Tanzania employment services agency (TaESA)

KANCHI

JF-Expert Member
Sep 3, 2011
1,533
230
Vp jamani wana jf aliyewai kupata kazi kupitia hawa jamaa anipe maujanja bac kwani nataka kuwasiliana nao wanisaidie na mimi nipate pa kupatia shibe.
 
hata mimi natafuta sana hayo maujanja mwenye info please help us
 
Taasisi ikishakuwa ya serikali uchakachuaji unakuwa ni mwingi sana, cha msingi hangaika kutumia private requiting angencies huku huwa hakuna uchakachuaji mwingi
 
Hii wizara ya Kazi na Ajira Tanzania ingefutwa tu....coz nafikiri ni mzigo tu kwa serikali!!
 
Pale unapeleka vyeti vyako orijino wanakusajiri, then unaendelea na mishe zako mpaka kama wakikupigia simu...
Uzuri wa taasisi kama zile wakikuita wao wanakupiga interview wao basi unapewa kazi ila ngoma ni ngumu sana mpaka wakuite...
Nina washkaji zangu kadhaa wamepata kazi za maana sana saiv!
Ofcoz kuna kujuana sana pale ila tatizo kubwa saiv makampuni mengi yanaajiri yenyewe badala ya kutumia taasisi kama zile..

Ila haigharimu kitu, we peleka vyeti orijino tu wanakusajiri then unarudishiwa vyeti vyako wala hawachukui copy so utagharamia nauli tu....
Fanya usajiri wateme wakikuita poa, wasipokuita poa pia
 
Mimi wameshanizingua sana,coz nilipeleka cv zangu 2009 wakaniita 2011 lakini ni uzushi mwanzo mwisho yaan kuchakachua ...
kwanza kama kuna kazi ya maana kwanza wao wenyewe wajipgia pande kwa hiyo utangoja sana.........
 
hiyo kitu ni real.ila tu uwe na elimu at advanced na bachelor nafasi huwa ni kubwa, hamna ubabaishaji wowote.upeleke tu mkuu
 
Mimi wameshanizingua sana,coz nilipeleka cv zangu 2009 wakaniita 2011 lakini ni uzushi mwanzo mwisho yaan kuchakachua ...
kwanza kama kuna kazi ya maana kwanza wao wenyewe wajipgia pande kwa hiyo utangoja sana.........

Hiyo ni Taasisi ya serikali, haina nafasi za kazi bali inasaidia kuwapatia mbinu watafuta kazi za namna ya kujijua (self assessment/analysis) kama unaweza kupambana vema katika soko la ajira kwa kujitafutia kazi nchini na nje ya nchi, kuandaa maombi ya kazi pamoja na cv, kujiamini na kujibu vema katika usaili, kujiajiri au kuajirika. Inategemea kwa kiasi kikubwa kuletewa mahitaji ya ajira kutoka taasisi binafsi, lakini si lazima wapitie TaESA. Kuilaumu TaESA ni sawa na kujilaumu mwenyewe, isaidie ili ikusaidie. Aidha, ni kituo kikuu cha taarifa za soko la ajira. Kina wajibu wa kufanya uchambuzi wa mahitaji ya soko la ajira nchini na nje ya nchi na kutoa ushauri kwa serikali, shule, vyuo, taasisi za utafiti na wadau mbali mbali kuhusu umuhimu wa kutengeneza mitaala inayoendana na mahitaji ya soko la ajira. Ili uweze kuwa na ushindani wa kimkakati katika kukabiliana na mahuitaji ya soko la ajira unantakiwa ujiandae vema katika masomo yako, otherwise, jipange kujiajiri.
 
mnnnh kazi iipo,subira yavuta kheri ila ukisubiri sana huwa shari.

haraka haraka haina baraka.

ngoja ngoja yaumiza matumbo.

chagua moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom