TANESCO toeni taarifa za kukatika umeme kwa njia ya sms kwa wateja wenu wote.

ambagae

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
3,241
1,301
Wiki hoi nimepokea sms za kawaida mbili kutoka TAMISEMI moja ikikumbusha Watanzania kuhakikisha watoto wa miaka 5 wanaanza shule za Awali na wale wenye mi 6 wanaanza darasa la kwanza. Sms ya pili ilikuwa inahimiza watoto wapelekwe shule za sekondari bila kukosa.
Cha ajabu TANESCO wana namba za simu za wateja wao lakini hawatoi taarifa za kukatika umeme kwa kutumia sms ila naona mikoa mingine wameanzisha magroup ya WhatsApp ndio wanatoa taarifa kwa wateja wao waliopata nafasi za kuungwa na group hilo. Hata hivyo siyo kila mteja wao na simu janja. Sasa ni wakati waanze kutoa taarifa za kukatika umeme kwa wateja wake kutumia sms za kawaida.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kipindi enzi za Kipara walifululiza kunitumia SMS za kuomba maoni yangu ati wafanye maboresho!😁

TANESCO wilaya,mkoa na HQ kila siku ikabidi nipige BLOCK tu.

Kazi yenu ya msingi imewashinda mnataka kuboresha nini? Hizo sms si bora mnitaarifu mnakata saa ngapi.
 
Back
Top Bottom