TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

View attachment 318027

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.

Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.

Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.

Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

View attachment 318124
Atangulie tu.alikuwa mbabe sana.
 
NI kweli mkuu upo sahihi huyu mama alionyesha ubaguzi wa wazi ktk bunge la katiba dhidi ya wazanzibari weupe sijui ndo hao wanawaita Hisbu. Alisema Zenji ni ya watu weusi. Aiseee akapumzike panapostahili. Huenda Mungu ana maskusudi yake kumtwaa sasa hv ktk kipindi ambacho Zanzibar inapita pagumu kwenye viashiria vya ubaguzi.
Ni kweli kabisa mkuu, watu aina ya huyu mama ni hatari sana, hawapaswi kuwepo kwakweli, wanaweza wakatusabishia machungu yasiyopimika, wako tayari nchi isambaratike kwa kulinda maslahi yao.
 
Watu wengine na Mungu wao.
Huyu kiumbe alitesa sana watu. Hata kupendekeza mapinduzi na kumwaga Damu ndio wachukue serikali.
Alikuwa chombo kizuri kwa Shetani na Damu za watu.
Alitamani sana watu wauane kwa mstakabali wa Zanzibar. Sio mfano wa kuiga na wala kupewa nafasi tena FINDISHO KWA KATIBA YA TANZANIA
 
Pumzika Kwa Amani Mama.Wewe Ni Mwanamke Shujaa Na Ulipigania Kwa Nguvu Zote Ulichokiamini.#RIP
 
Namnukuu: na mimi namwambia jussa sasa zanzibarrrrr ni nchi ya kimapinduzi serikali ya kimapinduzi haitolewi kwa karatasiiiiii labda watupindue na uwezo huo hawana maana sisi ndio wenye mamlaka. CHUNGENI NDIMI ZENU
Hapa kwenye mamlalaka mimi ndio palinisumbua ni sisi binadamu au akiye juu?
 
Mimi nashangaa sana .hata marehemu alipanga foleni na akapewa karatasi za kupigia kura .lakini kulikuwa na umuhimu gani kwa mama yetu kupanga foleni ya kupiga kura wakati kura haitaleta mabadiliko
 
Hii ardhi iko siku kila mtu ataiwacha .tupendane na tusifarajane kwa sababu ya kuitawala ardhi
Hii ardhi mtawala wake ni mmoja tu .
 
Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuun

Sisi Sote Ni Waja Wa MWENYEZI MUNGU Na kwake Tutarejea
 
kuwa na UTU japo kwa sekunde moja. siasa isikufanye ukawa na chuki kiasi hicho. unafurahia kifo cha binaadam mwenzio?
mimi naona yupo sahihi, mtu anayesema hawatatoa nchi kwa njia ya karatasi labda mapinduzi huyo ni mchochezi hafai kabisa kuendelea kuwepo, angeweza sababisha hata vita kwa haya maneno, ila wa tz ni wapole, alipaswa kushtakiwa huyu
 
mimi naona yupo sahihi, mtu anayesema hawatatoa nchi kwa njia ya karatasi labda mapinduzi huyo ni mchochezi hafai kabisa kuendelea kuwepo, angeweza sababisha hata vita kwa haya maneno, ila wa tz ni wapole, alipaswa kushtakiwa huyu
Huyo mama alikuwa sahihi kwa 100% kuwa serikali ya mapinduzi haiwezi ondolewa madarakani kwa makaratasi labda kwa mapinduzi, na aliwapa challenge kuwa wapindue, na mimi nasema wapindue ili waingie madarakani.
 
Back
Top Bottom