Dotto Biteko Aagiza Kusimamishwa Meneja Huduma kwa Wateja TANESCO na Afisa Uhusiano wa TPDC

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
MTWARA; NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (tanesco), kumsimamisha kazi Meneja wa Huduma kwa wateja kwenye shirika hilo na kuweka mtu mwingine kufanya hiyo kazi.

Pia amemuagiza Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kumuondoa mara moja kazini Ofisa Uhusiano na kuweka mtu mwingine kwa kushindwa kufanya kazi yake.

Biteko ametoa maagizo hayo leo Novemba 14, 2023, wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Msimbati, Halmashauri ya Mtwara, mkoani Mtwara.

Amesema Meneja wa Huduma kwa Wateja Tanesco, amekuwa akitoa majibu yasiyoridhisha kwa wateja pindi wanapopiga simu kwenye shirika kupata majibu kutokana na tatizo la umeme.

“Tanesco tuna kitengo cha huduma kwa mteja , ni kweli tuna changamoto ya umeme, lakini watu wakipiga simu majibu wanayojibiwa wananiandikia meseji, wanalalamika wakisema majibu tunayopewa waziri sio yenyewe,” amesema.

Biteko ambaye alioneshwa kukerwa na mwenendo wa meneja huyo wa huduma kwa wateja amesema ni lazima watendaji serikalini wawajibike ipasavyo.

“Nimemuelekeza Mkurugenzi wa Tanesco yule Meneje wa huduma kwa wateja pale Tanesco ondoa mara moja, weka mtu mwingine,” amesema na kuongeza

“Lazima tuheshimiane kazi ifanyike, wananchi wanataka umeme, watu wanataka gesi, watu wanataka gesi ibadilishe maisha yao, hatuwezi kuja hapa tumevaa tumependeza watu wanalia shida ndogo ndogo,” amesema.

Kwa upande wa Ofisa Uhusiano TPDC, Biteko amesema ameshindwa kufanya kazi yake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa , kusikiliza kero kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya miradi ya gesi nchini.
 
Katika zama za mitandao ya kijamii, ilitakiwa Tanesco Kila Mkoa iwe na akaunti mitandaoni, ukitaka kukata umeme toa taarifa katika akaunti ya Mkoa, ikitokea dharura, toa taarifa katika akaunti ya Mkoa husika.

Sasa wananchi wanaona umeme hakuna, hawana pa kuangalia sababu ya umeme kukatika, au namna ya kuwasiliana na uongozi wa Tanesco Mkoa.

Hii inaenda kote mpaka mamlaka za maji.

Nadhani Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo akae nao, tunataka hata wawe wanakuja mitaani kwenye vikao vya serikali za mitaa, vijiji, walau mara chache kwa mwaka, mabaraza ya madiwani. Hapo ndio Wanapata link na kuyasikia ya kwenye jamii.

Wakitaka orodha ya mitaa sugu kwa kukatika umeme kwa Kila Mkoa, wafungue akaunti tu, wananchi wataitaja, pia hata Waziri atakuwa anazisoma hizo kero live kwenye akaunti ya Kila Mkoa, na anaweza kufuatilia
 
Huyo meneja wa TNESCO anastahili kabisa kuadhibiwa. Ukiwatumia ujumbe majibu yao ni yale yale kama mzaha. "Tuambie jina lako na mahali ulipo." Jibo hili ni kama roboti linajibu. kia mtu anajibiwa hivyo. Wanashindwa kuwa na watu wa huduma kwa wateja kama mitandao ya simu?
 
Cha kushangaza siasa inanguvu ktk taluma ilo linapolekea migogolo malalamiko na ugomvi na ugumu wa kazi
 
Back
Top Bottom