Tanzania kabla ya sasa

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
1. Kabla ya mwaka 1999 tanzania ilikuwa nchi pekee kubwa duniani kutokuwa na tv ya taifa.

2. Kabla ya uhuru wa kuanzisha vyombo binafsi vya habari kulikuwa na radio moja rtd, magazeti ya dailynews na sundaynews, uhuru na mzalendo na gazeti la mfanyakazi.

3. Mwenyekiti na katibu wa chama cha mpira wa miguu fat waliteuliwa na serikali.

4. Chama cha wafanyakazi kilikuwa ni jumuiya ya chama tawala, ccm (juwata), hakukuwa na miagomo wala maandamano wakati huo.

5. Timu ya YANGA ikipata ushindi enzi hizo walishangilia ccm!,ccm!,ccm!...jaribu siku hizi uone!

6. Kiongozi alikuwa akikaribishwa kwenye mikusanyiko kwa kibwagizi cha chama chetu chajenga nchi.

7. Bendi za dansi hazikuweza kuruhusiwa kurekodi nyimbo zao bila kuanza kwanza na wimbo wa siasa kusifu chama au viongozi.

8. Usafiri wa uma mikoani, mabasi ya kamata na trc.

9. Bidhaa muhimu ziliruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya ushirika tu.
 
Vyama vingi vimeleta mageuzi

Really?

Mageuzi yepi hayo? Nionavyo mimi bado Sisiemu imeshika hatamu, kama vile TANU na ASP vilivyokuwa vimeshika hatamu kabla ya kuungana na kuunda Sisiemu.

Kila kitu nchini kinapigwa mnada kama viongozi hawana akili nzuri (Vyama vya upinzani vimefanya nini?)
Hospitalini ndo usiseme, wenyewe (wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala) wanatibiwa nje, hata check up ni nje ya nchi!
Ati bado watoto wanafeli darasa la saba-halafu waende wapi?-watoto wenywe wana miaka 13-16 wanaanza kazi.
Haki za binaadamu zinavunjwa kama watanzania hawana akili nzuri vile- vihausi geli vingi vina miaka 10 tu!
Mvua ikinyesha kidogo ndo hivyo tena! Sasa ngojeni kipindupindu kitakavuoongezeka kwa nguvu!
nk nk
 
Back
Top Bottom