Tanzania ina wahasibu na wakaguzi 8,000 tu wenye CPA za Bongo!

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
mhasibu.jpg

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) imesema kwamba Tanzania ina uhaba mkubwa wa wahasibu wenye CPA (Certified Public Accountant) ambapo kwa sasa walio na sifa hizo ni 8,000 tu nchi nzima waliofanya na kufaulu mitihani inayotolewa na taasisi hiyo ya umma.

Kwahiyo, NBAA wanasema wanahitaji kuwa na wahasibu wengi zaidi nchini wenye CPA, kwani mahitaji ni makubwa.

Humphrey Sympholian kutoka NBAA anasema kwamba, Sheria ya Wakaguzi na Wahasibu ya Mwaka 1974 inafafanua bayana kwamba, mtu au taasisi yoyote inayofanya miamala inayoyozidi Shs. 20 milioni ni lazima awe na mhasibu mtaaluma mwenye CPA.

Ameeleza hayo katika warsha iliyoandaliwa na Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) leo hii ikiwakutanisha marais wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania pamoja na Jukwaa la Wafanyabiashara (JWT) na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika kongamano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mhasibu House jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa marais walioshiriki kongamano hilo ni kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (College of Business), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (College of Business), Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ushirika Moshi (MoCU), St. John’s Dodoma, IAA Arusha, TIA, University of Iringa na IFM.

Mwenyekiti wa TAA, Dkt. Fred Msemwa, amesema kongamano limelenga kuwanoa kifikra na kuwajengea uelewa mpana kuhusu masuala ya ajira na mafunzo kwa vitendo na lilenga kuwasajili wanafunzi wote wa uhasibu na masuala ya fedha kwa vyuo vikuu vinavyotoa taaluma hiyo.

Dkt. Msemwa amesema kupitia kongamano hilo wanafunzi watafahamu changamoto mbalimbali ndani ya jamii ambazo watakwenda kuzifanyia kazi wawapo kwenye mafunzo.

Lakini changamoto kubwa iliyoonekana kwenye kongamano hilo, ni uhaba wa wanachama licha ya kwamba TAA ina umri wa zaidi ya miaka 30 sasa tangu ilipoanzishwa rasmi mwaka 1983 kama taasisi isiyo ya kiserikali.

Dunstan Nyeme, ambaye ni mhasibu wa chama hicho, amesema mpaka sasa TAA ina wanachama 1,500 tu, ambapo kati yao 1,250 ni Wataalam Wahasibu na Wakaguzi na 250 ni wahasibu wanafunzi.

Kwa upande wake, Noel Lewis kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) amesema suala la uhasibu limekuwa changamoto kwao kutokana na sheria zilizopo.

“Tumeshapaza sauti zetu katika majukwaa mbalimbali, ikiwemo bungeni hivyo tunaamini Serikali itasaidia kutatua changamoto zetu wafanyabishara hasa katika masuala ya kodi,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Rais wa Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Laurent Wilson amesema kupitia mafunzo hayo watapata muongozo wa namna watakavyowaunganisha wafanyabiashara katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uhasibu na mahesabu.

Kutokana na hali hiyo, kongamano hilo limelenga (kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa TAA Victorius Kamuntu) kuhamasisha wanataaluma wa fani ya uhasibu kujiunga, lakini wakitilia mkazo kuhakikisha wanakuwa na mpango wa pamoja na ushirikiano wa wanafunzi wa elimu ya juu katika kuhakikisha kwamba wanajiunga.

Kwa maana hiyo, TAA imedhamiria kuwasajili wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini wa masuala ya uhasibu na fedha.

Malengo yao mengine ni haya yafuatayo:

Chama kuwa na mpango wa Pamoja na Ushirikiano wa wanafunzi wa Elimu ya Juu katika kuwapa uelewa mpana kuhusu masuala ya Ajira, Biashara na mafunzo kwa vitendo hasa kwa wahitimu .

Kutoa mafunzo kwa wanachama wanafunzi ambayo wataenda kufanyia kazi mara wawapo kwenye mazoezi na baada ya kuwa wamemaliza vyuo na Mafunzo.

Chama kimeandaa majadiliano ambayo yatawashirikisha wadau wengine kama Wizara ya Viwanda, JWT, NBAA kuona namna wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali watasaidiwa katika masuala ya utunzaji wa kumbu kumbu za awali za mahesabu kama sehemu ya mafunzo yao.

Chama kusajili wanafunzi wote wa uhasibu na masuala ya fedha kwa vyuo vikuu.

Kila chuo kupitia uongozi wa wanafunzi wanachama wote kupatiwa vyeti maalum vya utambuzi kuwa tayari wamesajiriwa na majina ya wanafunzi wote kuwekwa kwenye tovuti ya Chama cha Wahasibu.

Chama kuwashirikisha wanachama wake katika mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuwapa uelewa mpana.

Kuandaa na Kushirikiana na Bodi ya Uhasibu ili wanafunzi walio wengi wajiunge na kuanza kufanya mitihani ya Bodi ya Uhasibu.

Kuendelea kuwaombea nafasi za kujitolea hasa wanafunzi wanachama wanaohitimu vyuo kabla ya ajira katika viwanda mbali mbali.

Kuwajengea uwezo kabla ya kumaliza masomo ili waweze kukabiliana na changamoto katika ajira mafano kwa matumizi ya technolojia kila mhasibu walau lazima ajue “Accounting Package” .

Kuwepo na Makongamano kwa wataalam wabobezi kwa masuala ya Uhasibu, Ukaguzi na biashara ili kuwavutia wanafunzi katika kupata uzoefu na kupenda kujifunza Zaidi.

Kushirikiana na Taasis zingine pale panapohitajika.


Nyeme anasema malengo ya TAA ni pamoja na kutoa mafunzo ya viwango mbali mbali vinavyotolewa na wasimamizi wa taaluma za Uhasibu na Ukaguzi (IFAC na NBAA) kwa wanachama wake ili waendane na Mabadiliko hayo katika utoaji wa huduma.

Pia, kutoa elimu kwa wanachama wake ambayo itasaidia kuendana na mazingira na mabadiliko ya teknolojia na kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanachama, ili kukabiliana na changamoto katika ajira na kufikia uwezo wa kuajirika.

Kwahiyo, anasema, kuna faida nyingi za wanafunzi watakaojiunga uanachama, ambazo ni pamoja na:

Kupewa vyeti vya uwanachama kwa kila mwanafunzi atakaejiunga na chama.

Kupata mafunzo yakayotolewa na chama hasa yakuweza kukidhi mabadiliko ya kiteknolojia na kupatiwa vyeti.

Kuwaunganisha na kuwaombea nafasi za kujitolea katika taasis mbali mbali hasa viwanda vidogo ili wapate uzoefu.

Kupokea maombi kwa wanachama wanafunzi ambao wangependa kupewa barua za utambulisho kwenye taasis mbalimbali kwa ajili ya kujitolea ama kufanya kazi kama zinahitajika.

Kuhudhuria mafunzo yatakayo andaliwa mara kwa mara vyuoni.

Kupatiwa taarifa za fursa mbali mbali za kujiendeleza.

Kupatiwa fursa ya kuongea na wafanyabiashara waliofanikiwa.

Kuunganishwa na kupatiwa mafunzo ya vitendo ya biashara za mitandao (e-business).

Kuendelea kufanya mikutanao na viongozi wa wanafunzi kutatua kero za namna ya kuandaa wasifu, namna ya kujisajiri ili kuanza kufanya mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi n.k.


Kwa idadi hiyo anayoisema, maana yake hao hawatoshi hata kwenye taasisi za umma kuanzia halmashauri, ofisi za wakuu wa wilaya, mikoa, wizara na idara mbalimbali, achilia mbali taasisi binafsi na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) ambavyo kwa sasa vinakadiriwa kufikia 1,000 nchi nzima.

My Take:
Uhasibu ni miongoni mwa sekta nyeti na muhimu, lakini ambayo imekuwa haiangaliwi kwa umakini hata na jamii na ndiyo sababu hata chama husika kimeshindwa kuwa na wanachama wa kutosha licha ya ukweli kwamba wanaohitimu fani ya uhasibu na sekta ya fedha kwa ujumla ni wengi.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba, wanataaluma ya uhasibu wenyewe hawataki kujirasmisha kama zilivyo taaluma nyingine zikiwemo ualimu, utabibu (udaktari), uanasheria, uhandisi na kadhalika, hali ambayo inawafanya wasionekane umuhimu wao hadi pale mtu, watu, kikundi au taasisi inapohitaji huduma ya kihasibu.
Kwa mukhtadha huo, ninaona kwamba, uamuzi wa TAA kupita kwenye vyuo vikuu vinavyohusika na masuala ya uhasibu na fedha ili kuwasajili wanafunzi wawe wanachama ni mzuri kwa kuwa naamini yawezekana wengi wao hawakuwa wakijua ama hawaoni umuhimu wa kujiunga na vyama hivi.

Naomba ‘nisinene nikamala’, huu ni mtazamo wangu tu, nakaribisha maoni mbalimbali kuhusu hili.
 
NBAA ijitathmini namna nzuri ya kuwafanya wataaluma wa uhasibu kuwa wanachama wa bodi, changamoto kubwa ya NBAA ni kuwa haiko na hari ya kuongeza wanachama kivitendo ndio maana mfumo wao sio rafiki kwa wanaohitimu kozi za uhasibu, mfumo walio nao wataaluma wengine kama wafamasia, wauguzi, madaktari, wanasheria, waalimu, n.k unawapa fursa kujiunganisha moja kwa moja na bodi zao za kitaaluma tofauti kabisa na bodi ya uhasibu....
Mfumo wa mafunzo ya kitaaluma ili kufannya mitihani ya bodi ya uhasibu uko too individual and disorganized kwa maana ya kwamba MTU alieko wilaya za ndani ya nchi na baadhi ya mikoa hana access ya kusoma kwa nafasi na akafanya vizuri mitihani yake kwakuwa learning centres nyingi ziko mikoani na mikoa iliyo endelea tu. alieko kigoma anaweza kosa sehemu ya review classes mpaka aende mwanza kwa mfano ndipo apate access napo atatumia gharama kubwa na ikiwa ni mwajiriwa anawezaje pata ruhusa kirahisi? Matokeo anafanya mtihani kwa maandalizi hafifu na failure rate inaongezeka daily au anaamua kupuuza anabaki na cheti cha chuo only.
Wanasheria wanayo law school kwa wote...
 
Back
Top Bottom