TASUBA kuongeza kozi mpya za sanaa na utamaduni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea na kujadili taarifa ya Utekekezaji wa Majukumu ya Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) ambapo imeishauri Serikali iendelee kusimamia Taasisi hiyo ili izalishe wataalam wengi kwenye Sekta ya Utamaduni na Sanaa.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Oktoba 24, 2023 Jijini Dodoma, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Taasisi hiyo ina mpango wa kuanzisha kozi tatu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada ambazo ni Urithi wa Utamaduni na Utalii, Usimamizi wa Sanaa na Masoko pamoja na Uzalishaji wa Muziki.

"Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo katika kukidhi mahitaji ya Soko la ajira na kujiajiri kwa vijana, Serikali imeendelea kufanya ukarabati katika Taasisi hiyo, kununua vifaa pamoja na kuongeza idadi ya wanachuo" amesema Mhe. Ndumbaro.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mussa Sima ameiagiza Wizara iongeze kasi katika kuboresha mazingira ya Chuo hicho ili kiweze kudahili Wanafunzi wengi zaidi.

Wakichangia taarifa hiyo kwa nyakati tofauti Wajumbe wa Kamati hiyo, wameishauri Serikali iendelee kuisimamia Taasisi hiyo ili iweze kuzalisha wadau wa Utamaduni na Sanaa wanaolinda, Mila na desturi za Kitanzania pamoja na kuangalia namna wasanii wanavyoweza kupata leseni kutoka katika Taasisi hiyo kabla ya kuanza kufanya Sanaa kama ilivyo kwa Taaluma nyingine ikiwemo Uhasibu ma Sheria.

F9M-4Q-XIAEGkan.jpg
F9M-4kuXYAA59mi.jpg
F9M_AwfW8AAWEli.jpg
F9M_EW7XwAAdvh4.jpg
 
Back
Top Bottom