TANGA: Rais Magufuli azindua stendi mpya ya mabasi Korogwe. Prof. 'Maji Marefu' atamani atawale miaka 20

Mi uchumi wangu unaendelea kuimarika kama wewe haufanyi kazi umelala unategemea uletewe hela imekula kwako

Ukiambiwa Uchumi Wa Nchi Mbovu Unafikr Wanamaanisha Wakina Bakhresa Na Mengi Hawana Pesa Au Hawafanyi Kazi Kwanza Wewe Mwanauchumi Gani Usiejali Muda Asubuh Hii Upo Jf Unapiga Porojo Mjinga Utamjua Tu Kwa Kujisifu Anacho Wakat Hata Chai Kunywa Tatizo.
 
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani Tanga leo ikiwa siku ya tano. Leo yuko wilayani Korogwe kufungua stendi mpya ya mabasi.
======

Miongoni mwa walioongea mpaka sasa ni mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani maarufu kama Maji Marefu ambae ametoa hoja ya Rais Magufuli kuongoza nchi kwa miaka ishirini kwani kumi ya sasa haitamtosha na anaeongea kwa sasa ni mbunge wa Bumbuli ambae yeye katilia mkazo hoja ya utaifa na kutoa historia fupi jinsi walivyoinyonya Afrika na kisha kuwa washirika wa maendeleo ndani ya muda mfupi.

Anaeongea kwa sasa ni waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na anasema Korogwe na maeneo ya milimani ni moja ya sehemu zinazobeba kura nyingi za CCM mkoa wa Tanga tofauti na eneo la Pwani. Amedai hata yeye kura zake za viti maalum zimetoka huko ila watu wa ukanda wa Pwani ni waswahili kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli Mkuu Yuko Sahihi Kusema Mawaziri Wake Ni Wapumbavu Km Waziri Anadai Pesa Unatoa Ww Mh Rais,ni Kweli Mh Rais Ndyo Anayetoa Pesa Kweli?
 
Bilali alikuwa hafungui vitu vidogo vidogo kama hivi. Yaani mpaka Stand ya magari!!?

Hiyo stand naona itakuwa na hadhi ya International airport!!
wee kuna muda mpaka wakasema mh anatembea na mikasi mfukoni
hata zahanati ya kijiji twende

wakili wangu Tundu Lissu
 
Hatuzungumzii Uchumi Wa Mtu Mmoja Mmoja Amka Wewe Usiwe Ni Fikra Mgando

Daaa kama hauzungumzii uchumi wa mtu mmoja mmoja ambao baadae unajenga jamii yenye uchumi mkubwa isiyo tegemezi sasa unachangia nini? haujui 100 inaanza na moja? huwezi kufanikiwa kama haujaanzia chini acha kuzingua na shule yako ya kukaririshwa
 
Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani Tanga leo ikiwa siku ya tano. Leo yuko wilayani Korogwe kufungua stendi mpya ya mabasi.
======

Miongoni mwa walioongea mpaka sasa ni mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani maarufu kama Maji Marefu ambae ametoa hoja ya Rais Magufuli kuongoza nchi kwa miaka ishirini kwani kumi ya sasa haitamtosha na anaeongea kwa sasa ni mbunge wa Bumbuli ambae yeye katilia mkazo hoja ya utaifa na kutoa historia fupi jinsi walivyoinyonya Afrika na kisha kuwa washirika wa maendeleo ndani ya muda mfupi.

Anaeongea kwa sasa ni waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na anasema Korogwe na maeneo ya milimani ni moja ya sehemu zinazobeba kura nyingi za CCM mkoa wa Tanga tofauti na eneo la Pwani. Amedai hata yeye kura zake za viti maalum zimetoka huko ila watu wa ukanda wa Pwani ni waswahili kidogo.

Wewe umi tunakujua mzungu,sema wa pwani waelewa si watu wa kudanganywa kwa pea ya kitenge na kofia na huyo mwengine apeleke hoja bungeni ya kubadilisha katiba wako wengi watapitisha tu asitafute kiki mitaani.
 
hahahahaha kwakweli tumepata rahisi ..
maneno yake sasa !!!!!
sijui kwanini watu huwa wanaenda kumsikiliza ................
wanatakikana wakapambane na hali zao huu muda wa kazi watu wapo mkutanoni na yeye anafurahia watu wote kuwepo hapo mida ya kazi dadeki zao hahaha itatuchukua miaka200 kuondokana na umasikini muda wa kazi watu wanasikiliza kejeli
 
hivi huu muda watu wanautoa wapi wa kusikiliza hii kitu mida ya kazi ?

hii ni kazi ya mkuu wa mkoa..............................................................................................................
 
Anaunguruma hivi sasa mubashara kutoka Korogwe TA, ambapo anazindua stendi ya kisasa ya magari. Anasisitiza utunzaji mzuri wa stendi hii, anawasifu watu wa korogwe kuwa ni wastaarab na wanaothamini mali na rasilimali za nchi hivyo ana imani nao wataitunza ipasavyo, anasema stendi hii imejengwa kwa ushirikiano na Benki ya Dunia kitu kinachodhihirisha kuwa Tanzania inaaminika kwa wafadhili wa maendeleo nje ya Nchi.

Anasema maduka/vibanda vyote vinavyozunguka stendi hiyo wagawiwe wafanyabiashara ndogondogo wa hapo korogwe.

stendi hii iliyojengwa kwa gharama ya tshs bilioni 4 ni stendi ya kisasa kabisa kuwahi kujengwa hapa nchini hivyo itachochea ukuaji wa uchumi na uwekezaji hapa nchini.
ENDELEA KUFUATILIA HAPA NA TBC1 KWA UPDATES
 
Vibanda vya maduka, stendi ya Korogwe ni vya wanakorogwe na si vinginevyo.Hivyo kwa wale ndg waliozaliwa na maduka na si wenyeji wa Korogwe mjiandae kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom