Mbunge wa ilula
JF-Expert Member
- Jun 3, 2012
- 211
- 18
Leo hii nimetangaza kazi ya bartender aliyemaliza form six na mpaka sasa nimepigiwa simu na watu kumi graduates,inatisha
...kula Vyakula vya mama ntilie mfulizo kunapunguza sana akili...angalia hili nalo!Mashavu yako unataka kutugeuza sample ya research yako eeh? Vilaza mnatusumbua sana.
Matatizo ya ajira yanaweza kuisha au kupungua iwapo sekta binafsi zitawezeshwa kukua na kupanuka zaidi. Sasahivi zinashindwa kukua kwa sababu kodi kibao, umeme wenyewe ndo huo tena mtu anazalishaje?
Tunategemea zaidi ajira chache za serikali ambazo zinataka darasa. Kila mkoa ungekuwa na viwanda na maduka makubwa 5-10 nina hakika ungekuwa unauliza kwanini Dar es Salaam ina watu wachache?
Tatizo liko sehemu zote, kinachowaumiza vijana ni kuwa na matarajio makubwa baada ya kumaliza msomo yao. Mtu akimaliza bachelor anawaza kupata kuanzia laki saba huyo ukimuambia nitakulipa laki 3 hakuelewi hata kama hana kazi anahisi anaidharirisha degree yake wakati hata uzoefu hana.
Serikali haina mipango endelevu ya kuweka mazingira ya kuwaajiri hawa inao wasomesha bado haijafikiria mikopo watarudishaje kama hawana kazi mitaala yenyewe hawawajengei wanafunzi hawa kuwa na elimu ya ujasiliamali kiasi kwamba kinageuka kitendawili.
Leo unapomwambia ajiajiri wakati hata hajui anaanzaje.
kwanza we maoni yako ni yapi? unahisi tatizo liko wapi?
sikia bro. ukisoma kila tangazo la kazi, wanahitaji experience ya miaka.3+ hafu mimi sina ata ya week moja, je ilo ni.kosa langu?
na hizo kazi wanazowekana watoto wa mjomba na shangazi yake mpwa wake je? nazo ni.kwasababu sikuandika cv nzuri?
yatasemwa mengi sana, lakini tatizo ni viongozi wa juu hadi wa chini katika sector husika. hii issue ni kubwa, kuizungumzia unahitaji counter book la 4 quire ili ukamilishe abstract tu.
smtym vijana tunachagua kazi,wakati mwingine inabidi ukubali to start small