Tangu Mbowe atoke lupango hakuna tena upinzani, wote tuna macho na tunaona kinachoendelea

Unataka muda wote watu wazungumzie siasa,shughuli zao zakiuchumi nani atawafanyia?.Muda ndio itakaotuambia kua hao watu wapo au hawapo.sio lazima wafanye siasa kwajinsi unavyotaka.
 
daah! Umenikumbusha kumbe lisu bado yupo mara ya mwisho kumsikia kulipwa yale mafao yake ya ubunge, nimeamini mbwa mpe fupa ang'ong'e habweki tena.
Acha uongo lissu kila wakati anaongea,juzi tu katika kuulizwa maswali mengi na alikuwa anayatolea ufafanuzi kupitia club house.kama wewe.umejikita kusikiliza unayoyajua ya simba na yanga usitoe hitimisho kwa usichokijua.
 
Una akili Sana we kijana.. kiufupi Tz hakuna mtu aliopo kutetea maslahi ya Umma kabda ya maslahi yake. Ukiangalia vizuri Siasa zetu zinapamba moto muda ambao viongozi wetu Wana nufaika na Jambo husika. Mfn: Tumeskia kelele nyingi sana na wanahabari wakaitwa viongozi wakafanya vikao, wakaitisha maandamano kwa sababu tu Mbowe atoke jela( sio jambo baya). Je umeona wapi nguvu kama hiyo ikitumika kupinga mrundikano wa ushuru bandarini? Umeona Maandamano yakiitishwa kupinga Tozo, kupanda bidhaa au uwajibikaji m bovu wa watumishi wa Umma( mfn ARDHI, TRA, ). Si Chadema si Act si Cuf wote wapo kimaslahi binafsi then sisi badae.
Mkuu Kwani lazima wafanye viongozi wa vyama vya upinzani,kwa nini usianze kufanya wewe hapo ulipo organise watu mfanye hayo maandamano kupinga hayo unayoyasema.Kwa nini unataka uganyiwe-mabadiliko yanatakiwa kuanza na wewe sio lazima upinzani.
 
Na bado wanatutukana tuu kwa ujinga wetu. Mbowe anakaa jela, Lissu anachapwa risasi 16 mwilini, wengine wanapotea na kuacha familia zao wajane nk. Ila sie badala ya kuwaunga mkono na kuwapigania tunatumia muda wote kuhusu Diamond kumuoa Zuchu au Aziz ki na Chama nani bora.
Hivi Watanzania wanadhani Lissu au Mbowe walizaliwa wateseke kwa ajili ya Watanzania wajinga? Mbona mtu kama Mbowe ambaye Mungu alimbariki akazaliwa kwenye siagi na asali anaweza kujitenga na siasa na kuishi kwa amani tuu lakini hilo hatulioni?
Chadema, NCCR au CUF hawawezi kuibadilisha nchi kama wananchi wenyewe wamezubaa kama ma zombies hata wakipigwa tozo kwenye hela zao wenyewe walizo weka akiba Bank wanamsifu Rais.
View attachment 2333087
Kwani Lissu alipigwa risasi kwa sababu zipi?
 
Mwenye njia mbadala tofauti na TOZO atuambie ili tulifanyie kazi. TOZO zimekuja na zitaendelea kuja kwa sababu serikali haina mtaji wa kutosha. Je njia nyingine ya serikali kupata pesa ni ipi? Au serikali ipunguze nini katika mipango yake ili kutunusuru sisi?
Upinzani sio lazima kiongozi ndio awe na majibu. Akipewa majibu na mtu yeyote ya jinsi ya kuondokana na TOZO na akayaona yanafaa atatuambia. Na sio upinzani tu hata CCM wenyewe!
 
Moja kwa moja,

Kwanza niwasifu wapinzani wote waliojitolea maisha na muda wao kuleta sera mbadala, kukosoa na kushauri serikali pale inapobidi.

Wapinzani walipitia kipindi kigumu sana hasa hasa 2015-2020, bila kusahau 2021 ambapo Kiongozi mkuu aliwekwa ndani kwa tuhuma zilizoshindwa kuthibitika mahakamani.

Tangu Mbowe ametoka lupango, upinzani wa Tanzania umepata erectile dysfunction! Hali inazidi kuwa ngumu ila wote wapo kimya, wengine wanaenda mbali wanasifu na kutukuza hali ya sasa. Hatuelewi na hatuna hakika juu ya masharti(kama yapo) aliyopewa baada ya kurudi uraiani.

Kinachoshangaza watu wengi zaidi ni kuwa japo 2015-2020 walibanwa kweli kweli na J.P.M ambaye aliitwa dikteta, wengi walijitutumua na kuonyeha makali yao hasa hasa Tundu Lissu. Ila wakati huu ambao tunategemea wawe huru kutoa maoni yao, wote wapo kimya, yaani ni mwendo wa praise and worship!

Mi nashauri tu, tutangaziwe kuna chama kimoja nchini maana hakuna maana kuruhusu vyama vingi ili watu wapate options, at the same time hakuna wazo lolote mbadala linalotoka kwenye upinzani.

Vyama vya upinzani havifanyi hata 20% ya kazi yao, sio Lissu, Mnyika wala Mbowe wote wapo kimya.

Kila mtu apambane na hali yake, hii ndio sheria mpya katika siasa za bongo.
Alaa! Wakati wa Mungu wenu Ngosha simlikuwa mnasema upinzani unakwamisha maendeleo?
 
Moja kwa moja,

Kwanza niwasifu wapinzani wote waliojitolea maisha na muda wao kuleta sera mbadala, kukosoa na kushauri serikali pale inapobidi.

Wapinzani walipitia kipindi kigumu sana hasa hasa 2015-2020, bila kusahau 2021 ambapo Kiongozi mkuu aliwekwa ndani kwa tuhuma zilizoshindwa kuthibitika mahakamani.

Tangu Mbowe ametoka lupango, upinzani wa Tanzania umepata erectile dysfunction! Hali inazidi kuwa ngumu ila wote wapo kimya, wengine wanaenda mbali wanasifu na kutukuza hali ya sasa. Hatuelewi na hatuna hakika juu ya masharti(kama yapo) aliyopewa baada ya kurudi uraiani.

Kinachoshangaza watu wengi zaidi ni kuwa japo 2015-2020 walibanwa kweli kweli na J.P.M ambaye aliitwa dikteta, wengi walijitutumua na kuonyeha makali yao hasa hasa Tundu Lissu. Ila wakati huu ambao tunategemea wawe huru kutoa maoni yao, wote wapo kimya, yaani ni mwendo wa praise and worship!

Mi nashauri tu, tutangaziwe kuna chama kimoja nchini maana hakuna maana kuruhusu vyama vingi ili watu wapate options, at the same time hakuna wazo lolote mbadala linalotoka kwenye upinzani.

Vyama vya upinzani havifanyi hata 20% ya kazi yao, sio Lissu, Mnyika wala Mbowe wote wapo kimya.

Kila mtu apambane na hali yake, hii ndio sheria mpya katika siasa za bongo.
Mlikuwa mnawadharau CHADEMA naona akili zimeanza kuwarudi sasa mkiambiwa muandamane hamtaki mfanya tendo la ndoa tu na waume zenu wenzenu wapo lockup wanateseka. safi sn Mbowe piga kimya mpaka wapate akili
 
Wahenga walipata kusema:
1. Penye udhia tia rupia
2. Mkono mtupu haulambwi.
3. Sio vyema kuongea wakati una chakula mdomoni.

...JPM aliwanyima Asali so pamoja na kuwabana walikua wanajitutumua kuweka press na kupaza sauti zao maana walikua na njaa...now wanalamba asali, wanakula vinono vya inchi, why wahangaike?

Watanzania wanapaswa watambue siasa ni kazi km kazi nyingine, km sisi tunavyokua tunalia lia tukikosa kazi, then tukipata tunatulia, tunaacha kulalamika, its the same kwa wanasiasa...siasa ni sehemu ya kujipatia kipato na kupeleka watoto wao shule sio sehem ya kumkomboa mtu mwingine.

NB. kuna yule mpinzani kila mara alikua anaitisha press za kuelezea hali ya uchumi naona now yupo kimya km sie yeye.

angiza soda mkuu nalipia umepiga mlemle kabisa siasa ni ajira
 
Upinzani upo kwa mujibu wa katiba na kukaa kwao kimya hawajavunja katiba so waache wakae kimya.


Katiba ya Nchi haisemi wapinzani ni Ngao wananchi wajinga wasio jitambua so wawe tayari muda wote kurisk maisha yao na wakienenda kinyume na hivyo basi upinzani ufutwe.
Ikiwa kuna kifungu kinaelekeza hivyo basi utakuwa na hoja ila kama hakipo kaa kimya and enjoy the test of the food you cooked.
Kwangu mimi vyama vya upinzani kwasasa viongezewe Luzuku kwasababu zile pesa za Maroli ya kusomba polisi mara wanajeshi kwenda kuwakabiri wapinzani zipo tu hazina kazi so hizo pesa zilizokuwa zikitumika kuwalipa posho Police inabidi wapewe wapinzani kwa maana sasa wapo kimya na ndicho CCM walikuwa wanakitaka na wamekipata.


Alafu we ni Ke ama Me?.
Why unataka mwanaume/mwanamke mwenzio avunjwe mguu auawe kwa kupigania haki zako wakati wewe upo bize kutaka kujua Demonde kavaa nini?
Huu ujasiri unaupata wapi wa kuja kulaumu wapinzani?.

Ni mara ngapi wapinzani wa Tanzania wamekabiriwa kwa mkono wa chuma watawala na hamkuonyesha japo kuguswa?.

Unajua mbowe kafilisika kwa kutetea mak*ma?.
Unajua kwasasa mwili wa Lissu unamatobo kama net ya Mbu kwa kutetea wasenge ambao wapo biza kujadili Simba na Yanga?.

Wakati wapinzani wanauawa, kufungwa na kufilisiwa hamkuwai kusimama nao na mlipo ambiwa kuwa ndiyo wanaosababisha kila mtanzania asimiliki Noah ya makinikia mkashingilia, mkasema wasurubiwe ila kwasasa nao wamezisoma nyakati hawataki tena ku risk maisha kama zamani mmenza kuwachokonoa.
Most of you guys manaoanzisha nyuzi zenye taswila kama hii hamjawai hata kusawapoti wapinzani maisha yenu yote dhumni lenu kuu la kuanzisha nyuzi kama hizi si kwasababu ya masahibu yanayoikumba Tanzania bali dhumni lenu kuu ni kuendelea kufifisha upinzani ili uondelee kuonekana machoni pa watu kuwa si lolote kama wengi wanavyoamini.

TOKA NYUMA YA KEYPADS KAMA WAPINZANI WALIVYOKUWA WAKIFANYA USISUBIRI MWANAUME/MWANAMKE MWENZIO AKUPAMBANIE KESHO YAKO.

HATA CHE GUAVALA ALISHINDWA BAADA KUGUNDUA ANAEPAMBANIA HANA NIA YA KUSAIDIWA.
Safi sana ufafanuzi mzuri na majibu yaliyoenda shule haya.ASANTE.
Kwani Lissu alipigwa risasi kwa sababu zipi?
Kwa sababu ya chuki na ubinafsi wa mwendazake.
 
Unajua baada ya mateso ya 2020 nilifika sehemu nikawaza hivi kwa nini upinzani usifunge mdomo ili wote tutambue huwa wanafanya kazi gani. Hatimae wamekaa kimya sasa waTanzania tujitetee wenyewe. Wewe unataka mke wake alie tu yeye peke yake? Na watoto wake wahuzunike tu? Sasa msaada upo kwa Bwana aliyeziumba mbingu ba nchi!
 
Back
Top Bottom