Ndugu zangu naomba tutafakari kidogo na hii hadithi ya EL kuendelea kuwepo katika midomo na mawazo ya watu katika kuwania urais 2015, hii ikiwa pamoja na kashfa zote na hii sera ya kujivua gamba kuonekana inamuogopa. Sasa basi kama hamna lolote litakalotokea na akiweka watu wake NEC 2012 basi njia ni yake na ukichukulia kwamba Mwinyi na Mkapa wote walishindwa kumuachia kiti mtu wao, basi na JK hatoweza, EL anakua rais 2015, japokua wanasema a week in a political life is a long time, lakini Tanzania yetu hatujafika hapo siasa za kinafiki zisizokomaa bado zinatawala kwa hiyo 2015 ni kesho tu. Sasa serikali, ccm, tanzania ya EL itakuaje? tusafiri kidogo hadi mida hiyo tujionee as time travel is always a human fascination.
Kwanza huyu jamaa ameutaka urais toka 1995 na 2015 itakua ni miaka 20 kamili lazima ataunda serikali ya Ki-Lowassa Lowassa yaani itakua na marafiki, wapambe, na loyalists bila kujali ari, uwezo, upeo wa uongozi na uzalendo wao kwa taifa hili. Kumbuka hii itakua ni kama sherehe lazima walioumia nae miaka yote hii wazawadiwe. Tumeliona hili kwenye serikali hii ya Kikwete na jinsi linavyotuumiza kwa sasa kwa kua a mawaziri na viongozi wanaolindana na wasiokua na uzalendo, uwezo na wala tija ya kazi. Hapa majina kama Mahanga,Karamagi, Chenge, Nchimbi, Malima, Sofia Simba, Masha, Kapuya etc yatarudi tena katika uongozi, wote wana matatizo katika uongozi
EL anaamini ana maadui wengi waliomletea matatizo katika njia yake takatifu ya kupata urais na jinsi alivyo hawa lazima wawajibishwe, hizi ni siasa za visasi. Tofauti na Mkapa aliyeunda serikali ya umoja katika CCM na Kikwete alielipiza kisasi kwa kiwango kidogo kutokana na character yake na imani yake, EL anaona ameonewa na kunyanyaswa siyo kisiasa tu bali hata utu wake na hii ni very personal kwake kwa kua anaamini yeye ndiye aliyekua anafaa muda wote kua rais ila aliwekewa fitna. Hii kwanza ni tabia ya kujiona wewe uko sawa kila wakati na unaonewa tu hata ukifanya makosa ni tabia isiyo faa katika uongozi wowote hata wa familia. Hii ndugu zangu itaathiri utendaji wa serikali yake kwa kua nguvu za ziada zitaelekezwa kwenye hili na siyo kusaidiana kujenga Taifa kwa kushirikiana na kusikiliza mawazo ya wote.
Kwa kiongozi aliyejiuzulu na skendo iliyomuhusu yeye mwenyewe ni vigumu baadae kuchukulia hatua au kuziba mianya ya wizi na ubadhirifu serikalini na ukichukulia yeye na watu wake wa karibu ni wafanya biashara kwenye nchi isiyo na uongozi madhubuti wa kisheria basi hatutakua na budi kuangalia maozo ya serikali zote zilizopita siyo tu yakiendelea bali yakiongozeka pia katika muda wake wa utawala.
Nyerere hakumtaka Lowassa na Malecela kwa sababu mbili tofauti, Lowassa kwa ugeni wake katika ngazi za juu za maamuzi ya nchi na chama na fedha zake za haraka haraka alizozipata kwa kipindi kifupi. Na kwa upande wa Malecela kwa sababu ya Kutaka kuhodhi madaraka yote ya Kichama na serikali. Network ya Malecela ilikua tishio kwenye CCM ambapo Nyerere hakutaka mtu mmoja kuwa na nguvu kuliko chama so akawaengua wote.Fast forward 2011 EL siyo tu kwamba ameongeza hela pia ana nguvu kwenye chama ambayo hakuwa nayo 1995 na hii ni shida kwa demokrasia yetu changa kichama na kitaifa.
Hii ina ubaya na uzuri wake. Ubaya ni kwamba hamna mtu atamkosoa kwenye chama, serikali, na atatumia nguvu hizi za umoja huu kudidimiza uhuru wa habari, upinzani na demokrasia nchini. uzuri unaweza kua ataweza kuharakisha mambo yafanyike haraka zaidi kwenye ngazi zote kichama na serikali, lakini je kama ataunda timu dhaifu haya mazuri hatutayaona kwa sababu serikali siyo mtu mmoja/rais serikali ni timu. Kama Nyerere's one man show ilishindwa EL hatoweza.
Tofauti na wenzake Rais EL atataka kiti cha urais kiwe karibu nae hata wakati akiwa amestaafu. Hapa tutaona atakavyojipa nguvu aogopewe kichama na kiserikali ili apate nafasi ya kumchagua mrithi wake 2025. Kama tulivyosema hapo juu atajipa nguvu kwa kuengua maadui, kujaza nafasi zote kwa watiifu wake, kubana vyombo vya habari au kutumia marafiki kuvinunua kama wanavyofanya sasa hivi, na kumaliza nguvu za wapinzani kwa kupachika watu wake ndani ya upinzani na kutumia nguvu za dola ambazo inaaminika ana uhusiano nao vizuri. siasa za urithishaji viti zitakua zimeanza rasmi Tanzania.
EL ana kiburi kisichofaa katika siasa za nyakati hizi za uwazi, ushirikiano na demokrasia zaidi. Kwani Katika skendo yake alijishirikisha mwenyewe sana bila kujali matatizo yanayoweza kumkuta na baada ya hapo hakupanga kuongelea hili kiundani na Rais, Spika wala kamati ya Bunge kumnusuru alikaa kimya kijeuri akiamini ataogopwa hatoguswa kinyume chake kamati ikafanya kazi ikabidi awajibike kwa shingo upande na kuanza kutafuta wachawi kila kona kusababisha nyufa wenye chama na serikali ambazo zimeathiri wananchi kwa kiasi kikubwa.
Je ujeuri huu, ubinafsi huu, umungu mtu huu unatusaidia vipi katika matatizo yetu Watanzania? Nafikiri haitusaidii kua na kiongozi wa aina hii haswa katika muda huu ambao tunataka uongozi unaoweka maslahi ya taifa kwanza.