TANGA: Rais Magufuli azindua stendi mpya ya mabasi Korogwe. Prof. 'Maji Marefu' atamani atawale miaka 20

Sasa mawaziri na RC watafungua vyoo sasa vya stand au shule!! Afanye mambo makubwa ya nchi vingine awaachie wadogo.....
 
Alafu anajinasibu kua yeye ni m bana matumizi huku anapoteza fedha za serikali kwa kufungua vitu ambayo hata mkuu wa wilaya tu angeweza kuzindua na ikatumika gharama ndogo ya Ml. 2-3

Sawa umeeleweka mwache aendelee kufanya kazi akimaliza atakusikiliza na wewe!
 
This is too cheap kwa kweli... Rais kuzindua STENDI YA MAGARI

Sawa ni cheap maana aliwaahidi na limetekelwzwa kwako ni cheap lakini kwake ni ahadi imetimizwa akimaliza kuzindua endelea kufuatilia ziara yake ujue atakua wapi tena maana alipo upo!!
 
Akiongea leo mjini korogwe katika kuhitimisha ziara ya siku 5 ya mh. Rais huko mkoani Tanga, mbunge wa korogwe 'profesa maji marefu' amesema kuwa, ipo haja katiba ya CCM kurekebishwa ili kumpa fursa mh. Rais kuongoza miaka 20 badala ya 10.

Bwana maji marefu aliongea hayo katika mkutano huo huku akishangiliwa kwa vifijo na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Je, wana great thinkers, mnaonaje, aongezewe?
tuko zaid ya milioni 45
maji marefu ni ya mto au bomba?
 
Amwachie jimbo la Korogwe atawale hiyo miaka 20 ila sio Tanzania, Tuheshimu katiba ya nchi! hawa watu wa CCM sijui wanavutishwa nini huko Lumumba!
 
Bado kidogo ataanza kuomba ni kusimamia sendoff za watu kwani ni rais mpenda kiki na miradi yote hiyo ni ya kikwete,, stendi hiyo ya korogwe ni ya muda tangu ijengwe

Ndio faida ya kuishi kwenye nchi huru, unaongea chochote unachojisikia haya andaa mwaliko atakuja kusimamia kwenye ukoo wenu.
 
Watanzania wako zaidi ya mil50, wenye ndoto na dhamira ya kufanya zaidi ya ayafanyayo wako weeeeengi mno...

Tatizo la Tanzania ni CCM, ukiitoa CCM utakuwa umetatua matatizo meeengi ya Tanzania.

CCM ikitoka madarakani hata nchi tukimpa Mzee Rungwe tu, ndani ya miaka mitano Tanzania itapiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom