Tanzania: Vyama vya upinzani vyanyimwa ruzuku Rasmi

Utaratibu wa benki kuu malipo ya cheki ni yasiyozidi Tzs.10,000,000 tu na zidi ya hapo ni transfer au cash deposit. Yawezekana kabisa voucher ndo msajiri hajapeleka hazina kwa sababu zake.

Nakubaliana na utetezi wako kwamba Msajili inawezakana hajafikisha hazina, bila yeye kufikisha voucher aliyoimwagia winu wake kama msajili wa vyama vya siasa Hazina haiwezi kufanya cho chote, ni utaratibu wa serikali yetu.
 
Hiyo ndo bongo ni full ubaguzi, yaani pesa za walipa kodi anakalia mtu mmoja, huu ni upuuzi mtupu! Ndo maana nasema viongozi wetu mara zote wapo kwa ajili ya kutugawa na si kutuunganisha! Uzalendo ni sifuri, tendwa ukimuona tu una pata picha ni mwakilishi wa ccm!
 
Naona ni bora zifutwe kabisa maana huku ndio moja wapo ya kuharibu pesa za uma. Pesa hizo zingepelekwa katika ustawi wa jamii na kuengezea mishahara waalimu.
 
Hayo ndiyo madhara ya jeuli maskini. Alijua tu mtaenda kupiga magoti kwake. Si nilisikia hamtashirikiana na Tendwa au hana sehemu ya kusaini au mlijisemea tu bila kujua maana halisi ya msemo wenyewe. Poleni si muanzishe omba omba nyingine kabla hawajaamka watawapeni. Nashindwa kuelewa hiki chama kikishika dola omba omba yao si ndo itazidi? Tukana lakini ukweli upo, je ulishawahi kuambiwa hata makusanyo yaliyopatika kwa uhamasisho wa Jr ni kiasi gani?

USIMWAMSHI ALIYE LALA!
 
Wadau,

Katika kile kinachoonekana kuwa ni kudhibiti vya vya upinzani hususani CHADEMA, msajili wa vyama ameamua kukalia cheki za vyama hivyo na kutoa cheki ya CCM.

Huku vyama vingine vikiendelea kukalia kuti kavu, kwasasa bwana Tendwa ameamua kuonyesha U-CCM wake moja kwa moja baada ya kuelezwa kuwa hela wanayoipatia CHADEMA (ambayo ni halali kuipata) ndiyo inayoimaliza CCM kwa CHADEMA kujijenga zaidi.

Hivyo basi, wakaamua kukalia ruzuku za vyama vingine kwa kisingizio kuwa CHADEMA wakilalamika wataambiwa mbona hata CUF wala NCCR hawajachukua? Ila ukweli ni kwamba lengo ni CHADEMA na vyama hivi vingine vinaelewa mchezo mzima baada ya mbinu ya CCM ya kuitumia CUF kufa kabla ya utekelezaji.

Tuko hapa ofisini huyu msajili anakera sijui Demokrasia anayoisimamia ni ipi? Ofisi nzima tumeduwaa kwakuwa tumeona hizo cheki na CCM kupewa yao ila wengine hususani CHADEMA hakuna!

UPDATE:

Baada ya Habari hii kuingia humu JF Leo Tarehe 06/10/2012. Ninavyoandika hapa, tumeitishwa kikao cha dharura, aliyeitisha anasema sababu ya kikao hicho ni kutotunza siri za ofisi na kuanza kuliki kwenye mitandao ya kijamii, kwa yeyote anayetaka kujakujua ukweli aje aone kama atapata huduma.

Ila ninachosikitika kuna watu humu ofisini wameazwa kuhisiwa kutoa taarifa kumbe siyo wao.Nitawajuza nini kiliendelea baada ya kikao.

Tunashukuru kwa taarifa, wasifikiri watanzania wote wapo tayari kufumbwa midomo kwa madudu yao..!
 
Chadema wanyimwe ruzuku wanatumia hela vibaya sana kwenye maandamano yasiyo na maana!
 
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu

Umechangia bei ngapi hadi sasa brooooo?????????? Waswahili bwna?????? unaakili za kitoto kweli........kwani ruzuku kwa vyma vya siasa ndo waifahamu leo...........bora urudi bgmyo ukaendelee kulisakata segere saigoni.
 
Tunashukuru kwa taarifa, wasifikiri watanzania wote wapo tayari kufumbwa midomo kwa madudu yao..!

Tendwa ni mlevi wa madaraka na wakuogopwa kama ukoma, anaonekana ana choyo sana yule mzee! Pesa za walipa kodi bado anazibana?! Kama angekuwa anazitoa mfukoni sijui ingekuwaje?! Poor Tendwa! Atakuja kuishi uhamishoni kwa aibu!
 
Nakubaliana na utetezi wako kwamba Msajili inawezakana hajafikisha hazina, bila yeye kufikisha voucher aliyoimwagia winu wake kama msajili wa vyama vya siasa Hazina haiwezi kufanya cho chote, ni utaratibu wa serikali yetu.

How comes hali hiyo iwaathiri wapinzani tu na cheki ya CCM iwe tayari kwa wakati?
 
CCM 1.2billion
CHADEMA 233million
CUF 98million

Hata hivyo utaratibu wa kutoa hizi hela ofisi ya Msajili inahusika kwa sehemu ndogo sana kwa kuandika Voucher kwenda hazina ambapo hazina inahamishia fedha hizo kwenye account za vyama kwa njia ya kielectroniki wala hakuna utaratibu wa Cheque kama mtoa habari alivyosema. Pia ile Voucher huwezi kuandika chama kimoja na kuacha vyama vingine kwa SABABU YOYOTE ILE.
Pengine ingeelezwa kuwa serikali haina fedha kwa sasa ningeelewa kwakuwa ni ukweli kuwa vyama vyote havijapata ruzuku hadi jana.

Malya: Maelezo yako yanaelimisha endelea na smimamo huo daima. Thank you very much and a very big up!!!
 
aaah! kumbe hela mnapata sasa mbona mnatuchangisha na sisi wananchi wakat hatujui hzo mnazopata mnazifanyia nini...wizi mtupu

wewe umetumwa kunaambaye amekulazimisha kuchangia oparation za chadema. sisi tunawaamini viongozi na pesa tunayochangia tunaona ikifanya kazi acha majungu.
 
Hayo ndiyo madhara ya jeuli maskini. Alijua tu mtaenda kupiga magoti kwake. Si nilisikia hamtashirikiana na Tendwa au hana sehemu ya kusaini au mlijisemea tu bila kujua maana halisi ya msemo wenyewe. Poleni si muanzishe omba omba nyingine kabla hawajaamka watawapeni. Nashindwa kuelewa hiki chama kikishika dola omba omba yao si ndo itazidi? Tukana lakini ukweli upo, je ulishawahi kuambiwa hata makusanyo yaliyopatika kwa uhamasisho wa Jr ni kiasi gani?

USIMWAMSHI ALIYE LALA!

Unatakiwa kuongea kama mwenye akili timamu ile ni ofisi na kinachotakiwa kufuatwa ni taratibu na sheria.na kumbuka siku zenu zinahesabika na nchi itakombolewa kutoka kwenye utawala wenu kwani mlinzi wenu shehk yahaya hayupo tena
 
Back
Top Bottom