Tanesco mnacheza kweli

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Ninasikitika sana kusema haya nitakayoandika hapa ndani lakini ndiyo hali halisi na inanikera sana na sina budi ku-share nanyi.
Hivi kweli hadi hivi sasa bado Tanesco ina sifa za kuitwa kampuni/taasisi ya umma pamoja na ubabaishaji wa miaka nenda miaka rudi!Kwa dhamana waliopewa na watanzania hadi hivi sasa hawajapata ufumbuzi wa nini tatizo linalosababisha umeme uwepo kwa mgao?!Binafsi,naamini tatizo/matatizo wanayajua ila ni kwamba hawataki kufanya kazi ni hii ni kutokana na kutokuwepo kwa mshindani katika sekta ya uzalishaji umeme.
Yaani haiingi akilini kwa miaka yote hiyo umeme unakuwa ni kitu cha msimu wakati sayansi haiamini suala kama hilo kuwepo kwa msimu katika matumizi ukizingatia tuko katika kizazi cha sayansi na teknolojia;mbaya zaidi wamesaini mikataba na makampuni matano:Songas.aggreko,IPTL,Dowans,Richmond yote haya ili kuongeza nguvu katika uzalishaji umeme na huku ya kitu mamilioni ya Tshs kwa kazi hiyo halafu bila aibu wanasimama mbele ya vyombo vya habari wanatutangazia mgao wa umeme!!
Kuliko kupoteza fedha katika haya makampuni si bora wangewekeza katika uzalishaji wa umeme kutoka baharini;wakapate somo India kuhusu hilo.Sijawahi kusikia kina cha bahari kimepungua kama wanavyozungumzia vyanzo vyeo vinavyoandamwa na matope.
Hivi kweli,wanafanya kazi ama wanauza sura kwenye magari na majengo ya kampuni yetu ambayo wameifanya ionekane nuksi kwa watanzania na wageni wanaofikiria ni kwa jinsi gani katika hali kama hiyo waje kuwekeza nchini Tanzania huku miji/majiji yakiwa giza na kuandamwa na uchafuzi wa mazingira kwa moshi na kelele za majenerata;sijui wanategemea maisha yetu yawe vipi kiafya na kiuchumi?
Siku zote hali ya hewa ya nchi yetu wanaijua;halafu bado wanaendelea kutegemea umeme wa nguvu za maji.Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani walivyokuwa hawako serious na kazi zao ndani ya kampuni.
Nimesikitishwa sana kwa jinsi kampuni inavyoona fahari kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuutangazia umma wa watanzania ratiba ya mgao wa umeme;halafu mgao wenyewe unaendeshwa kiupendeleo.Na mfano hai,ni eneo fulani ukishuka Sinza kumekucha tangu mgao uanze hilo eneo halijawahi kukumbwa na dhahama hiyo wakati maeneo yaliyojirani na huo mtaa kila siku umeme unakatwa halafu mbaya zaidi ni usiku tu.
Na niamaini tangu uhuru hadi hivi sasa hawana kitu cha kujivunia kimaendeleo katika nchi hii tangu wapewe majukumu ya kuwa kampuni pekee inayozalisha umeme hapa nchini Tanzania.
Ni kawaida kwa mtu mwenye akili zake timamu kuweza kuchagua na kukikubali kitu kizuri na kukataa kibaya.Binafsi,siwakubali hata kidogo katika utendaji wa kazi zao hadi hivi sasa.
 
Imefika mahali, kero kama hii kutokuwa kero tena! Milango ipo wazi ya kuzalisha umeme hapo Tz. Kwa kuanzia unaweza kufuata mfano wa kijana wa Malawi ambae alikuwa na kero kama yako kama inavyosomeka katika bandiko hili.
 
Tanesco hawana shida wanawasikiliza wanasiasa (mawaziri na wabungee) na kuyumbaa na kuiyumbishaa jamii bila kujali ni wateja ama laaa...
 
Sisemi kitu manake nina hasira kweli. Mgao plus faulty siku mbili sina umeme!!
 
Mimi sijui kama ndio wale wenye dili zao za jenereta wamerudi tena kwa kasi ya ajabu kama hii. Mimi naona TANESCO wameamua kuwatesa Watanzania na serikali nayo imebariki mateso haya kwa moyo mkunjufu kabisa. Kusema kweli inaumiza sana kwa sababu biashara zetu sisi wabangaizaji zimesimama, jamani masaa kumi na mawili sio mchezo acheni kabisa
 
Naomba kwa mtu yeyote ambaye ana baruapepe(e-mail address)ya Tanesco anipatie iliniweze kuwamegea vipande vyao;wakiweza kumeza au kuteme shauri yao ili mradi nimewapa yanayonikera.
 
Jamani hivi ni kweli hakuna mtu yeyote hapa jamvini ambaye ana baruapepe za hii kampuni ambayo haina cha kujivunia tangu kuanzishwa kwake!?Maana nilipata moja info@tanesco.go.tz lakini inaonyesha kwamba haifanyi kazi japo kwenye wheel covers zao wameiandika hiyo.
 
Sie tunawavumilia, basi umeme uwepo halafu umeishiwa hujalipa kamwezi kamoja wanakuja kama nyuki kukata umeme! Hawa wako kama ATLC wafanyakazi wengiiiii utendaji hakuna...... Embu punguzeni hao wafanyakazi wasio wa lazima huko tanesco huenda hata uendeshaji wa shirika ukaboreka
 
Hatuwezi kufika mbali na Tanesco hii yenye kuongozwa na watu wasio na sifa za kuwa viongozi. Na kibaya kabisa hata wakubwa wizarani nao ni kama viongozi wa Tanesco. Hawajui wanachofanya.Tukiamua kuzalisha umeme tunaweza kuzalisha mpaka kuuza nje.
Ila kwasababu wakati kama huu hawa viongozi uchwara ndo wanapotengenezea pesa, we all suffer because of them
 
Tanesco ni kitovu cha UFISADI toka Net solution hadi kwa Vishoka wao wa mitaani,kama vile hilo shirika lina kalaana ka Ufisadi,ningekuwa mimi nauwezo hii kampuni ningeitupilia mbaali kwenye gereza la Guatanamoooo,
 
Wakuu mnafahamu mbali na matatizo yote haya, kuna charges fulani zimechomekwa kny bill?....just check invoice au receipts zenu...sasa hivi tunalipia additional charges (taxes) kama ifuatavyo;

VAT ---- ------------------18%
EWURA.............................1%
REA (Rural Energy Agency) ...3%

Total taxes on electricity --- 22%
 
Fikiria kabla ujatoa lawama.toa boriti kwanza kwenye jicho lako!!!!!investment in energy sector it is not a jokes!!!!!

nini maana ya shirika la umma,?ni kujiendesha si kwa kibiashara bali kutoa huduma ikitegema rukuzu kutoka serikalini,wakulaumiwa siyo Tanesco ni serikali kupitia WIzara husika.MD wa Tanesco yuko answerable kwanani,board ya tanesco,Rais au Waziri wa Nishati na madini.

Lets us be realistic which will lead the nation to the comprehensive soln to our problem not only energy sector.
 
Tanesco wametangaza nafasi ya kazi ya Mkurugenzi. Naamini kutokana na mchakato huu, watafanikiwa kupata mtu saafi zaidi, mzalendo.
 
SHAME ON U TANESCO!! Manake hata sijui niseme nini! Tumeishasema vya kutosha ila ndio hivyo watanzania kazi yetu kusema na kulalamika tu kwenye magazeti na blogs. Hivi mnakumbuka Wazimbabwe wakati fulani walipandisha bei ya mkate kulitokea nini?? Anayekumbuka aseme hapa. Sasa sisi Watanzania kama kawa talk, talk, talk, complain, complain, complain BASI. Hivi kweli tuta-achieve tunayoyataka kwa kulalamika kwenye internet na magazetini??????????????
 
Watanzania tuamke, tuanze kwa kuwang'oa wanasiasa wanaowakingia vifua hao watendaji wabovu wa TAHA NEISCOL hlf baada yao ndo tunalitaifisha hilo shirika feki na kuwapa tenda wazalendo wenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa njia mbadala walete umeme hata ikiwa ni kwa gharama za juu lakini uwe wa uhakika!
 
Fikiria kabla ujatoa lawama.toa boriti kwanza kwenye jicho lako!!!!!investment in energy sector it is not a jokes!!!!!

nini maana ya shirika la umma,?ni kujiendesha si kwa kibiashara bali kutoa huduma ikitegema rukuzu kutoka serikalini,wakulaumiwa siyo Tanesco ni serikali kupitia WIzara husika.MD wa Tanesco yuko answerable kwanani,board ya tanesco,Rais au Waziri wa Nishati na madini.

Lets us be realistic which will lead the nation to the comprehensive soln to our problem not only energy sector.
Hawa hawawezekani wewe si ulisikia jana taarifa ya habari wanasema mtambo wa tegeta umeshindwa kuwashwa mapema kwa sababu vifaa vilikuwa vimekwama bandarini, what a joke. ingekuwa ni gari ya mke wa waziri ingepigwa simu tu bandarini ikawa cleared in one dday lakini vifaa vya umeme hadi nchi inakuwa na mgao mkali eti vifaa vimekwama bandarini, kweli lack of priorities.
 
Back
Top Bottom