TANESCO: Hamna mgao wa zaidi ya saa 12, yasema labda iwe hitilafu ya miundombinu. Bwawa la Nyerere kuanza majaribio January

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Msemaji wa shirika la umeme nchini TANESCO Kenneth Boymanda amesema hali ya uzalishaji wa umeme imekuwa ikibadika hasa umeme wa kutumia nguvu za maji na kupelekea upungufu na kulazimika kugawa umeme ili kiwango kinachozalishwa kifanane na mahitaji.

Boymanda amesema inapotokea hitilafu kwenye mitambo ya uzalishaji inaongeza shida ya upungufu na kupelekea malalamiko kwa baadhi ya wadau kukatiwa umeme japokuwa hawakuwa kwenye ratiba.

Pamoja na hayo, Boymanda amesema hakuna ratiba ya ukataji wa umeme inayozidi masaa 12 au mgao wa siku 2. Amesema jambo linaloweza kutokea ni njia ya kupeleka umeme kupata hitilafu lakini sio mgao wa umeme kutokana na mapungufu ya uzalishaji.

Tanesco imesema uhakika wa umeme upo kama Serikali ilivyosema na uingizaji wa mashine ya kwanza ni January na uzalishaji wa majaribio unaanza mara moja mashine ikifika.

 
Umbwa kabisa, hapa kwangu umeme ulirudi saa 9 usiku na umekatwa saa 12 alfajiri, jana kutwa hapakuwa na umeme, narudia umbwa kabisa
 
Back
Top Bottom