Tangazo kutoka Tanzania Movie Talents

Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,864
5,672
TIMU YA TANZANIA MOVIE TALENTS KUWAKILISHWA NA JAJI SINGLE MTAMBALIKE KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU ADAM PHILIP KUAMBIANA

Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited na Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni Waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents tunapenda kutoa pole zetu za dhati kwa Wazazi wa Marehemu Adam P.Kuambia, Ndugu wa Marehemu , Jamaa, Marafiki kwa ujumla na Rais wa Klabu ya Bongo Movie, Ndugu Steve Nyerere kwa kuondokewa na Mmoja kati ya Wasanii Mahiri kabisa katika tasnia hii ya filamu nchini vilevile tunatoa Pole zetu kwa Wasanii wa sanaa ya Maigizo Tanzania na Klabu ya Bongo Movie kwa kuondokewa na Msanii mwenzao Adam P Kuambiana.

Kutokana na Msiba huo wa Marehemu Adam Philip Kuambiana, Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents unapenda kutangaza kusitisha Zoezi la Usaili wa Shindano hilo lililokuwa linaendelea Mkoani Arusha kwa siku moja kwaajili ya Kuungana na Watanzania katika Msiba huu Mkubwa ulioikumba Tasnia ya Filamu Nchini Katika kuomboleza na Kushiriki katika Mazishi ya Marehemu Adam Philip Kuambiana yanayotarajiwa kufanyika leo Jumanne tarehe 20 Mei 2014 katika Makaburi ya Kinondoni.
Kutoka Kwenye timu ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha, Timu hiyo itawakilishwa na Mmoja wa Majaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents, Ndg Single Mtambalike ambae anatarajia kusafiri kwa Ndege kutoka Mkoani Arusha kwaajili ya Kuungana na Watanzania wote na wasanii wengine katika msiba na mazishi ya Marehemu Adam Philip Kuambiana. Vilevile Ndg Single Mtambalike ataungana na Wafanyakazi wa Proin Promotions Limited waliopo jijini Dar Es Salaam katika Msiba huo.
Timu nzima ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha tunapenda kutoa Pole zetu za Dhati kwa wafiwa wote na watanzania wote tulioguswa na msiba huu wa Msanii wa Filamu Nchini Adam Kuambiana.
Shindano la Tanzania Movie Talents litaendelea kama kawaida siku ya Jumatano asubuhi kama ratiba ilivyopangwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

Imetolewa na-
Josephat Lukaza
Afisa Mahusiano - Tanzania Movie Talents
Proin Promotions Limited
 
Angalau hapa kuna press release ya maana imetolewa na watu wanaoonekana hawakukurupuka.

bado najiuliza ni vigezo gani vimetumika huyu kibaka steve nyerere ndio awe kiongozi wa bongo movie? au hawa watu wenye akili timamu kama single mtambalike hawapo kwenye chama cha bongo movie? am just curious. .....
 
Nafikiri watu wafupi wengi wanakuaga na matatizo ya u mach know
So usiahangae kuhusu uyo stivu nyerere
 
Angalau hapa kuna press release ya maana imetolewa na watu wanaoonekana hawakukurupuka.

bado najiuliza ni vigezo gani vimetumika huyu kibaka steve nyerere ndio awe kiongozi wa bongo movie? au hawa watu wenye akili timamu kama single mtambalike hawapo kwenye chama cha bongo movie? am just curious. .....

Huyo Afisa habari ni graduate wa Chuo kikuu na alikuwa na blog yake tangu chuo mpaka sasa... Atleast hawa TMT wamejielewa kuajiri proffessional na kufanya kazi kiproffesional zaidi sio kila kitu udaku.
 
nilichogunduwa hii ni company limited, mara nyingi vilaza hawana nafasi kwenye kampuni, ni share holders tu ndio king markers. hongera zao na pole kwa wale wanaoongozwa na kibaka Steve nyerere.
 
nilichogunduwa hii ni company limited, mara nyingi vilaza hawana nafasi kwenye kampuni, ni share holders tu ndio king markers. hongera zao na pole kwa wale wanaoongozwa na kibaka Steve nyerere.

Yeah kitu kuwa Ltd coy inamaana imekaa kiproffesional na kufata taratibu zote za usajili Brella na TIN number TRA. Kuliko hizo unity uchwara zisizo na mission wala vission ndio maana hawajielewi wale.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom