Tangazo kuhusu nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada kwa mwaka wa masomo 2012/201

prakatatumba

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
1,328
190
2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
(a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
(b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
(c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:

(a) Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
(b) Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
(c) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition’.

VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
(i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
(ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
(iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
(iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
(v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
(vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
(vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
(viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.

MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
Maombi yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)



source: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::
 
Back
Top Bottom