Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu

NAOMBA UNISAIDIE NAMNA YA KUMFUKUZA MAMA YANGU MZAZI KWANGU NIMECHOKA!

Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu wkani nilikua nafahamu jinsi Mama wakwe walivyo na roho mbaya. Kweli sikuishi naye, Mama mkwe wangu hata hakuwahi kuja mjini kusalimia, ndoa yangu ilikua na amani kwa miaka 12 ya mwanzo. Lakini mwaka jana mwanzoni Baba mkwe wangu alifariki dunia, Mama mkwe ni mtu mzima ana miaka kama 67.

Alibaki kijijini mwenyewe hivyo mume wangu kwakua ndiyo mkubwa kwao aliniambia kuwa anataka kumchukua Mama yake kuja kuishi naye. Nilikataa wkani nilishajiapiza hivyo, lakini mume wangu alisema hawezi kumuacha Mama yake akiteseka kijijini. Nilikubali shingo upande lakini ili kumkomoa mume wangu nilienda kijijini na kumchukua Mama yangu ili tuje tuishi wote.

Mimi Baba yangu yuko hao, lakini nilidanganya kuwa Mama je Dar kuchekiwa kwani mara nyingi alikua analalamika miguu, basi alikuja nikijua kuwa, wakiishi na Mama mkwe wangu watagombana au mume wangua tachukia na kumfukuza Mama yake ili tuishi wenyewe. Mama yangu alikuja mwaka jana na mume wangu alimpokea vizuri, tuna nyumba kubwa tu hivyo hakuna tatizo kwa hilo.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, Mama mkwe wangu pamoja na umri wake mkubwa ni mtu poa sana mpaka naona aibu, anamka anafanya usafi nyumba nzima, yaani hata kama nipo anasema hapana nikikaa hivi sifanyi kitu nitakufa kwa uzee, ananisaidia kupika, anapenda watoto, alikua Mwalimu, yaani anafundisha watoto wangu, wananidhamu na wanamuelewa kuliko hata mimi.

Hana kelele na sasa hivi mume wangu alikua mlevi ila kwa Mama yake kaacha pombe kwani Mama alimuambia hawezi kula chakula mtoto wake akiwa nnje hivyo ni kama kamnyoosha, yaani Kaka Mama mkwe wangu hana shida. Shida imekuja kwa Mama yangu, ana visa mpaka naona kama anataka kunivunjia ndoa yangu. Mwanzo nilikua namuona Mama yangu kama mtu wa kawaid, hana maneno na nimu mzuri.

Lakini baada ya kuja Dar, kwanza ni mtu wa majirani, yaani yeye akiamka Mama mkwe kashapika chai anywe aende kwa majirani, tunapokaa si uswahilini sana ila kuna majirani kashazoea nao. Pili anavituko vingi, napenda kugombeza watoto na akigombeza anatukana kabisa, lakini pia mimi na mume wangu tunafanya kazi, tuna utaratibu wa kufanya vitu kwa pamoja.

Mama yangu hivyo hataki, analeta maneno maneno kuwa mume wangu hachangii chochote, mimi ndiyo namlisha na vitu vingi, kisa tu mimi nafanya kazi serikalini na Mume wangu binafsi hivyo anajua mimi nina akili sana na nina pesa nyingi sana hataki nichangie chochote. Anashindwa kujua kuwa msahara wa mume wangu ni zaidi ya mara tano ya mshahara wangu na kila kitu tunaandika majina yetu au ya watoto.

Mama yangu baada ya kuja huku kuna jirani yetu alimshawishi na kuingia kanisa moja hivi, basi baada ya kuingia huko akaambiwa kuachana na Baba kwani yeye hajaokoka, basi sasa hivi ni kwamba wamegombana, yaani hata ukimuambia kuhusu kurudi nyumbani anakataa kwakua kaambiwa haezi kuishi na mtu si wa dhehebu lake. Shida nyingine nikuwa, anasumbua kuhusu fedha za sadaka, yaani hata kama huna ataongea na hapo nyumbani hakutakalika.

Usiku anaweza kufungua Radio, akafungulia nyimbo kwa nguvu vila kujali kama watu wamelala, sasa hivi kaanza kitu kingine, kila siku saa nane usiku huamka na kuanza kukemea mpaka asubuhi. Yaani kaka ni mambo mengi mpaka najuta, mume wangu hajwahi kunilalamikia hata siku moja lakini najua kuwa anaumia na vituko vya Mama yangu an ipo siku atachoka.

Naomba nisaidie Kaka, nifanye nini, nina ndugu zangu hapa Dar nikiwaambia wanisaidie kumchukua wanakataa kwani washamjua tabia zake wananiambia sikutumwa kumchukua kijijini. Yaani nina mdogo wangu yeye hana ndoa anaishi mwenyewe, nimemuambia amchukue Mama kabla hajanivunjia ndoa yangu yeye anasema angalau mimi nina ndoa ya kuvujja yeye akiishi na Mama hata ndoa hataipata, nisaidie, nifanye nini, nimfukuzeje wakati kijijini Baba hamtaki kwasabbau ya dini, nisaidie Kaka?
Haya tupe mrejesho wana nzengo.
 
Safi sana hizo karaha unazipata kwa mama yako angekua mama wa mwenzio hapo ungejipa unabii kua ndo mana ulipata maono ya kutoishi nae
 
Unatafuta laana wewe si bure.aya za mwanzo pale juu zinaonyesha unaroho mbaya sanaaa
Ila ulibadilisha gia angani baada ya kuona mama mkwe wako anakusaidia baadhi ya mambo..asingeonyesha huo msaada kwako basi ungemtesa sana na kuishi nae jino kwa jino.

Mungu alivyokuumbua sasamama yako ndo kivuruge kweli kweli..safi sana.ukiamua kutoa upendo usichague mtu wa kumpa huo upendo.toa tu malipo yako yanaweza kuwa kwa watoto wenu huko baadae.

Kama uliweza kuonyesha hiyo roho mbaya kwa mama mkwe wako aliyekuzalia mume na mama ako aliyekuzaaa utashindwa kuua kweli!!vipi kwa watu baki utaweza kuwasaidia wapatwapo na matatizo kweli!!unaroho mbaya ni kinyama.mtu akisoma mwandiko wako kwa kina ataligundua hilo.

Kupitia huu mwandiko wako tayari nimeweza kugundua una umbo la namna gani.

Punguza roho mbaya mkuu.

Na utumie hekima ya hali ya kujuu kuongea na wazazi wako angalia ulimi wako usijekukunyang’anya hata kile kidogo ulichokishika mkononi.chunga sana.
Ana roho mbaya ya kishetani afu mchoyo
 
Acha nikucheke kwanza afu ndipo nikushauri dada 😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Ukiyataka mwenyewe sasa komaa nayo. Wewe hapo cha kufanya mnyime sadaka cha kwanza, pili likizo mwambieni mnaenda kjjn hivyo muongozane ila hilo lazima umshirikishe mumeo usimfiche mwambie unataka kufanya nini kuhusu mamako. Tatu, uwe unamkalisha na kumwambia ukweli usiogope akikuakasirikia wala nini. Nne, Fanya kumuondoa kwako mapema kabla haya lete sekeseke zaidi. Atakuja kusema mamako mkwe mchawi hapo hapatatosha atakuaibisha. La mwisho uachage kuwawazia watu mabaya kabla hauja wajua(mamamkwe).
NAOMBA UNISAIDIE NAMNA YA KUMFUKUZA MAMA YANGU MZAZI KWANGU NIMECHOKA!

Tangu zamani nilishaapa kuwa nikiolewa siwezi kuishi na Mama mkwe wangu wkani nilikua nafahamu jinsi Mama wakwe walivyo na roho mbaya. Kweli sikuishi naye, Mama mkwe wangu hata hakuwahi kuja mjini kusalimia, ndoa yangu ilikua na amani kwa miaka 12 ya mwanzo. Lakini mwaka jana mwanzoni Baba mkwe wangu alifariki dunia, Mama mkwe ni mtu mzima ana miaka kama 67.

Alibaki kijijini mwenyewe hivyo mume wangu kwakua ndiyo mkubwa kwao aliniambia kuwa anataka kumchukua Mama yake kuja kuishi naye. Nilikataa wkani nilishajiapiza hivyo, lakini mume wangu alisema hawezi kumuacha Mama yake akiteseka kijijini. Nilikubali shingo upande lakini ili kumkomoa mume wangu nilienda kijijini na kumchukua Mama yangu ili tuje tuishi wote.

Mimi Baba yangu yuko hao, lakini nilidanganya kuwa Mama je Dar kuchekiwa kwani mara nyingi alikua analalamika miguu, basi alikuja nikijua kuwa, wakiishi na Mama mkwe wangu watagombana au mume wangua tachukia na kumfukuza Mama yake ili tuishi wenyewe. Mama yangu alikuja mwaka jana na mume wangu alimpokea vizuri, tuna nyumba kubwa tu hivyo hakuna tatizo kwa hilo.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, Mama mkwe wangu pamoja na umri wake mkubwa ni mtu poa sana mpaka naona aibu, anamka anafanya usafi nyumba nzima, yaani hata kama nipo anasema hapana nikikaa hivi sifanyi kitu nitakufa kwa uzee, ananisaidia kupika, anapenda watoto, alikua Mwalimu, yaani anafundisha watoto wangu, wananidhamu na wanamuelewa kuliko hata mimi.

Hana kelele na sasa hivi mume wangu alikua mlevi ila kwa Mama yake kaacha pombe kwani Mama alimuambia hawezi kula chakula mtoto wake akiwa nnje hivyo ni kama kamnyoosha, yaani Kaka Mama mkwe wangu hana shida. Shida imekuja kwa Mama yangu, ana visa mpaka naona kama anataka kunivunjia ndoa yangu. Mwanzo nilikua namuona Mama yangu kama mtu wa kawaid, hana maneno na nimu mzuri.

Lakini baada ya kuja Dar, kwanza ni mtu wa majirani, yaani yeye akiamka Mama mkwe kashapika chai anywe aende kwa majirani, tunapokaa si uswahilini sana ila kuna majirani kashazoea nao. Pili anavituko vingi, napenda kugombeza watoto na akigombeza anatukana kabisa, lakini pia mimi na mume wangu tunafanya kazi, tuna utaratibu wa kufanya vitu kwa pamoja.

Mama yangu hivyo hataki, analeta maneno maneno kuwa mume wangu hachangii chochote, mimi ndiyo namlisha na vitu vingi, kisa tu mimi nafanya kazi serikalini na Mume wangu binafsi hivyo anajua mimi nina akili sana na nina pesa nyingi sana hataki nichangie chochote. Anashindwa kujua kuwa msahara wa mume wangu ni zaidi ya mara tano ya mshahara wangu na kila kitu tunaandika majina yetu au ya watoto.

Mama yangu baada ya kuja huku kuna jirani yetu alimshawishi na kuingia kanisa moja hivi, basi baada ya kuingia huko akaambiwa kuachana na Baba kwani yeye hajaokoka, basi sasa hivi ni kwamba wamegombana, yaani hata ukimuambia kuhusu kurudi nyumbani anakataa kwakua kaambiwa haezi kuishi na mtu si wa dhehebu lake. Shida nyingine nikuwa, anasumbua kuhusu fedha za sadaka, yaani hata kama huna ataongea na hapo nyumbani hakutakalika.

Usiku anaweza kufungua Radio, akafungulia nyimbo kwa nguvu vila kujali kama watu wamelala, sasa hivi kaanza kitu kingine, kila siku saa nane usiku huamka na kuanza kukemea mpaka asubuhi. Yaani kaka ni mambo mengi mpaka najuta, mume wangu hajwahi kunilalamikia hata siku moja lakini najua kuwa anaumia na vituko vya Mama yangu an ipo siku atachoka.

Naomba nisaidie Kaka, nifanye nini, nina ndugu zangu hapa Dar nikiwaambia wanisaidie kumchukua wanakataa kwani washamjua tabia zake wananiambia sikutumwa kumchukua kijijini. Yaani nina mdogo wangu yeye hana ndoa anaishi mwenyewe, nimemuambia amchukue Mama kabla hajanivunjia ndoa yangu yeye anasema angalau mimi nina ndoa ya kuvujja yeye akiishi na Mama hata ndoa hataipata, nisaidie, nifanye nini, nimfukuzeje wakati kijijini Baba hamtaki kwasabbau ya dini, nisaidie Kaka?
 
Shida yako ulimleta Mama yako kumkomoa Mmeo kwa kumleta Mama Mkwe ambaye asingeweza kukaa pekee yake kijijini.Ili kuleta amani lazima mama yako arudi kijijini kwa sababu Mmewe yupo ambaye ni Baba yako.Harafu amehubiriwa vibaya kabisa Kanisani!
Kanisa halina Mamlaka ya kumwachanisha Mme na Mke kwa visingizio kwamba Mmoja ameokoka na mwingine hajaokoka.
Kwa kuwa Mama yako ana Mme ambaye ni Baba yako ni kutumia busara arudi kwa Baba yako!
 
Back
Top Bottom