Tanganyika Majimaji, Congo Mayimayi, Kenya Maumau. Mjue Mama Onema wa kundi la SIMBA WA MULELE

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,719
10,215
IMG-20240214-WA0031.jpg

Magwiji wa Afrika walikuwa wengi tu wa aina ya Kinjekitile Ngwale...

Soma historia ya huyu mama anaitwa Mama Onema ambaye aliishi Congo na ndio alikuwa akiwakinga na Risasi waasi wa kundi la SIMBA MULELE wakipigania ardhi yao dhidi ya wavamizi Marekani na kibaraka wao Mobutu.

Mama Onema alikuwa anawatengeneza Simba mulele ukipiga risasi inateleza mwili kama maji....

Baadae Mobutu alimkamata Mama Onema na kumuua ili asirithishe utaalam huo kwa watu wengine.

Lakini inasemekana utaalam huo tayari alikuwa ameshauchukua mtoto wake mmoja na kuendelea kitoa huduma...

Kumbuka huyu mama kauawa mwaka 1965, si mbali sana kutoka hapa tulipo...

Huyu mama sababu ya kundi la waasi kujiita "mayi mayi'' hii ni lugha ya Kilingala (kikongo) ikimaanisha "maji maji" na inasemekana waasi wa kundi la mayi mayi hadi leo wanatumia dawa hii na ni lazima mwanajeshi wao achanjwe.


Nahisi maelezo hayo yamekupeleka hadi kwenye historia ya vita ya maji maji huko Songea.

Kumbuka pia mama Liti wa Singida na jinsi alivyokabiliana na wajerumani.

Afrika tuna maeneo mengi sana ya kufanya Hija kwa mitume wetu hawa.

Bahati mbaya walio wengi (kama Liti) baada ya kuuawa mafuvu yao yalichukuliwa na wajeruman na waingereza hadi leo yamehifadhiwa huko
 
Back
Top Bottom