Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
Sahihisho. si ALFA ni ALPHA na pia si mtoto wake ni kampuni yake na familia yake. Mtoto wake anayejitokeza kila mahali anaitwa Fred, sasa kama hiyo kampuni imepewa, hapo ndipo tunaanza kuona ni kwanini watu wanamtetea Mkapa, wanajua baada yake ni wao

Kama ni ALPHA na OMEGA vilevile kwa hiyo twisha....
 
Kweli kazi ipo,

kama jamaa ameweza kuchukua hiyo basi hakuna wa kumzuia maaana wengi walijaribu kwa madau makubwa na ya kutisha mno wakashindwa na JK alikuwa akiwakenulia macho mpaka wengine wakajikuta wanazurura katika korido za mambo ya nje.......na wengine kuwa mawaziri wa vijana kutoka wizara kubwakubwa....

Kaka Halisi hebu jaribu kutupa uhakika, Huyu jamaa ni fisi lakini sio reckless kiasi hiko....siamini kama hizi nyeti zina ukweli wowote....

Tanzanianjema
 
Duh! Hata matanga ya RICHMOND hatujaanua Lowasa tena anatuletea msiba mwingine?
 
Nataka kuogopa, kwa sababu, mwanzo wenyewe unatia shaka kwamba mtoto anaitwa ALFA, inaonekana kuna utata, kwa kweli tenda ya vitambulisho imekua na matatizo tokea enzi za ALI AMEIR akiwa Waziri wa MAmbo ya Ndani hadi kukawa na kesi mahakamani, lakini hatua ya pili nayo imezua utata mkubwa Idara ya Uhamiaji, maana zabuni imekua ina utata mkubwa sana.

Nina hakika ni vigumu sana kwa EL kuingia humo, na kina Kihomano watakua waoga sana kumhusisha, labda kwa mgongo wa nyuma si kwa ALPHA/ALFA
 
Jamani jamani, why kumpa mtu wa kati tender hali zipo kampuni ambazo zinatoa vitambulisho moja kwa moja?

Mimi nashindwa kabisa kuelewa huu mpango wa serikali kupitia kwa mtu kununua kitu chochote kile toka nje!..Tunahitaji majenerata ati tunauza tender! wakati tunafahamu GE ilipo na pia Tanesco ndiye mzalishaji na msambazaji umeme!. Uongozi wa Tanesco hawawezi kufanya kitu bila mkono wa mtu toka nje....why?

Hilo swala la viongozi kuwapa watoto wao nafasi za kufanya biashara, kusema kweli mimi sina tatizo nalo kabisa maadam watoto hawa hawatumii mali ya serikali kuendesha biashara zao.

Naunga mkono kabisa kiongozi yeyote anayejaribu kwa kila hali kuhakikisha mwanaye anapata elimu, kazi na hata nafasi kubwa ktk utumishi maadam anazo qualifications!..Labda utata unakuja tu pale napojaribu kufikiria hiki kimila cha kwetu ambacho kinampa kichwa mtoto wa mkubwa kutofuata sheria na ubinafsi kutangulia Utaifa. Lakini nje ya hapo nadhani vijana hawa wanastahili pia nafasi sawa ya mchango wao ktk uzalishaji...

Can they deliver?...that's a catch 22!
 
Ukweli ni kuwa ALPHA kama kweli imepewa hiyo tenda basi yeye atakuwa "Middle Man" kwa maana ataenda na kuitoa hiyo tenda kwa mtu au kampuni nyingine yenye uwezo.

Kama serikali ingeenda moja kwa moja basi milioni au bilini kadhaa zingeweza kunusurika.
 
Mkandara,

Ni vema nikusahihishe. Kuna conflict of interest kama mtoto wa Waziri Mkuu, au kampuni ya Waziri Mkuu, au kampuni ya mtoto wa Waziri Mkuu, ikipewa tenda na serikali.

Serikali haipashwi kuruhusiwa kumpa mkuu wake, au mtoto wa mkuu wake, au kampuni ya mkuu wake, au kampuni ya mtoto wa mkuu wake, tenda yoyote.

Augustine Moshi
 
Ndg Mpaka Kieleweke,

Tunaomba urudi hapa na utupe kwa undani habari kuhusu Mzee Lowassa na issue ya Utengenezaji Vitambulisho!.Ukweli wa habari hiyo una Utata,kwa sababu Mtoto mkubwa wa Lowassa anaitwa Fred na sio Alpha kama ilivyoripotiwa hapo awali.Lakini kuna Mtanzania kwa jina hilo (Alpha) ambaye anaishi Marekani,Jimbo la Minnesota alikuwa anafukuzia Tender hiyo.Jamaa huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya GWP Mortgage Service ana mahusiano ya mbali na Lowassa.

Inasemekana mke wake ana undugu na mama Rebecca.Kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita jamaa alikuwa anarudi Tanzania mara kwa mara kufukuzia kazi hiyo.Sasa kuna uwezekano kabisa kuwa huyo jamaa amepewa kazi hiyo kwa mlango wa nyuma!
 
Vitambulisho vya urai ni swala nyeti sana, na halianzi tu kwenye uwezo wa kutengeneza hivyo vikaratasi. Vikaratasi hivyo ni kama vile cheti unachopata baada ya kuhitimu shule. Kunamaswala ya msingi ambayo ni muhimu kwetu.

Kwanza, kampuni inayopewa tender, itatumia utaratibu upi kujua huyu ni mtanzania?

Pili, ni nani anayethibitisha urai wa mwananchi? Ni kampuni hiyo hiyo, kama hapana, taratibu za ushirikiano zikoje?

Tatu, uaminifu wa hii kampuni unapimwaje? Kwani watakuwa na habari nyeti za wananchi, ambazo zinaweza kutumika kwa masilahi binafisi.

Nne, Taratibu zipi zitatumika kutoa maombi ya kupatiwa vitambulisho hivyo? Tuwakumbuke watu wavijijini watashiriki vipi kwenye hili? Hii Kampuni itaenda mpaka huko ama?

Tano, gharama za kitambulisho ni zipi?

Sita, database ipi ijengwe kwa watoto wanaozaliwa sasa ili kuepusha ukosefu wa utuzwaji wa data wa kizazi chetu usijirudie?
 
By the way do we need these bloody IDs?
Ni kweli haielekei kama tunavihitaji.

Pamoja na umuhimu wa kuwatambua wageni, lakini inapofikia masuala ya kisiasa wananchi wamekuwa makini kuhakikisha wasio raia wanakaa kando.

Sasa iwapo tutaleta urai wa makaratasi na enzi yenyewe ya rushwa, basi tutawahalisha wageni kuingia hadi chumbani.
 
Heshima zenu wazee,

Aliyeianzisha hii thread anasema kuwa ni habari za kuaminika, lakini imekaa kama tetesi; kwanza jina la huyo mtoto wa Lowassa members wengine wameonyesha kuwa limekosewa, pili inaelekea kuwa tender ya vitambulisho ilishawahi kutangazwa na ikaleta matatizo.

Wazee, forum hii imepata heshima kwa kuwa inashusha nondo (kama anavyoziita Mzee Es) zenya manufaa kwa wasomaji na taifa kwa ujumla, sasa member anapoanzisha tetesi anaziita habari za uhakika then anapotea inashusha hadhi ya forum.

Wazee tunasubiri nondo zenye kujenga taifa kwani safari bado ni ndefu. Our beloved country is bigger than any body.

Mpaka Kieleweke rudi utupe hizo habari za kuaminika kwa undani zaidi.
 
Hizi story zilianza siku nyingi sana,kwanza ilikuwa ni mtoto wa JK na Rostam,sasa naona ni mtoto wa Lowassa....lakini si ndio haohao?
 
Yule aliyehusika na RDC ndiyo huyo huyo tena.. licha ya Lowassa kuomba watu wasilihusishe jina lake na kijana huyo... rejea maswali yangu kwa Hosea...
 
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Farao!
Huyo fred kaingia ubia na the famous bwana Albawadi wa Kempiski kwenye kampuni moja ya madini ya Tanzanite na sasa wako mbioni kujenga bonge la hoteli kwenye maeneo nyeti Arusha(usichanganye na 77)!
 
Mkandara, here is the problem.

Mtoto wa mkulima kama mimi na wewe hata kama tuna qualifications hatuwezi kushindana na watoto wa Lowassa au JK. (Ofcourse sisi ni wapiganaji..tutaweza...albeit all odds) lakini tatizo kubwa ni kwamba kwa mwendo huu...unaziba opportunities kwa wale ambao wako genuinely interested to improve their lot and the nation.

Weka playing level field..tangaza tenda..wacha watu washindane kwa vigezo. Then, hapo sitakuwa na shida wala maneno na bwana Alpha or any body! The problem is watu kama hawa katika maisha yao..wanategemea hisani na majina ya wazazi wao...indirectly unawaumiza wasio na connection like me! Nashukuru Mungu nilienda shule jamani...

Kwa mwendo huu...watoto wa wakulima we shall be forever in trouble!
 
Maskandali mwaka moja tu kibao. Je baada ya miaka kumi itakuwaje? Ndiyo maana nasema afadhari serikali ya BWM kulikuwa na seriousness.

Hawa wanamtandao wanatuchezea movie tu na sie wadanganyika hatujaona, tunafikiri jamaa bado wako honeymoon wanapanga mikakati ya maendeleo kumbe wenzetu tayari washanza mchezo.

JK kulinganisha na BWM ni kama maji na mafuta!!!!
 
Mzee wangu Augustine,

Nimekusikia sana, ila nadhani nimejaribu kuzama zaidi ya hivi Vitambulisho na tender!

Kitu kinachonishinda kuelewa ni hukumu gani tunawapa hawa vijana?. yaani baba yake akiwa Kiongozi basi hatakiwi kusaidiwa ktk maisha yake?... ndipo nilipo lazimika kukubali kuwa wanayo haki sawa na vijana wengine kwa wazazi wao. Hili la Lowassa kumpa kijana wake Tender, nadhani sote tumeshakubaliana kuwa ni uvunjaji wa sheria na wala haikutakiwa kuwepo tenbder hata kidogo.... lakini mzee kumwezesha mwanae afikie mafanikio kisheria nadhani hapa tutakubaliana pia kuwa sii haramu.

Tatizo kubwa ni mazingira yetu...na sielewi kabisa njia ya ku-deal na issue kama hizi.

Ni sawa na kumkopesha fedha Mbongo!.. Ukiwa nazo kutoa ni moyo na wengi watashangaa kama huna roho ya kusaidia, lakini siku utakayo mpa ndo imetoka. Fedha hutarudishiwa na matusi juu utapewa..kibaya zaidi huyo mkopaji ataendelea kuwa maskini kalamba zote na mabinti!

Ndio maisha yetu na wengi husisitiza kuwa Tenda wema wende zako! Je, huku si kuangushana?.
 
Wazee,

Tender ya vitambulisho bado hatujawa na uhakika, mara kaingia ubia na the famous bwana Albawadi wa Kempiski. Jamani tuwekane sawa kidogo.
 
wale Digimarc walitupwa ama wale ni wa kutengeneza Shahada za kupigia kura?
 
Back
Top Bottom