Tapeli kaja kama Mwalimu

mkakaflani

Senior Member
Sep 30, 2023
119
277
Hatimae yule tapeli aliyekua analalamikiwa hapa jukwaani, baada ya kumpiga bodaboda wa jamaa 50K, amekuja inbox kwangu kama mwalimu ili ampige kibunda bodaboda wangu na aniharibie kabisa uaminifu kwa jamaa (bodaboda).

Ila Kwa sababu somo nililipata humu, imebidi nimpigie mwalimu kuhakiki kama namjua na kujua kama kweli ana uhitaji wa usafiri.

Cha ajabu kapokea anaongea kama amebugia kiazi Cha moto, nimerudia kupiga anakata na saivi ndo hapatikani kabisa.

Mtanisamehe Kwa uandishi mbovu.
View attachment 2785700
 

Attachments

  • IMG_8789.jpeg
    IMG_8789.jpeg
    22.5 KB · Views: 4
Ile namba ya polisi na tcra.nimeipiga block.

Maana unaripoti lakini hakuna taarifa yo yote inayorudi.wao kazi yao kukutumia meseji tu.

Ilitakiwa wawe wanakurudishia mrejesho.bwana namba uliyoiripoti mwenyewe tumeshamkamata yupo kituo fulani njoo.

Lakini hamnaa.kazi kujaziana meseji tu.

Na wao wamekuwa matapeli sasa.
 
Sasa na namba ya huyo tapeli umeificha, weka wapa na namba yake, hueñda mamlaka husika zikaona na kumtia hatiani
 
Sijakuelewa kwa ungetoa namba ingekuaje ?
Atawasiliana na boda afu atajifanya ananijua sana Mimi ili kuweka uaminifu kwa boda,baadae atampa maelekezo ya kumuwekea kiasi cha pesa kwenye simu,Kwa kisingizio cha ukosefu wa huduma za mtandao husika maeneo hayo na atamrudishia pindi atakapofika.
 
Mbona kama hueleweki kiongozi
Atawasiliana na boda afu atajifanya ananijua sana Mimi ili kuweka uaminifu kwa boda,baadae atampa maelekezo ya kumuwekea kiasi cha pesa kwenye simu,Kwa kisingizio cha ukosefu wa huduma za mtandao husika maeneo hayo na atamrudishia pindi atakapofika.

Na hapo boda akiwa mshamba atakua kapigwa na kitu kizito, maana jamaa hatopatikana tena na muamala umefanikiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom