Hii ndio solution ya hili tatizo

Jan 13, 2023
92
99
Tatizo ni nini?

Sasa hivi kumekuwa na hofu kwa baadhi ya watu wanaokula samaki Sato na Sangara kutoka ziwa Victoria baada ya riport kuwa wakazi wengi wa kanda ya ziwa wanapata kansa na hili sio tu Tanzania imegundulika hata kwa upande wa wenzetu Uganda na Kenya kwenye jamii zinazozunguka Ziwa Victoria kuna idadi kubwa zaidi ya waathirika wa saratani kuliko maeneo mengine.

Hili inatupa ushahidi ya kuwa cases za saratani kuwa nyingi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja na Ziwa Victoria.

Kumekuwa na nadharia ya kuwa chanzo cha kansa ni kutokana na kula samaki walioathirika na chemicals (chloroform & Formalin) zinazotokana na matumizi ya maji ya kuoshea maiti yenye dawa ya chloroform, yanayodaiwa kuwa yanatumika kuhifadhi samaki wasiharibike.

Sababu nyingine inayotajwa ni kuwa ziwa Victoria limezungukwa na mikoa yenye viwanda na migodi mingi na uchafu kutoka viwandani na migodini utililisha maji yake kwenye mito na hiyo mito yote kutoka maeneo hayo upeleka maji yake ziwa victoria. Lakini pia kuna wakati walikuta maji ya mto Mara yamebadilika rangi na samaki wanakufa. Wananchi wakilalamika kuwa uenda inasababishwa na utililishwaji wa maji machavu mto Mara kutoka migodini yenye kemikali ambazo ni sumu kwa samaki (zebaki) ila uchunguzi wa serikali ukasema si kweli.

Ni wazi kabisa maji ya ziwa yanakuwa contaminated sana na pesticides residues na uchafu mwingine mwingi tu hali inayofanya samaki kutoka ziwa Victoria kuonekana sio salama kwa watumiaji.

Wasiwasi uzidi kuongezeka na kufanya baadhi ya watu kuacha au kupunguza kula samaki wanaotoka Ziwa Victoria Lakini kiuharisi ni vigumu sana kuepuka kula samaki hususani Sato, kwa sababu ndio samaki pendwa na kiafya pia ni muhimu, samaki wanakiwango kikubwa sana cha protein, wanavirutubisho muhimu kama vile Vitamin B, madini chuma, magnesium, phosphorus, Omega 3 fatty acids na calcium. Kwa ufupi matumizi ya samaki kama kitoweo ni muhimu kwa watu wote hasa wenye matatizo ya shinikizo la damu, kisukari na kwa watoto inasaidia kuongeza IQ kwa watoto na faida zingine kedekede.

Nini kifanyike?


Miongoni mwa njia inayoweza kukufanya wewe na familia yako kuendelea kula samaki bila kuiweka afya yako na jamii yako salama ni kufuga au kuzalisha samaki wako mwenyewe au kununu Samaki kutoka chanzo cha uhakika. Samaki wa kufugwa ni salama kwa afya ya mlaji kwa sababu wanafugwa kwenye closed system, hii inafanya iwe rahisi kudhibiti uchafuzi wa maji na mfugaji anakuwa na full control kuanzia maji anayotumia hadi chakula wanachokula samaki anaofuga. Hii inatoa assurance ya usalama wa kiafya kwa mtumiaji wa mwisho atakula samaki salama wakiwa na ubora na radha ile ile kama wale waliotoka kwenye vyanzo vya asili na kupata nutrients zote muhimu anazotakiwa kupata.

Hii ni fursa kwa watu kuwekeza na kufanya ufugaji wa samaki kibiashara kwa ukubwa kwa maana mahitaji ya samaki ni makubwa kuliko samaki wanaozalishwa. Pia ni vizuri kuanzisha utamaduni wa kufuga samaki kwa ajili ya kitoeo kama unavyofuga kuku, ngombe, mbuzi n.k. Sio vibaya ukaanza utamaduni wa kufuga na samaki.

Mbali ya kuwa utapata kitoweo lakini pia ufugaji wa samaki ni njia moja wapo ya kutunza mazingira na kujiburudisha maana kuwaona tu pilika pilika za samaki ni burudani tosha itakayo kupunguzia msongo wa mawazo na kupata relaxation. Vitu vya muhimu unavyotakiwa kuwanavyo kama unataka kuanza kufuga samaki ni kuwa na maji, eneo na hela kidogo (chakula & operationsl cost) za kuwahudumia samaki.

Mimi nitakuwa mstari wa mbele kuiweka salama jamii ya watanzania (walaji wa samaki) kwa kuhamasisha juu ya ufugaji wa samaki kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, wafanya biashara, taasisi hadi taifa, kwa kuhamasisha uanzishwaji wa miradi midogo na mikubwa. Reasources muhimu kama maji na maeneo yanayofaa kwa ufugaji wa samaki yapo ya kutosha wajibu ni wetu kuyatumia vizuri resources zetu kwa kuanza utamaduni huu wa kufuga samaki.

Niko hapa kama mtaalamu wa ufugaji samaki sio tu kutoa hamasa, natoa pia ushauli wa kitaalam na muongozo wa njia bora ya kufanya ufugaji wa samaki kisasa kuanzia kuandaaji wa sehemu ya kufugia samaki (bwawa, tanki au kizimba), jinsi ya kupata mbegu nzuri, jinsi ya kutengeneza chakula na kulisha samaki hadi jinsi ya kufanya management. Pia nasimamia na kuboresha miradi ya ufugaji samaki kwawale ambao tayari wameshaanza.

Uweza kunicheck tukaongea directly au What’App: +255758779170
 

Attachments

  • 845330618_2_644x461_fish-farm-consultant-and-sales-of-fish-product-upload-photos.jpg
    845330618_2_644x461_fish-farm-consultant-and-sales-of-fish-product-upload-photos.jpg
    19.2 KB · Views: 2
  • pexels-alexey-demidov-12349154 (1).jpg
    3.5 MB · Views: 1
  • pexels-pixabay-371669.jpg
    2.9 MB · Views: 1
  • pexels-ömer-derinyar-18676349.jpg
    pexels-ömer-derinyar-18676349.jpg
    1.9 MB · Views: 2
  • pexels-petr-ganaj-17914573.jpg
    pexels-petr-ganaj-17914573.jpg
    759.3 KB · Views: 3
  • pexels-alexey-demidov-12349154.jpg
    3.5 MB · Views: 2
  • pexels-alexey-demidov-10813727.jpg
    pexels-alexey-demidov-10813727.jpg
    2.3 MB · Views: 3
  • pexels-jonathan-cooper-12708906.jpg
    pexels-jonathan-cooper-12708906.jpg
    990.9 KB · Views: 2
  • pexels-tom-fisk-1103812.jpg
    pexels-tom-fisk-1103812.jpg
    1.5 MB · Views: 2
  • pexels-jimmy-ramírez-10436681 (1).jpg
    1.5 MB · Views: 1
Summary:
Tatizo ni nini?
1. Kumekuwa na nadharia ya kuwa chanzo cha kansa ni kutokana na kula samaki walioathirika na chemicals (chloroform & Formalin) zinazotokana na matumizi ya maji ya kuoshea maiti yenye dawa ya chloroform, yanayodaiwa kuwa yanatumika kuhifadhi samaki wasiharibike.

2. Sababu nyingine inayotajwa ni kuwa ziwa Victoria limezungukwa na mikoa yenye viwanda na migodi mingi na uchafu kutoka viwandani na migodini kutiririsha maji yake kwenye mito na hiyo mito yote kutoka maeneo hayo upeleka maji yake ziwa victoria.... na utiririshwaji wa maji machafu mto Mara kutoka migodini yenye kemikali ambazo ni sumu kwa samaki (zebaki) ila uchunguzi wa serikali ukasema si kweli.

3. Ni wazi kabisa maji ya ziwa yanakuwa contaminated sana na pesticides residues na uchafu mwingine mwingi tu hali inayofanya samaki kutoka ziwa Victoria kuonekana sio salama kwa watumiaji.
 
Back
Top Bottom