Mkuu,
Hii hali inayoendelea ni nchini kote,kila kipembe, mkoa, mji na kijiji.
Lililo baya ni kuwa kiwango cha wagonjwa wa kisukari itazidi sana kwa sababu watu watalazimika kula vyakula vya uwanga tu zaidi. Pia utapia mlo kwa watoto na watu wazima.
Hii itapelekea watu kufa kama kuku na kuziumiza familia nyingi kiuchumi zaidi ya huu umaskini walionao leo.
wakati watawala wetu wanataka tuamini uchumi unaboreka, uhalisia wa maisha kwa wananchi wa kawaida uko tofauti, maisha yao yanazidi kudidimia na kuwa ya shida zaidi.
Katika nchi nyengine wananchi yamewashinda na wamepeleka ujumbe kwa watawala, sisi hatujafikia kiwango cha ujasiri bado. Tunakula "amani na utulivu wetu" huku tunajifea kama kuku na hata wa kutuzika hatuna.....Lakini tutafika! Lini!!???
Serikali inavyosema inajizatiti kukabiliana na kisukari... Vituko kweli kweli!
Hii habari ipo IPPMEDIA
Serikali yajipanga kudhibiti kisukari
Na Elizabeth Zaya 27th January 2011
[FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali imezindua programu maalum inayolenga katika kushughulika na udhibiti wa ugonjwa wa kisukari nchini ambapo jumla ya Dola za kimarekani milioni 2.3 zinatarajia kutumika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizindua programu hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Hussein Mponda, alisema programu hiyo itadumu kwa miaka minne na lengo lake ni kuhakikisha ugonjwa huo unadhibitiwa kwa asilimia kubwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dk. Mponda alisema kati ya magonjwa yasiyoambukiza, kisukari ndio unaonekana kuwa wa kwanza kwa kuongeza idadi ya wagonjwa ambapo asilimia tano mpaka sita ya wagonjwa wa kisukari wanaishi mijini, na asilimia moja tu ni waishio vijijini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alizitaja baadhi ya sababu zinazochangia ni umaskini, matumizi mengi ya tumbaku, kutofanya mazoezi, matumizi mabovu ya chakula na matuimizi mengi ya kilevi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha alisema programu hii pia inalenga kutoa huduma kwa wagonjwa wanaougua ugonjwa huo katika Hospitali, Kliniki na katika kila Zahanati zilizoko nchi nzima.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kwa sasa Serikali imeboresha mfumo wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa kisukari, kwa kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapatiwa elimu mahsusi ya na namna ya kujijengea tabia ya kupima ugonjwa huo kila mara ili wale wanaobainika waweze kutibiwa mapema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aliongeza kuwa endapo wananchi watajenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara, idadi ya vifo vinavyotokana na uzembe wa kuchunguza afya vitapungua.[/FONT]