Taswira ya Mlimani City Complex - Dar es Salaam (top view)

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
i935_mlimanicitycomplex.JPG
 
Thanks ulotuwakilishia picha hii........naona maeneo mengi yako wazi hakuna majengo hivyo viwanja vinauzwa ??
 
Thanks ulotuwakilishia picha hii........naona maeneo mengi yako wazi hakuna majengo hivyo viwanja vinauzwa ??

hivyo viwanja haviuzwi mama, hiyo yote ni mali ya Chuo kikuu na hata hiyo complex ya Game city (Mlimani city) imejengwa kwa nguvu ya mafisadi, viwanja ni vya reserve ya chuo kwa ajili ya chuo future plan
 
Na ili pawe na hadhi panapaswa kubaki hivyo na nafasi,sio chuo kama manzese! makelele ya taarabu na midundiko,maprof watakonsetreti vip!
 
Hivi kile kituo cha mafuta maarufu kama Shell, hakihamishiki pale mbele ya complex hiyo?
 
picha ya zamani hiyo lakini, barabara ilikuwa bado ikijengwa. hope it looks much different now.
 
Katika hiyo picha barabara haijakamilika, na ile parking pale Mlimani haionyeshi na jengo bado halipo, si 47 bali 46!!!

unajua wabongo walio wengi wapo kama wewe! mimi nimefanikiwa kutoa taswira hii, sasa wewe unayejua kwamba kuna parking lounge, barabara nzuri nenda kapige hizo picha halafu uje kupost hapa! nawasiwsi kwamba wewe ni fisadi wa mawazo!
 
hivyo viwanja haviuzwi mama, hiyo yote ni mali ya Chuo kikuu na hata hiyo complex ya Game city (Mlimani city) imejengwa kwa nguvu ya mafisadi, viwanja ni vya reserve ya chuo kwa ajili ya chuo future plan

Hiyo future plan ya baada ya miaka hamsini ndio iwe mali ya chuo. Unadhani after 50 years bado watanzania watakuwa wanahitaji majengo kama haya ya MLIMANI CITY.
 
jamani natafuta Bunju b kwa masister kwenye Googlearth nitapata wapi inapoonekana poa?

Picha za Googlearth ni za zamani mama. Kwa picha mpya nadhani inabidi ununue software ambayo sio ya burebure.

Ila kama unazihitaji hizo za zamani, inabidi u-install software yake ndio unaweza kuzichungulia, au umuombe mtu aliye-install tayari aiweke kama kwenye alivyofanya huyu muanzisha thread.

I hope that helps.
 
Hiyo future plan ya baada ya miaka hamsini ndio iwe mali ya chuo. Unadhani after 50 years bado watanzania watakuwa wanahitaji majengo kama haya ya MLIMANI CITY.

hilo nalo neno! unajua inauma sana! utakuta hao jamaa kwasasa wanachuma tu na hata kodi sijui kama wanalipa, nadhani kwavile mkataba unasema baada ya miaka 50 inakuwa mali ya TZ basi hapo nahisi ni kodi free!
 
Kiukweli mliman city sio city tena!! Kwa wale ambao hawajui plan haikuwa hiyo kabisa, plan ilikuwa nzuri na ya kuvutia ambayo ingeweza kuleta watalii hata kutoka nchi za jirani na mataifa tajiri na kutoa vyanzo vya ajira kwa maelfu ya watanzania, kilicho fanyika ni uroho tu wa masifa na kukuapa mapato haraka, yale magodauni wanayo jenga hayakuwepo kwenye original master plan. Ukienda GImcoafrica kuna model na master plan yake. Kilicho fanyika utatoa machozi

Kale ni ka kariakoo tu hamna kitu
 
Back
Top Bottom