Tanzia: LiverpoolFC afiwa na mwanae

Nashukuruni sana ndg zangu,hakika nimempata salaam zenu na sina chochote cha kusema zaidi ya kwmb natambua sana salaam zenu tena sana na naiheshimu sana kama ilivyoada yetu humu jamvini,Zaidi ni kwmb kama alitangulia kusema Mzee Wa Rula ni hakika tumempoteza mtoto leo saa tatu na nusu asubuhi ktk hosptal ya Mount Meru ambaye alizaliwa tar mwezi uliopita na ghafla tar 5/12/11 alibadilika na tukampeleka hosptali na mpk leo mauti yanamkuta na hakika Mi pamoja na familia tupo ktk wakati mgumu kwn hakika tulimpenda sana ila MUNGU mwny uweza wa yote amempenda zaidi na mtoto alikabiliwa na ugonjwa ambao madaktari wa Sefsis na sikuweza kuwanukuu vema lakini nakumbuka wameniambia hivyo na mazishi tumefanya leo hapa nyumbani. Kwa kweli wanaJF nimewakubali ktk umoja tulionao kw muda wowote mtu uitajipo. Nawashukuru wote mlioguswa na kifo cha mtoto wetu! Muwe na wakati mzuri na zaidi tumtukuze MUNGU mwenye uwezo!

.........Maskini jamani, pole sana.
 
Pole sana mkuu kwa msiba ulowapata. Najua inauma sana tena maumivu yake hayaelezeki hasa kwa mama mtoto. Mungu azidi kuwatia nguvu na kuwapa faraja.
 
pole sana livapuu na familia yako nzima kwa msiba uliowafika,
BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina lake lihimidiwe...!!
BWANA MUNGU BABA wa mbinguni atawafuta machozi na kuwapa faraja yake iliyo kuu ipitayo faraja zote za wanadamu.
 





















Ndugu zangu wote wa hapa jamvini!!!! Sina mengi ya kusema katika hali yoyote ile iliyonikuta ila ni MUNGU pekee ndiyo awape nguvu ya kipekee na moyo huu uendelee kwa yoyote yule apatwaye na janga lolote kama hili:


Sina Mengi zaidi ila ntarudi after:


LiverpoolFC Member Arusha:




 
Pole sn, Inshaallah Mungu atawapa subra na muweze kukabiliana na hili. Na Inshaallah Mungu atawapa rizk nyengn.

Naamini madhal mlingoti umesimama, kupandisha bendera huwa si kazii.

Pole baba eenhee!!
 
Pole sana wanafamilia kwa kumpoteza mtoto wenu mpenzi. Mwenyezi mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu kwenu. Poleni sana
 
Pole sana Mkuu LiverpoolFC Maisha ndo iunabisd yasonge tena....Mungu atakujaali mwengine:sorry:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom