Tanzania govt on Homosexuality: We can do without UK aid

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa , BERNARD MEMBE jana aliungana na Rais wa Zanzibar , Dr. Ali Mohammed Shein na Rais a Ghana John Atter Mills kupinga kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon ya kutaka nchi zinazoomba misaada kwao zitambue haki za Mashoga.

"Hili suala ndio sera ya Conservative (chama anachoongoza Cameroon ambacho ni wafadhili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Waliipa baiskeli, pikipiki na magari uchaguzi wa mwaka 2005 na 2010). sasa wanaliunganisha na masuala ya misaada.

Awali lilichomoza kwenye vikao vya maofisa waandamizi wa jumuiya ya Madola. Waingereza wliupenyeza kwenye ajenda ha haki za binadamu mawairi tukalikataa kwenye kikao chetu, alisemA Membe.
Alisema mapema mwaka jana nchi moja kubwa rafiki na Tanzania aliteua balozo wake mpya nchini aliyekuwa aje na mke mwanaume mwenzake lakni Rais Kikwete alikataa na hatimaye akabadilishwa.

 
Acha ziendelee kuwa habari zisizo rasmi maana nchi yetu haina dini na OIC ni kwa ajili ya muslim world
 
Kwenye kurasa yake ya Twitter Mh. Kikwete amemnukuu Waziri Membe kama hivi:

"Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake. Hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja. Hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nchi nyingine. Miongoni mwa nchi 54 za Jumuiya ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo cha miaka 30. Nchi yetu haiwezi kuyumbishwa na masharti ya aina hii na kamwe hatutaruhusu kuingiliwa na nchi nyingine." (Mh.Bernard Kamilius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa)

Jakaya Kikwete
@jmkikwete Tanzania, East Africa


lakini mbali na yeye kujibu kwa kutumia mtandao wa twitter lakini nchi haiwezi kuongozwa kwa kauli za kwenye twitter. tunataka rais aitishe kongamano la kujadili suala khili na majibu yatayotoka hapo ndio yawe msimamo wa taifa na kama tunajitoa jumuia ya madola au la... na tuende mbali ata kuvunja uhusiano wa kibalozi na uingereza kwani ametutawala kwa muda mrefu alichukua rasilimali zetu kipindi cha ukoloni wake na mpaka sasa hakuna fidia aliyolipa kutokana na madhara ya ukoloni aliotufanyia

kutokana na madhara yote tuliyopata tokana na ukoloni wake bado tumejiunga na jumuia ya madola kwanini tuendeleze fikara za kikoloni mpaka leo?

kama kweli nchi hii kuna viongozi basi tunataka waseme tunawafanya nini waingereza kutokana na kauli yao ya kudhalilisha utu wetu na pia watuambie wananufaika nini kuendelea na jumuia ya madola?

Na kama hii haya ndio masharti ya misaada lazima rais atuambie anapotembea huko yeye binafsi anapewa masharti gani? mbali na haya waliyoweka kwa nchi nzima
 
Kuna taarifa za chini kwa chini kwamba wakuu wa nchi wanangoja uungwaji mkono wa wananchi ili kujitoa katika jumuia ya madola kwasababu ya matamko ya waziri mkuu wa uingereza kushinikiza ushoga kwenye nchi zinazoomba misaada kwa uk, pia jumuia hii imekuwa ni kama muendelezo wa ukoloni mamboleo na hakuna faida yoyote kutokana na kuendelea kuwepo katika jumuia hii

kama unaunga mkono wazo la kujitoa kwa Tanzania jumuia ya madola pls send sms au tuoa tamko kwenye post hii , vile vile kama unapenda Tanzania kuendelea katika jumuia ya madola vile vile weka komenti zako hapa na sababu

Mi naunga mkono kwa Tanzania kujitoa na Watanzania wote tunapaswa kulikubali hilo kwani hata hiyo jumuiya yenyewe haikuwa na tija kwetu,pili kwanini watulazimishe kuhalalisha jambo chafu kama hiilo kisa msaada tuu??Kwa kauli ya Cameroon ni sawasawa kuwa anapima msimamo wa nchi zetu,anajua ni la kipumbavu lakini anapima kwani nasi twajua hilo ni la kipumbavu sasa tukikubali tutakuwa wapumbavu zaidi ya alivyofikiria.
Shupavu
 
Naona hapo watawafurahisha bakwata, lakini wananchi wengi ambao tunaamini nchi na serikali yetu haina dini tutaendelea kuupinga uamuzi huo mpaka pumzi ya mwisho.
 
hatuwahitaji wafadhili wa aina yoyote ile.........................tunachohitaji n kumwamini Matnzania ya kuwa atajiletea maendeleo yake mwenyewe...............OIC mbona haisaidii Palestine na hususani Gaza ambako wanaishi maisha ya aibu na umasikini ule wa kutupwa................halafu gadaffi mbona walimtelekeza.....................na Saddam Hussein pia walimtelekeza........................nchi zilizomo kwenye hiyo jumuiya mbona hazionyeshi mwelekeo wa maendeleo?
 
Huwezi kuwa ombaomba halafu ukasema eti hutaki masharti! Hakuna kitu cha bure...mwenyewe JK alishawahi kusema "ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa japo kidogo".

Duuu! Hii ni hatari ,hatari kweli kweli !!!!
 
Maamuzi magumu yanatakiwa yafanyika kama BAKULI is the only major means of existence.
 
Kitakapofanyika kikao au sherehe za Wake za Mabalozi waishio nchini, "jamaa" ataenda??
 
ni hivi karibuni jk na salma wametoka huko, sasa sijui kilichoongelewa huko, ntafurahi sana kama tukijitoa but upande wa pili nikiangalia haya maviongozi yetu ya ccm, esp. hii awamu ya jk inayoongoza kwa kuwa matonya kuliko awamu zote naona kama vile itakuwa ngumu kwao kujitoa coz wanawategemea sana kiuchumi katika kuendesha nchi
 
....kwa sababu ya ushoga au?
...maskini wale watu walivyomfanya baba Mutasin.
 
Habari zisizo rasmi baada ya Uingereza kuleta kizungumkuti serikali kwa kupitia waziri wa mambo ya nje kufikiria uwezekano wa kujitoa kwenye jumuiya ya madola na kujiunga OIC. K wa mujibu wa source inaonekana kuwa hii huwenda ikapata baraka mapema sana kutokana na hali ya uchumi inavyokwenda sasa nchini.
Wananchi wataombwa kuacha udini na kujali utamaduni ili kubariki kujiunga na OIC kwa dhumuni la kujikwamua kiuchumi baada ya mfadhili wetu uingereza na nchi nyingine za ulaya zinazosubiriwa kutangaza kuunga mkono uingereza kuweka hicho kama kigezo kikuu cha msaada.

Nchi za scandnavia huenda zikatoa nazo tamko hivi karibuni kuweka kigezo cha haki za binadamu (including MASHOGA) kama sababu ya nzito ya kupata msaada chanzo kimeeleza.

Membe na binamu yake JK hawana njia mbadala isipokuwa OIC chanzo kimeelezwa.

OIC: The Organisation of Islamic Cooperation (OIC) (formerly Organization of the Islamic Conference) is the second largest inter-governmental organization after the United Nations which has membership of 57 states spread over four continents. The Organization is the collective voice of the Muslim world and ensuring to safeguard and protect the interests of the Muslim world in the spirit of promoting international peace and harmony among various people of the world.

The Organization was established upon a decision of the historical summit which took place in Rabat, Kingdom of Morocco on 12th Rajab 1389 Hijra (25 September 1969) as a result of criminal arson of Al-Aqsa Mosque in occupied Jerusalem


Hapo ndipo pale yale maamuzi magumu tena.


Kwani mkuu hatuwezi kuishi bila kutembeza bakuli la omba omba? Lazima tukijitoa jumuia fulani tuhamie nyingine kwa sababu ya kuomba? Je nako wakiweka kigezo cha kuwa lazima tuoe wake wanne? Itakuwaje?
 
'Jamani safari zangu ninazozifanya nje ya nchi zina manufaa makubwa sana kwa nchi yetu,tunapata misaada mikubwa toka kwa nchi hizi hasa katika bajeti yetu,kwa wanaobeza safari zangu nje ya nchi hawawatakii mema wananchi wa nchi yetu na tusipopata misaada hii nchi yetu itayumba"Kauli ya JK.
Tumekwisha maana viongozi wetu hawana njia mbadala ya kutatua matatizo ya wananchi bila misaada toka nje.
 
Kikwete tunamkubali watanzania.Mambo yake kimyakimya sio mtu wa majigambo kama CDM.Nasikia yapo mambo mengi sana ameisha yazuia akiwemo lile suala la mabalozi kuwapa fedha wapinzani ili kung'oa CCM.KIKWETE nomaaaa yaani kimyakimya tu.
 
Back
Top Bottom