccm...hii ni hatari sana kwa taaluma ya Aidan Eyakuze ambaye Taasis yake inaeshimika kwa tafiiti zenye kulenga kuboresha mambo mbali mbali kwa serikali kwa watu wake. mfano mmoja ni Elimu kwa kupitia mradi wake wa UWEZO Tanzania inafanya tafiti na kuipa mrejesho serikali kwa chanamoto mbali mbali za ukweli toka kote nchini na serikali kupitia wizara ya elimu na TAMISEMI mara nyingi imeonyesha mabadiliko na kufanya utekelezaji kwa baadhi ya maeneo hayo Muhmu. sasa My take ....kama ccm inakununua Aidan..hivi chama hiki kikiwa madarakani kiendelee kuamnini na kufanyia kazi tafiti zako zijazo?? na hasa sasa nasikia mtaongeza evaluation katika afya na mazingira?

Aidani..sio masikin wa hela kwa elimu na nafasi yake pale twaweza...uswahiba wake tena wa siku nyingi na January anaamua kupindisha taaluma yake na taasis yake kutoa matokeo ya kufurahisha ccm....hii aitosh kuzuia maamumuzi ya wananchi wanaotaka mabadiliko ambayo UWeZO Tanzania imevumbua madudu mengi tu uko chini katika tafit zake za elimu kwa miaka 5 mfululizo.....Aidan wanishangaza sana....

IMAGE ya Twaweza na UWEZO Kenya, Uganda na Tanzania inaenda kuingia doa na dosari kubwa sana kwa upenzi huu binafsi wa Aidan Eyakuze na January Makamba.....

Hivi dhambi hii kwa CCM, January na Aidan mtaungamia wapi...ili hali nafsi zenu zinajua mnafanya hujuma ya makusudi.....shame on YOU Aidan na Shame on Makamba.....

Mungu akupe uhai mrefu Mr Rakesh, ata kama Mkapa alikuwa rafiki yako sana ulimkosoa sana na kumpa fact wakat wa "HAKI ELIMU" hadi ulipooingia TWAWEZA hukusita kufanya hivyo kwa Kikwete na mengi tumeyaoona yanabadilika.....lakini kwa aliechukua Kijiti chako AIdan eyakuze huku sio tena ameendeleza ameamua kufanya Twaweza na UWEZO kuwa taasisi Ndogo za CCM.....shame na kwa washauri wake Uganda, tanzania, na kenya......
Nilikuwa napitia report nzima ya Twaweza, kama mtaalam wa utafiti naweza kusema kuna madhaifu makubwa kadhaa...

1. Methodology (technique) iliyotumika

2. Variable ya age hasa kwenye swali la 4 (nani utamchagua) haisapoti results obtained/conclusion. Kwenye inferetial statistics haijawahi kutokea kitu kama hicho, hii ya Twaweza ndio ya kwanza dunia nzima

3. Respondents kupewa simu na power bank ni unethical kwa maana nyingine respondents alikuwa na probability ya 95 c.f ya kuwa influenced

4. Kufikia sample ya watu 1800 kwa "enumeration" ina maana wamehoji kaya 200 tu Tanzania nzima. Na kaya hizo hawajatuambia kama wametumia stratified sampling techniques kwanza kabla ya kufanya random sampling huku wakijua Tanzania ina mikoa/wilaya etc

5. Results za Twaweza kwenye age varible hairespond na taarifa za tume ya uchaguzi... Na kiitafiti hii ndio njia rahisi kujua kama data ni cooked.

Mytake: Tusiyumbe wala kutetereka. Kuna tafiti ambazo nafkiri zitakuja na kutupa reliable & valid data kuliko hii ya Twaweza ambayo imepikwa na January, Aidan na Maria Sarungi
 
Anasahau, wameshatupanga tutakaotangulia ahela, wao wabaki, hawajui tumechoka? point ya wasiosoma na wazee kwa nini iwe advantage kwa ccm?

Tanzania haijawah kutendewa haki na wasomi na wanataaluma.

Nchi itaangua ktk machafuko yalaZma.

ili aslimia za CCM zitoshe ilibidi kuchukua kundi linaloamim Magufuli atapata asilimia nyingi, ni watu wachache Sana utawaaminisha kwamba Magufuli anamshinda Lowasa. Hii ni dalili mbaya kwa wapiga kura.


aidha hii ni ili kauli za kuingia ikulu zibebe mashiko

Magufuli amzidi Lowassa haitakaa itokee hadi dunia hii iwe mwisho. Ni kichekesho cha karne kuwa Magufuli ghafla amemzid Lowassa kwa 46%. Hawa watu ni bure kabisa tafiti mbovu!
 
Anasahau, wameshatupanga tutakaotangulia ahela, wao wabaki, hawajui tumechoka? point ya wasiosoma na wazee kwa nini iwe advantage kwa ccm?

Tanzania haijawah kutendewa haki na wasomi na wanataaluma.

Nchi itaangua ktk machafuko yalaZma.

ili aslimia za CCM zitoshe ilibidi kuchukua kundi linaloamim Magufuli atapata asilimia nyingi, ni watu wachache Sana utawaaminisha kwamba Magufuli anamshinda Lowasa. Hii ni dalili mbaya kwa wapiga kura.


aidha hii ni ili kauli za kuingia ikulu zibebe mashiko

Hayo machafuko atayaongoza nani? Fisadi Lowasa ama?

 
Kimeanza kunuka👇👇👇

Hi Prof. Nimetaarifiwa na baadhi ya watu kuwa ninyi mnasema Jenerali Ulimwengu na Dr. Alexander Makulilo watakuwa wanajadili utafiti wa Twaweza na mnarusha katika vyombo vya habari. Tafadhali naomba ufanye kazi professionally. Mimi nilikwambia sitaweza kufanya kazi hiyo. Nilipendekeza uonane na prof. Bakari. Kwa ujumbe huu naomba mtoe jina langu katika shughuli yenu haraka sana vinginevyo nitachukua hatua za kisheria. Nakuheshimu sana naomba tuheshimiane.

Message from Dr. Alexander Makulilo (Political Science UDSM)
 
Back
Top Bottom