MD25
JF-Expert Member
- Jan 28, 2012
- 3,074
- 1,018
Habari wana Bodi
Tunapozungumzia tatizo la ajira kwa vijana, sio tu wale ambao hawana kazi kabisa, ila inajumuisha mpaka wale ambao wapo kwenye ajira, lakini wanapata ubaguzi au manyanyaso flani flani, bila kuwa na njia ya kujikwamua.
Ni muda mrefu sasa, hili swala limekua likijadiliwa na kuendelea kujadiliwa bila kupata ufumbuzi, hadi imefika paala, sisi vijana ambao tuko kwenye hili tatizo tunaonekana kama bomu linalotaka kulipuka (tunafananishwa na bomu).
Kwa hapa tulipofikia, Serikali hii ina-ajiri kwa kiwango kidogo sana na kupelekea vijana wengi kutegemea ajira kwenye sekta binafsi (kuajiriwa au kujiari)
Kwe upande wa ajira za kuajiriwa kwenye sekta binafsi, kwa sasa, WA-INDI ndio wamekua wakipewa kipaumbele kana kwamba wao ni waTanzania huku mTanzania mimi na wewe tukiachwa. Makampuni makubwa yamekua yakiajiri waIndi na kuwalipa mishaara minono kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na waTanzania wenye elimu hiyo.
Tukija kwenye hizi biashara ndogo ndogo, WACHINA ndio wamejazana huko. Hizi biashara ndogo ndogo zilitakiwa ziachwe zifanywe na wazawa, ili kuweza kukuza, middle income. Kusingekua na mafuliko ya hawa wachina, leo hii vijana wengi wangekuwa wanamoyo wa kuingia mtaani na kujiajiri au kwa wale walioajiliwa, kutumia akiba yao kidogo kufungua hizi biashara ndogo ndogo. Kwa kufanya hivi kungesaidia kwa kiasi fulani tatizo hili
Sio kwamba Serikali haioni au haijui haya matatizo, wanaona na wanajua, ila wameamua kutuacha ili KUTUKOMESHA. Imefika wakati sasa, ingawa upo nchini mwako, unakuwa kama mtumwa vile na hii ni kwa sababu ya hii serikali kuwathamini hawa waHindi na wachina.
HITIMISHO
Vijana, umefika wakati inatupasa tutambue sasa hivi sisi ni kama watoto yatima, inatupasa tutambue kwa hali ilipofikia hata ukiwa na Masters utaishia kuwa-frustrated, na hii ni kutokana na mfumo uliopo. Tutambue kuwa serikali hii haina tena msaada na sisi, kwani kama wangekua wanafanya juhudi za kutatua hili tatozo, tokea 2010 hadi leo 2013, angalau dalili za unafuu tungeanza kuziona. Tutambue kuwa hawa watu hawana huruma nasi.
Vijana, inatupasa tujifunze kutoka hata kwa nchi jirani ya Kenya, walivyo wakali kuhusu ajira zao za ndani, hawataki maskhara kabisa.
Vijana, inatupasa tuwe na kauli moja kuwa hii serikali sasa inatosha, wanatakiwa watoke madaraki (IWE KWA HIARI AU KWA NGUVU YA UMMA), ili kupisha serikali nyingine ambayo itakuwa sikivu na kuweza kuona hili tatizo la vijana kuwa sio bomu. Lakini tukiendelea kulalamika, haitatusaidia na tutaendelea kuumia tu