Tanzania yapewa sifa na USA

Smarter

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
527
110
“Kabla ya kupanda hapa jukwaani kuzungumza nanyi, mliniona nazungumza na simu…alikuwa Balozi wa Marekani, ananiuliza kama nimesikia hotuba ya Rais Obama jana usiku kwenye Umoja wa Mataifa,” alisema Rais Kikwete.“Nikamwambia niko huku nahangaika, nitasikia saa ngapi? Wakati mwingine niko hoi bin taaban hata kusikiliza redio au televisheni huna muda.“Ameniambia kuwa Rais Obama ameeleza misingi ya Marekani kusaidia nchi zinazoendelea, na mfano wake akatoa Tanzania.

Akasema nchi yetu inaongoza kwa kujali utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu NGO,s, na tunatawala vizuri,” Rais Kikwete aliwaeleza wananchi.

“Kama siyo mimi na akina Mwandosya, nani mwingine anayemsifu,” alisema Rais Kikwete akimtaja Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, ambaye alikuwapo kwenye mkutano huo akiwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Mbeya.

Alisema kauli hizo za Marekani kuisifu Tanzania, hazitoi yeye, lakini kila anapofanya hivyo, baadhi ya watu huhoji kwani kila mara na Marekani.''


MY COMMENTS:
Ni sifa zipi zenye msingi Asifiwae Tanzania? Nyanja silizo sifiwa "utawala bora, utawala wa sheria, kuheshimu NGO,s, na tunatawala vizuri" Sitaki kuwa mshabiki, Sijaona chamsingi kwenye sifa hizi, Na unapo rejea sifa sidhani Marekani inaweza kuwa kirejesho cha sifa, Naamini Kwa yale maendeleo halisi na mipango sahihi ya maendeleo kwa mtanzania Marekani haiwezi kuisifia;
Mfano halisi, One cow per family hii project ya Rwanda ilikosa mfadhili, wana magharibi wakasema haina tija n.k, Wao Rwanda wakaifanya and results ni nzuri, PALIPOKUWA NA NYASI taratibu mabati yakanunuliwa, afya nakadhalika; Kwa project tangible and zenye magnificent results kamwe hawana support wala sifa za waziwazi,
Elimu na Afya bure, [Hili lawezekana,ila pia Hao watoa sifa hawawezi kulisifia, wanajua likifanikiwa hapatakalika;

Anyway, lets see.......




Ignoring the fact does not change it,
 
Smater,

..Tanzania inasifiwa kwa kuandikisha watoto wengi shule ya msingi.

..wangeangalia quality ya elimu wanayopewa watoto hao nina hakika kungekuwa na habari nyingine kabisa.
 
Si huyu ni matonya wa Tanzania?!. Anaona akisifiwa na Marekani basi hao watu wa Iringa watatoa kura sio? Ama kweli akili ni mali.
 
mpumbavu huishi kwa kusifiwa na kuamini kila analoambiwa ama alionalo,
bali mwelevu huangalia sana atokako na yuko wapi, anakwenda wapi.
watu wa iringa hawishi kwa sifa za kutolewa na marekani kwani je zitawasaidi vipi na mfumo mgumu wa maisha
unaowakabiri??
 
That's what we call remote assessment which is always fallacious. Mwambie aingie bongo vijijini ndo aone!
 
Obama ni mnafiki, Kenya ambako ndiko shina lake limetoka wamebadili katiba yao juzi juzi, lakini kwa kuwa wamewaudhi wamarekani kwa kumualika Omar Bashir wa Sudan, basi hakuongelea jambo hilo kubwa sana Africa ambalo ni very very rear kutokea-- Kubadili Katiba kwa amani na mshikamano sio kitu kidogo. I think ilideserve kuwa mentioned kwenye hotuba yake, but poor guy siku hizi anaogopa hata kutaja Africa, kwa jinsi wamemkalia vibaya na ngozi yake, basi ni tabu kweli kweli
 
Back
Top Bottom