Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,084
Wadau,
Katika kile kinachoonekana kuwa ni kudhibiti vya vya upinzani hususani CHADEMA, msajili wa vyama ameamua kukalia cheki za vyama hivyo na kutoa cheki ya CCM.
Huku vyama vingine vikiendelea kukalia kuti kavu, kwasasa bwana Tendwa ameamua kuonyesha U-CCM wake moja kwa moja baada ya kuelezwa kuwa hela wanayoipatia CHADEMA (ambayo ni halali kuipata) ndiyo inayoimaliza CCM kwa CHADEMA kujijenga zaidi.
Hivyo basi, wakaamua kukalia ruzuku za vyama vingine kwa kisingizio kuwa CHADEMA wakilalamika wataambiwa mbona hata CUF wala NCCR hawajachukua? Ila ukweli ni kwamba lengo ni CHADEMA na vyama hivi vingine vinaelewa mchezo mzima baada ya mbinu ya CCM ya kuitumia CUF kufa kabla ya utekelezaji.
Tuko hapa ofisini huyu msajili anakera sijui Demokrasia anayoisimamia ni ipi? Ofisi nzima tumeduwaa kwakuwa tumeona hizo cheki na CCM kupewa yao ila wengine hususani CHADEMA hakuna!
UPDATE:
Baada ya Habari hii kuingia humu JF Leo Tarehe 06/10/2012. Ninavyoandika hapa, tumeitishwa kikao cha dharura, aliyeitisha anasema sababu ya kikao hicho ni kutotunza siri za ofisi na kuanza kuliki kwenye mitandao ya kijamii, kwa yeyote anayetaka kujakujua ukweli aje aone kama atapata huduma.
Ila ninachosikitika kuna watu humu ofisini wameazwa kuhisiwa kutoa taarifa kumbe siyo wao.Nitawajuza nini kiliendelea baada ya kikao.