Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
mwenzenu... nimeamua kurudi kuandika hadithi zangu na visa vya kufikirika; sidhani kama mimi na Kikwete tunaishi sayari moja.

i have never been disappointed by our so called president like today. winding up of the speaker was better off
 
Na hapo ndipo utakaposhangaa sasa mwaka 2010 Kikwete anashinda tena kwa kishindo...........kweli ''mitanzania ndivyo tulivyo..''
 
Mkulo alitueleza during budget yake kuwa fedha za EPA sio za umma.
JMK kamalizia kwa kuwapa muda hawa wezi hadi 31 october, yaani serikali inawabembeleza wezi?

Sasa ameamua kuzihamishia hizo fedha serikalini ili wakazitafune vizuri, wakazipangie semina na makongamano meeeeengi yasiyo na tija.

Halafu cha KUZINGATIA ni kwamba ile kampuni ya swahiba wake, KAGODA iliyochotewa bilioni 40, uchunguzi wake wa ndani umekamilika lakini wa nje bado! wanasubiri msaada wa interpol!kama hawa interpol wameshindwa kumkamata JJ sembuse hawa EPAsiders?
 
This is beyong politics, tunahitaji kutafuta jina tofauti katika hili la utendaji wa mkuu kwani kama ni wakisiasa nadhani umepitiliza.

Katika mambo mengi ambayo tulitegemea ayazungumze kama Rais na Mwanasiasa hakuna hata moja quantifiable, ilikuwa kama kusiliza nyimbo za kila mwisho wa mwezi. Nadhani hii hotuba ageweza kuitolea DSM na kuacha siku ya leo kwa ajili ya maswali na majibu kwa PM
 
Mimi nafikiri akina MKJJ na wenzako ndiyo wenye matatizo kwa kuendelea kuwa na matumaini na huyu ndugu yetu. Sisi wengine ambao hatukuwa na matumaini yeyote na huyu bwana haitupi shida kabisa, na hivyo kwa kuwa sasa hivi nipo Dar naendelea kubugia tusker zangu tu.

In fact katika hii hotuba naona amekwenda beyond my expectation. I was expecting nothing, but he said something that did strike my nerve!

Tunachotakiwa sasa hivi ni kuomba Mungu aendelee kutupa bahati ili siku za utawala za CCM ziishe. Kwa sasa hivi nikiwasikiliza watanzania na wanasiasa wetu, both in the opposition and CCM, sioni matumaini yeyote zaidi ya kutegemea bahati na miujiza ya mwenyezi Mungu. Bahati mbaya tulio nayo ni kwamba bahati ya mwenyezi Mungu ni, unfortunately, very unreliable!!

Kwa kifupi madamu watanzania, hasa wasomi na waliosomasoma wanaendelea kuipenda na kuikumbatia CCM, kwa madai kwamba iliwasomesha na wametoka nayo mbali, nchi yetu imeliwa!

Kwa maneno mengine, na nikamnukuu jamaake Kasheshe, ni kwamba "tumenasa", tena tumenasa hasa!
 
Na nionavyo mwaka 2010 atashinda tena ingawa si kwa kura nyingi kama alivyo pata 1995. kweli JK nimsaani na nimeani huyu ndiyo mwanasiasa....hivi wale watu wa EPA wakirudisha pesa hawatashitakiwa!? mbona mimi si jamuelewa....
Hatawashtaki vipi na hela haikuwa ya serikali?hapo inabidi kuwashtaki wafanyakazi waliobunja taratibu za kiserikali,ata hivyo hayo makampuni ambayo yalisingiziwa yametoa ruhusa inabidi yapatikane ili kuthibitisha kuwa ni kweli jambo ambalo litakuwa ni gumu sana hasa ukizingatia yenyewe yalishafuta madeni hayo na hayana mpango na hio hela tena.
 
Hivi jamani mlitegemea Rais ambaye ni Incompetent kama Kikwete ataongea kitu chochote cha maana, huyu mtu uwezo wake ni mdogo sana katika maamuzi mbalimbali na hata kuchanganua mambo.

Tusitegemee jipya kutoka kwa Kikwete hata siku moja, tukubali tu tumelamba GARASA.
 
....., hasa wasomi na waliosomasoma wanaendelea kuipenda na kuikumbatia CCM, kwa madai kwamba iliwasomesha na wametoka nayo mbali, nchi yetu imeliwa! QUOTE]

KM

Ukiwa umesoma na ukashindwa kuelewa kiini cha matatizo ya mtanzania usomi wako ni sifuri.

Usomi gani unashindwa hata kusaidia kizazi chako cha pili kwa kuwawekea msingi mzuri wa maisha.

Eti nina digrii, msc, phd, call me prof, uwiiiiiiiiiiiiii
 
You made me laugh, I had to.
I believe this was not your intention - to make people laugh.





.
 
2010 naomba jamani wote tupigeni kura tusiache wapiga kura wachache watuharibie nchi....tuingie wote katika hii battle tuiokoe nchi yetu jamani..tunadharaulika hivi hivi..na tukidharauliwa tunakasirika.

Please Please Please!! tusibaki kulalamika tu..tutumieni nguvu tuliyonayo ambayo ni kubwa kuliko hii ya kupayuka kwa maandishi.....kura is everything ..kura is the only thing ambayo ita tu save watanzania na shida zote hizi za viongozi kama hawa........yaani leo nimetamani kutoa chozi!!
 
2010 naomba jamani wote tupigeni kura tusiache wapiga kura wachache watuharibie nchi....tuingie wote katika hii battle tuiokoe nchi yetu jamani..tunadharaulika hivi hivi..na tukidharauliwa tunakasirika...Please Please Please!! tusibaki kulalamika tu..tutumieni nguvu tuliyonayo ambayo ni kubwa kuliko hii ya kupayuka kwa maandishi.....kura is everything ..kura is the only thing ambayo ita tu save watanzania na shida zote hizi za viongozi kama hawa........yaani leo nimetamani kutoa chozi!!
sawasawa.... sasa tutazuiaje wizi wa kura?
 
jamani kuliko kuendelea kujadili hotuba mbovu ambayo hatuna uwezo wakubadili kitu hapo(yaani ndo imetoka) nadhani ingekuwa ni busara kuanza kupanga mikakati ya kura za kumng'oa yeye na kumpata kiongozi bora

hasa ukizingatia hawa watu ni wezi wa kura
 
hii kauli kaitoa the so called president kuhusu gharama za tz kutangaza utalii CNN!! 700,000UDS zimetumika
 
JK kweli amenisikitisha. JK Kama alithubutu ku freeze Account ya Kighoma A Malima ya offshore kabla ya uchaguzi mwaka 1995 akiwa waziri wa fedha inakuwaje mafisadi wanamshinda akiwa rais?, au anataka amwachie rais wa awamu ya Tano aje kuwashitaki mafisadi wa EPA na kina Chenge, Mkapa,...,
 
Watch my signature lol!
Yaani we acha tuu!JK ndiye mwenyewe mwingine photocopy!
 
Kilichobaki sasa ni kudai UHURU kwa njia ya amani....Mh Rais ni MATEKA WA KISIASA...Haya....WANANCHI MUANDAMANE KWA AMANI....WE WANT FREEDOM...WE WANT IT NOW!
 
2010 naomba jamani wote tupigeni kura tusiache wapiga kura wachache watuharibie nchi....tuingie wote katika hii battle tuiokoe nchi yetu jamani..tunadharaulika hivi hivi..na tukidharauliwa tunakasirika.

Please Please Please!! tusibaki kulalamika tu..tutumieni nguvu tuliyonayo ambayo ni kubwa kuliko hii ya kupayuka kwa maandishi.....kura is everything ..kura is the only thing ambayo ita tu save watanzania na shida zote hizi za viongozi kama hawa........yaani leo nimetamani kutoa chozi!!

Tatizo asilimia kubwa ya watanzania imeridhika na hali ya umasikini na ufukara iliyopo nchini, Watanzania wengi wameridhika na jinsi nchi inavyoendeshwa kigoigoi, watanzania wengi wameridhika na uongozi wa kifisadi na kijambazi wa CCM.

Watanzania wengi ni waoga, wamezubaa, wamepumbaa na wasioona tatizo lolote kwenye uongozi wa nchi yetu. Asilimia yetu hapa JF tunaopiga makelelele ni ndogo sana kulinganisha na wengi wanaoona kila kitu kiko sawa.

Tuna safari ndefu, safari isiyo na matumaini, safari ya maumivu.
 
jamani kuliko kuendelea kujadili hotuba mbovu ambayo hatuna uwezo wakubadili kitu hapo(yaani ndo imetoka) nadhani ingekuwa ni busara kuanza kupanga mikakati ya kura za kumng'oa yeye na kumpata kiongozi bora

hasa ukizingatia hawa watu ni wezi wa kura

Now you are Talking....
 
Back
Top Bottom