Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
Pole Mkuu, hayo ndiyo majaribu ambayo Mungu anampitisha mja wake. Lakini pia yeye ni ni mwingi wa fadhila na naamini atakujalia moyo wa uvumilivu. namuombea mtoto apumzishwe mahali pema, amina
Ndugu zangu,
january mwaka huu nilikuja hapa na habari za furaha kuu za kupata mtoto wa kiume (angalia link hiyo hapo chini)
https://www.jamiiforums.com/mahusia...a-kiume-mama-na-mtoto-wanaendelea-vizuri.html
leo hii nina huzuni kuu pia, Mwenyezi Mungu muweza wa yote kamuita mtoto huyo kurejea kwake na kutuacha na majonzi makubwa nisiyoweza kuyaeleza vyema. machozi mengi sana yamenitoka, ila sina la kufanya zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
RIP mwanangu mpendwa