TANESCO Yaomba kuongeza tena bei ya Umeme kwa 68%

Hayo ndio maisha bora kwa kila mdanganyika.Nanukuu ''YAANI KIUNIT KUUZWA SH 800 MBONA BADO SO CHEAP'' huyo ndio waziri ambaye jimboni kwake yeye tuu ndio mwenye umeme halafu Serekali ndiyo inamlipia hizo bili.Mbona tutakomaa.........?
Halafu eti wafanyabiashara hawataki kulipa kodi serekali ya magogoni inachekelea au hupo kwenye kongamano la fursa Diamond Jubilee akitoka jioni utasikia kaenda Afrika ya Kati kusuluhisha.:bored::bored::bored:
 
toka mgao umeanza solar panels na generator bei juu sasa wakipandisha na huu umeme unaowaka kwa masaa kadhaa tutafika tu mwisho
 
Watz bwana haya ndo yakujadili na kuandama si siasa za zzk na cdm kuchukua all our enegy,hatuwezi ifanya serikali iwajibike kwetu tutaendelea skia kejeli za kila aina toka kwa mawaziri kama kimbachawene
 
Hivi labda me sijui hesabu, 68% ni kubwa sana kwa hali halisi ya maisha ya mtanzania. Ina maana kama nilikuwa nanunua umeme wa 10,000, saa hizi nikienda nitapata umeme wa 3,200 kwani elfu 6,800 ndo ongezeko wanalolamba?

Na hii gesi wanayoileta huku dar wanafanya nayo nini? Wanainywea chai au wanaitumia kama blower kufutia vumbi?

Nishalichoka liserikali hili, mtu ukiweza kufanya chochote fanya ili mradi usikamatwe na maisha yako yaende, ukiwasubiri hawa mabwege utakufa kabla ya wakati wako, wacha rushwa, wizi, utapeli, na yote yasiofaa yaongezeke, wameyataka wenyewe.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Vibatari na Mishumaa pia imeshapanda bei - Watanzania tukimbilie wapi sasa?
 
Hivi labda me sijui hesabu, 68% ni kubwa sana kwa hali halisi ya maisha ya mtanzania. Ina maana kama nilikuwa nanunua umeme wa 10,000, saa hizi nikienda nitapata umeme wa 3,200 kwani elfu 6,800 ndo ongezeko wanalolamba?

Na hii gesi wanayoileta huku dar wanafanya nayo nini? Wanainywea chai au wanaitumia kama blower kufutia vumbi?

Nishalichoka liserikali hili, mtu ukiweza kufanya chochote fanya ili mradi usikamatwe na maisha yako yaende, ukiwasubiri hawa mabwege utakufa kabla ya wakati wako, wacha rushwa, wizi, utapeli, na yote yasiofaa yaongezeke, wameyataka wenyewe.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums

halafu wanasema watauza umeme nje ! Mweeee !! Wananchi tunalalamikia garama kuwa ni kubwa sana, je hao wateja wa nje watakuja kweli?
 
Simbachawene atuambie kibakwe kuna uchumi gani wa wananchi wake kulipa ongezeko la 68% bei ya umeme

Kama unaona umeme ni gharama kawashe kibatari!

Kama gharama ya feli ni kubwa basi pigeni mbizi!

Ndege ya raisi itanunuliwa tu hata watanzania wakila majani!
 
Mimi sioni hata faida ya kupatikana kwa gesi zaisi ya kuwa tajirisha mabwanyenya na wapambe wao hapa!
 
Watanzania wenzangu,zamani enzi za marehemu Jamal akiwa waziri wa fedha ,wakati wa bajeti alipandisha kodi ya kinywaji aina ya CHIBUKU INAYOTENGENEZWA KARIBU KABISA NA MAKAO MAKUU YA TANESCO.Wale wazee wetu watumiaji wa chibuku walikataa kuongezewa kodi .
Walichofanya wazee wale wote kwa umoja wao walikataa kunywa chibuku.
 
Yaani watanzania mnashangaza kweli,kupandishiwa gharama za umeme kidogo tu mnaanza kulialia,naiomba serikali sikivu ya ccm ipandishe walau ifike 80% ili Tanesco waweze kujiendesha.
 
Gesi imegundulika miaka kadhaa iliyopita, na imekuwa ikitumika kuzalisha umeme kupitia makampuni mbalimbali. Niliamini sana kuwa upatikanaji wa gesi ungeleta unafuu katika kuzalisha umeme na hivyo unafuu kwa gharama za mtumiaji wa umeme. Watendaji wa serikalini walikuja na tambo nyingi tu kuwa ugunduzi huu ungeshusha gharama za umeme. Hata katika sakata la vulugu za Mtwara, hiki ndicho kilikuwa kibwagizo, kwamba gesi italeta unafuu wa uzalishaji umeme.

Kinachonishangaza mimi ni kuwa, uzalishaji wa gesi umeendelea kuongezekana na wakati huohuo bei ya umeme nayo imekuwa ikiongezeka. Sasa swali la kujiuliza, ni nani anaefaidika na gesi hii? Sasa kama gesi iliyopakana haileti unafuu wowote kwa wananchi, kuna haja gani ya kuendelea kugawa vitalu?
 
Ile mikataba inatumaliza, hata tuzalishe gas na mafuta kiasi gani, kama hatujarejea kwenye ile mikataba bei ya umeme itazidi kupanda tu.
 
Ingekuwa kule kwa wenzetu wanakojitambua,huyu waziri angeponza serikali nzima wangekuwa wanahemea uvunguni mwa vitanda vyao saa hizi.Watu wangeingia barabarani maandamano mchana na usiku huku wamebeba vibatari!
 
Mimi naishi nyumba ya kupanga, kwa sasa nalipa 16000/= kwa mwezi kwa ajili ya umeme. Kwa kupandishwa gharama ya umeme kwa asilimia 68 maana yake nitakuwa nalipa 28000/= kwa mwezi. Eeeh, mwanyezi Mungu tusaidie kumuondoa nduli CCM
 
Back
Top Bottom