Tanzania, unaugua ugonjwa gani?

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Nov 18, 2011
339
578
Ndugu Watanzania,
Nadhani ni kweli tunapaswa tupimwe akili zetu. Inakuwaje nchi inajenga ushabiki wa kisiasa kiasi hiki, na kushindwa kuutazama uadilifu na historia ya watu wanaoomba kuongoza nchi? Haiwezekani kila anayefanya ufyongo na kujiuzulu au kutimuliwa nafasi walizokuwa nazo, anaibuka na kutuomba kumpigia kura ya kuwa Rais. Hii ni dharau kiasi gani?

Lowassa ana kashfa kubwa sana na alijuzulu kwa kashfa hizo. Huyu katangaza nia na mashabiki wake wamejitokeza kwelikweli.
Muhongo naye hivyohivyo leo amefanya hivyo. Na tumeshaambiwa watu kama akina Rostam Azizi, Tibaijuka, Karamagi na wengine wengi wenye tuhuma lukuki wamo nyuma ya wagombea hawa na watu wanawapigia makofi.

Tanzania tunaugua ugonjwa gani? Kwanini tumeruhusu kudharaulika kiasi hicho?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom