Tanzania tuitakayo! Oh my God!

Watoto kama huyu ni wakutandikwa bakora za kutosha wazazi wamenunua sare za shule wao wanaenda kuchezea kwenye mavumbi sisi wenyewe wazazi tumesoma shule hizo hizo lakini tulikuwa haturudi nyumbani tuko kama vinyago!

-Nyerere-
Tembea ujionee...! Maeneo mengine Tanzania hii hii maji ni majanga, kufua nguo ni anasa. Usimlaumu huyo mtoto, jilaumu mwenyewe kwa kutokuijua nchi yako.
 
kwa kile kingereza chako usingeeleweka ili upate cheo andika kiswahili au kinyumbani

Ungekuwa unakijua kingereza ungenisahihisha kama afanyavyo FAIZA FOXY kwa kiswahili hapo ungeonesha umahili wako kuliko kulalama tu!! Hebu sahihisha pale nilipokosea!
 
Hii ndio nchi yangu ninayojivunia! Tumeijenga kwa miaka 55 sasa na haya ni sehemu ya mafanikio yetu.
 
Ungekuwa unakijua kingereza ungenisahihisha kama afanyavyo FAIZA FOXY kwa kiswahili hapo ungeonesha umahili wako kuliko kulalama tu!! Hebu sahihisha pale nilipokosea!
kingereza kinamsumbua sana mkuu wako ndiyomaana nimekushauri utumie kiswahili.

NB:
Umahili - Umahiri
 
Imagine huyo mwalimu yukoje kwanza kama huyo ndio mwanafunzi
Nadhani wanasomea nje tu hawana madarasa maana hilo vumbi Shati kaptula vifungo hazina so sad Mungu ndie anaejua kwa kweliiii viatu Hakuna maji safi hakuna huduma ya afya ndo ivo tena Bado hali ni ngumu sana
 
Kuna wakati huwa najiuliza, je sare za shule zina umuhimu gani kwenye elimu? Ukivaa mavazi tofauti itaathiri uelewa wa darasani?

Uniform..uniformity...alike. Are we all alike? Sometimes I think uniforms are a conditioning technique; to reign in diversity...(just thinking out loud)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom