Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,057
Tunayahitaji sana maendeleo lakini si u dictator wa kupotezana na wasiojulikana.Na ni kwasababu weshatujua kuwa sisi wenyewe hatuzipendi nchi zetu na hatuna muelekeo wowote wakutaka kujitawala kifikra na nyanja zote Kama mataifa huru.(mind Colonization).
Trump aliwahi kusema kuwa Africa haitakiwi kujitawala inabidi itawaliwe tena.
Hii kauli tuliichukulia simple bila kuijaji mara mbili mbili kwanini aseme hivi, na huko kututawala tena watatutawala kwa njia gani?? Kama unadhani alimaanisha watakuja tena kututawala Kama mwanzo basi utakuwa umepotea, tumejusahau tunadhani new colonial project imekwisha.??
Kila siku tumekuwa the home of new ideas kutoka nje ambazo hatuhusishi kuzijadili Kama zina faida kwetu ama lah, lakini tunalazimishwa kuzikubali tu. Viongozi wetu wanalazimishwa tu kuzikubali na wachache wanao kataa ndio hawa wanao itwa kila jina baya.
Prof Lumumba aliwahi kusema "Kuna njia tatu za kuwa kwenye dinner table, unaweza kuwepo Kama mhudumu, dinner or food to be eaten, now Africa has been at the dinner table as food for too long."
Hatuwezi kuupinga huu ukweli, vingozi wetu walio wangi wanapokuwa kwenye mikutano ya kimataifa kwenye mambo ya maana yanapojadiliwa vingozi wetu wengi wanaenda tu kwa kupiga picha tu. Wachache wanao jaribu kuwa serious na nchi zao ndio hao wanaoitwa madikteta na sisi wenyewe tulivo wajinga tunawaunga mkono maadui zetu kwa sababu zisizo na tija yoyote.
Sent using Jamii Forums mobile app