Tanzania ni taifa kubwa katika A.Mashariki. Cha kushangaza ni kwamba hatuna ONE OFFICIAL language. Tunatumia Kiswahili mitaani, kwenye mikutano,nk. lakini tunafundishwa Kiingereza mashuleni na text books zote ni za Kiingereza. Sasa kwanini tusifundishwe au tutumie lugha moja tu? ikiwa Kiswahili au Kiingereza. Kuna ushahidi unaonyesha kwamba: Wanafunzi wengi wanafeli kwa sababu hawaelewi vizuri Kiingereza. Hii yote inasababishwa na mchanganyiko wa lugha. Chukulia mfano mwanafunzi wa High School kutoka Uingereza anayetumia Kiingereza afundishwe Kiswahili ktk masomo yake. Je atapasi vizuri?
Nchi nyingi zilizoendelea zinatumia lugha moja tu kama Uingereza, Marekani, Iran, China, Italy, France, Russia, Israel nk. Kwa mfano Nyerere alitaka Kiswahili kiwe lugha ya Taifa na kitumiwe kwenye text book ktk Universities. Kuna umuhimu mkubwa kwa TZ kutumia lugha moja mashuleni, iwe Kiswahili au Kiingereza.