Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Mojawapo ya mambo yaliyonichefua kwenye muswada wa katiba ni pamoja na Part III hasa section 5 na 6. S.6 inasema kuwa wajumbe wa tume watatoka pande zote za muungano kwa idadi sawa (yaani kama wajumbe ni kumi basi Zanzibar watoke 5 na Bara watoke 5), ukienda mbele zaidi unaona kuwa maamuzi ya watu wa Bara yanaamuliwa na Wazanzibari.
Bunge letu lina wabunge takribani 360, kati ya hao zaidi ya 75 wanatoka Zanzibar (kama asilimia 20 hivi) sasa hili suala la katiba kwa nini tusitumie uwiano wa wabunge au hata uwiano wa watu, je kwa nini serikali yetu inabembeleza sana huu muungano?
Nadhani inabidi hii ipingwe kwa nguvu zote na wabunge wa bara maana huku si kuimarisha muungano bali kuendekeza upendeleo ambao nisingependa kuutaja hapa