Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
Nimepitia Thread hii;

Nimegundua yafuatayo:-
1. Bado kuna namba kubwa sana ya wachangiaji hawafahamu nini maana ya utawala bora!

2. Kuna Wachangiaji wako shalow sana, kwamba hawezi hata kuchambua mambo ingawa uhuru walio nao unawafanya nao waonekane wachangiaji makini.

3.Kuna namba kubwa sana ya watu ambao hata hawajasikiliza hotuba ya Rais hivyo wengine wanamwaga maneno tu bila kujua kilichoongelewa nini, Namshukuru Mungu nimemsikiliza Rais mwanzo hadi mwisho. Najua ana weakness zake kama binadamu. Lakini changamoto aliyonayo Rais yetu ni kwamba wananchi wetu hawafahamu kwa nini Rais hataikiwi kumfukuza Kasheshe pale kwenye halimashauri yake.

4. Wale wanaofuatilia siasa za Tanzania... wanakumbuka polisi aliyefukuzwa na waziri mkuu.... etc.

Kumbe watu wengi tunamlaumu Mh. Rais wakati sisi wenyewe ni watu ambao tuko shallow sana.

Kasheshe,
Madhali wewe umeisikiliza hotuba nzima ya rais naomba utupe summary ukizingatia vigezo ulivyovitaja kama vile utawala bora ili tuache kuwa shallow na tuongeze uwezo wetu wa kuchambua. Asante!
 
Kwa kweli kama rais hatuna jamani. Rais gani anaogopa watu, na yeye ndo mwenye rungu. Tena ameudhi sana kumsifia Fisadi Lowassa, mwisho anasema eti wahusika watachukua hatua, yeye anaogopa nini.

Kwa kweli anatakiwa ajiuzuru kama Musharaf wa Pakistani. nawasilisha hoja wana JF
 
Hii hotuba iliyojaa pumba iwekwe hapa wakuu kama kuna mtu ameshaipata. Naunga mkono wananchi walioleta wazo la kufanyika kwa maandamano ya amani, nadhani hii ndiyo njia pekee kwa sasa ya kuonyesha namna tunavyokerwa na uongozi wa awamu ya nne.

Nampongeza sana Mhe. Sitta kwa maneno yake mafupi lakini mazito yaliyobeba kiu ya Watanzania. Maneno hayo kama Kikwete atayatafakari atatambua kwamba ameongea pumba kabisa na iwe aibu kwake. Shame upon you Mr. President, shame upon your government, you treat Bunge as kijiwe, shame upon you. Watanzania, lazima tufanye jitihada za kujikomboa kutoka mikononi mwa mafisadi pamoja na chama chao.

Badly we are not luck because wapinzani hawana nguvu za kisiasa, upinzani uliopo ni dhaifu mno, hata tusitegemee kwamba utaiangusha CCM, otherwise mageuzi makubwa yaffanyike ndani ya upinzani. Ni nguvu za wananchi tu ndo zitatukomboa bila kujali itikadi za kisiasa.
 
Hivi hapa bado kuna watu wataendelea kusema walaumiwe wasaidizi wa rais? Alaumiwe yule aliyeiandika hotuba ama hotuba iliyoandikwa ndiyo ile rais aliyotaka kutoa?
 
Hivi hapa bado kuna watu wataendelea kusema walaumiwe wasaidizi wa rais? Alaumiwe yule aliyeiandika hotuba ama hotuba iliyoandikwa ndiyo ile rais aliyotaka kutoa?



JK kaona PR inakuwa na hali mbaya wakati Mukandara kasema CCM iko hoi kwa 40% sasa akaona akimbie aje kuzima maandamano ya waalimu .Yeye alitaka kukemea maandamano tu na kupinda kutolea maelezo ya EPA kwa neno la kurudisha pesa .Nangoja Kasheshe aje na uchambuzi makini tuone
 
Naona aliofanya Rais ni u´fisadi mkubwa kuliko uliowahi kufanywa na awaye yote:

1. Wezi amewageuza kuwa wakopaji halali na watarejesha mkopo bila riba

2. Amelihadaa taifa kwa kuchukua maamuzi mbali mbali ya kuwalinda wezi wakati wananchi wanaoiba kuku wakiuwawa kwa kuchomwa moto au kufungwa miaka 15 kwa wizi wa mifugo.

3. Amejivua madaraka ya kuwa kiongozi mkuu wa serikali mwenye miliki ya wafanyakazi wote walioko chini ya serikali kuu. Leo wakuu wa mikoa, mawaziri, wakurugenzi mbalimbali, wakuu wa wilaya wanateuliwa na rais nao wanamwakilisha rais katika sehemu zao za kazi.

Rais kusema kuwa anahitaji KUWAOMBA ETI WAWAJIBISHE wahujumu ni KUWAFISADI Watanzania kwa kiwango kisichovumilika.

Kwa maana hiyo UKWELI NI UFISADI WOTE ULIOFANYIKA ULIKUWA NA MASLAHI MWAKUBWA KWAKE NA HAWEZI KUMFUNGA KENGELE YEYOTE.

HII NI AIBU NA FEDHEHA KWA WATANZANIA NA KWA BAADHA YA WABUNGE WALIO MAKINI NA WENYE KUIPENDA TANZANIA
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 118 (34 members and 84 guests)

Mwenye hotuba hii atuwekee tusome mchezo huu wa kuigiza.......Kikwete najua unasoma Jf sasa hivi....
 
Hivi , Raisi wetu hana Marafiki wa kumshauri? au ndio wanafiki wenyewe? Basi namuomba angalau mwanae/binti yake moja amwambie ukweli Baba upo UCHI.

Maana hii hotuba kweli inaonyesha Tz hatuna Kiongozi bali picha ya Kiongozi. Nakumbuka kuna mchangiaji mmmoja alisema nchi ipo kwenye auto pilot, inajiendesha yenyewe.

Na ni aibu kwa CCM, na Watu mahiri walio CCM na kuona Nchi ina pwelea pwelea
 
Mzee Mwanakijiji,

Soma vizuri katiba na sheria... na sisitiza na sheria... Rais hawezi fukuza mfanyakazi wa TBC, TSN, BOT, TRA, etc. etc. hawateui yeye na wala sio muajiri...

Hapa kuna tatizo... ya mawazo ya miaka ya 40... ya taka ku-be applied kipindi hiki...

Baada ya muda mutaelewa... kwa sasa bado... I regret to learn... kwamba tatizo ni wananchi na wala sio Rais.

Kasheshe sio kwamba watu wanataka Raisi awafukuze etc, wanacho taka ni kuchukuliwa kwa hatu za kisheria kuelekea huko kwenye kuadhibu au kufukuza.

Eg kuna criminal issues ambazo mpaka sasa hazijachukuliwa hatua, sasa hapo tuseme nini? na report za mkaguzi zilisha sema.

pili wahusika hajatajwa hadharani, hata kama wana tuhumiwa tu.

Nakumbuka JK halisi alisema "..... wewe ni mke wa mfalme hutakiwi hata kutuhumiwa kwamba ume zini" alipo kuwa akimsema EL na tuhuma za Rushwa na Kujilimbikizia Mali.
 
Mzee Mwanakijiji,

Soma vizuri katiba na sheria... na sisitiza na sheria... Rais hawezi fukuza mfanyakazi wa TBC, TSN, BOT, TRA, etc. etc. hawateui yeye na wala sio muajiri...

Hapa kuna tatizo... ya mawazo ya miaka ya 40... ya taka ku-be applied kipindi hiki...

Baada ya muda mutaelewa... kwa sasa bado... I regret to learn... kwamba tatizo ni wananchi na wala sio Rais.

Kasheshe,

Nielewavyo mimi ni kuwa Raisi ndiye mwamuzi wa mwisho kabisa katika nafasi zote za uongozi za kuteuliwa iwe serikalini au kwenye mashirika ya umma. Maamuzi yote ya kuteua au kusitisha uteuzi yanafanywa hivyo kwa niaba au ruhusa ya Raisi. The buck stops with the President, period.

Hii hali inaongezwewa nguvu zaidi nchini Tanzania kwa sababu Raisi pia ndiye mwenyekiti wa chama tawala. Kushindwa kwa Raisi wetu kufanya maamuzi mazito kunasababishwa na mambo matatu;

1. Uwezo mdogo na kukosa nia
2. Uwoga na kulinda maslahi
3. Uongozi uliojaa ubabaishaji

Hata akivikwa joho gani, hata wakilaumiwa wasaidizi na hata akitoa hotuba ngapi - ukweli unabaki pale pale - kwa JMK tumetoka kapa.
 
We Kasheshe umetumwa nini?

Hivi ni nani anawateua wakurungenzi wa hayo makampuni uliyoyataja (TBC, TSN, BOT, TRA ect.? Au unataka kusema wakurungenzi wa hayo makapuni si wafanyakazi?
Soma between lines...

Nimesema wafanyakazi ndani ya makampuni... sijasema wakurugenzi aliowachagua yeye!

Mitizamo yenu ni ya miaka 40... kwa hilo la mitizamo ya miaka ya 40... mko sawa sana... na kwa kweli sawa sana...

Lakini kwa mitizamo ya sasa ya kujenga mifumo... you are very wrong and wrong indeed.
 
JK alichofanya leo hakina maelezo, ni kabaki jina Rais ya wabongolala (anvyodhani).

Mimi naamini au niseme nafikiria kuwa kwa vile Mungu anatupenda basi katuonyesha au katupa ishara nzuri sana leo. Uamuzi uko kwetu wananchi na sio tena wenye nchi.

Kumbukeni ya Urusi enzi za Yeltsin ilizaa tunda la Putin na tuangalie Urusi leo wako wapi.

Kwa kifupi Jk ameua CCM kazi iliyobaki sasa ni wananchi kushirikiana na vyama pinzani kurudisha nchi yetu nchi kavu.
 
Soma between lines...

Nimesema wafanyakazi ndani ya makampuni... sijasema wakurugenzi aliowachagua yeye!

Mitizamo yenu ni ya miaka 40... kwa hilo la mitizamo ya miaka ya 40... mko sawa sana... na kwa kweli sawa sana...

Lakini kwa mitizamo ya sasa ya kujenga mifumo... you are very wrong and wrong indeed.

Kasheshe niliposema wanaoserve at the pleasure of the President ana uwezo wa kuwafukuza at will...
 
Ni watu wanaofikiria huru kama mimi ndio wanaoweza kuchambua kwa haki... sio wale ambao mkate wao wanapatia kutoka CCM, au wale ambao wanategemea panapo 2010 na wao... wapate fedha za walipa kodi....

Kuna mambo ya msingi kabisa JK ambayo ameongelea... Nitataja machache!

1. Mchakato wa Sheria ya Uchaguzi (Election Financing) ndani ya vyama na wakati wa uchaguzi wa vyama... (hiyo mahafidhina hawajaona kwamba ni jambo jema)... by April 2009 sheria itakuwa imefikishwa bungeni.

2. Sheria ya kumpa au kuipa taasisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali Meno.

3. Kupitishwa kwa sheria mpya ya TAKUKURU.

4. Marekebisho ya Sheria ya EWURA.

5. Ukuaji wa Demokrasia na Uhuru wa maoni!

6. Fedha za EPA, kwenda kwenye TIB kuanzisha mtaji wa Kilimo, zingine kwenda kwenye ruzuku ya Mbolea na Dawa za Mifugo...

7. Chuo Kikuu cha Dodoma, Intake expected to 8,000 students, Kitila tukitoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam tulikuwa kama 5,000/-

8. Ukuaji wa Utalii - mapato kutoka $600mi.. kwenda $1200mil and USA kuongoza kwa watalii.

9. Umeme kwa wilaya zote nchini except Nkasi at least by now... but they are working on it.

10. Amezungumzia barabara kwa undani... mwenye akili timamu anaweza kujua hilo.

11. Issue ya Zanzibar whether ni nchi au sio nchi : done.

12. Issue ya Richmond... out of the scope... waziri Mkuu ndiye ataipeleka Bungeni specific, hivyo hakutakiwa kuizungumzia.

13. Muafaka ni sehemu ambayo bado wako nyuma.

14. Mambo ya inflation ameongelea kwa namna ambayo hata mimi nilikuwa sikuwa fahamu adhari zinginge ukitegemea mimi nimesomea mifugo.

15. Michezo... focus tunapeleka kwenye riadha.

16. Amedumisha utawala bora... waliosikiliza alisoma mapendekezo ya CAG. na hatua alizochukua ikiwa pamoja na kuunda tume ya Mwanyika...kurudishwa kwa fedha...

My take kwenye hili... huu ndio ulikuwa mchezo wetu waTanzania wengi wa Kuiba... dawa ilikuwa baada ya fedha zetu kurudishwa.. tuachane nao tuendelee na shughuli zingine we have other priorities... mifano hii imefanyika sehemu nyingi duniani kwa watu makini...

South Africa: Baada ya ubaguzi Mandela alivyochukua nchi... hakuwapeleka wazungu magereza aliunda tume ya maridhiano mambo yakaisha.
Kenya: Baada ya mauaji... wanachofanya sio kupelekana magereza.
Zambia: walifanya tofauti... wakatimuana kila wakati... b'se of nonsense decision za Chiluba.
 

..viongozi wote duniani waliofanikiwa HAWAKUWA WAOGA KUTOA UAMUZI.....sometimes delayed decisions cost our nation even more..kuliko mtu mzima rais wa nchi kutumia mgongo wa rule of law kama excuse ya maamuzi ya konokono....kwani kuna sheria gani inayosema MWIZI AKISHARUDISHA PESA ..ANAJEUKA HANA HATIA...SO rais kajeuka jaji.....

..mimi nadhani hata kitendo cha spika kuamua kumjibu pale pale,...ni kama kumpa ujumbe kwamba hawajaridhika..na kwa kweli SPIKA AMEONESHA UJASIRI.....maana mara nyingi ..alitegemea sifa...pia inadhihirisha KIKWETE NI RAIS DHAIFU KULIKO WOTE .....kiasi hata spika ameona dawa yake ni kumkosoa pale pale...kudoz six!!!!!

......usigeneralize..

..nimepitiapitia posts kadhaa, hii imejumuisha vizuri kilichojiri leo.

..tusubiri sherehe!
 
Back
Top Bottom